Siku ya Sheria: No mention of Tundu Lissu!, Je ni amesahaulika tu kutajwa, amepuuzwa au ameepukwa?!.

The Valiant

JF-Expert Member
Aug 16, 2017
2,828
2,000
Akhsante kwa pongezi zako ila nadhani utakuwa ni ' Mgeni ' Kwangu kwani nilishasema humu siku nyingi tu kwamba japo Mimi ni Mshabiki na Mpenzi wa CCM ( Ingawaje Kadi ya Chama bado sina ila nipo mbioni kuishughulikia niipate ) ila sitokuwa ' Mnafiki ' kwa Kuisifia CCM hata kama naona ' wamekosea / wamekengeuka ' bali nitawasema ili wajitathmini na wajirekebishe lakini pia nilishasema kwamba japo napenda ' Changamoto ' ambazo Vyama vya Upinzani nchini hasa vya CHADEMA na CUF dhidi ya Chama Tawala cha CCM ila hata wao pia ( CHADEMA na CUF ) nao wakienda ndivyo sivyo basi kama kawaida yangu sitonyamaza ' Kuwananga / Kuwasema '.

Siku zote ' msimamo ' wangu wa Kisiasa hasa hizi za Tanzania nitabakia kuwa ' neutral ' na nadhani siku zote GENTAMYCINE nipo hivyo humu na ndiyo maana unaweza kuona nakubalika na Watu wote wawe wana CCM wenzangu na hata ' Watani ' zangu CHADEMA na CUF. Hata CCM, CHADEMA na CUF wakifanya jambo chanya / jema mbele ya Jamii ya Kitanzania basi nitakuwa wa Kwanza kuwapa Sifa / Kongole zao bila hiyana.

Tanzania Kwanza, Vyama vya Siasa na Siasa baadae na hata ' tugombane ' vipi ila Sisi sote tutabaki kuwa Watanzania tu.
Nadhani wewe na Barbarosa mngefuatilia siasa za kwenu rwanda
 

MZEE MSASAMBEGU

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
2,785
2,000
Haaahaaaaa ndo maaa nikakuambia mchawi hawez mwona mwenzie mpaka..........! Kama nina matatizo ya akili basi ulianza wewe nenda katibiwe wewe kabla intensive mental haijakukuta! Wahi kungali zinakutosha bado usije ukatembea uchi badae barbarani!
Mi ni daktari wa magonjwa ya akili yanayowasumbua watu kama wewe....kumbe ushaanza kutembea uchi barabarani mkuu???
 

WILLIAM MARCONI

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
2,056
2,000
Wanabodi,

Leo nimepata fursa kuangalia sherehe za maadhimisho wa siku ya sheria zilizokuwa zikitangazwa live na TBC. Chama cha wanasheria ni mdau muhimu wa maadhimisho haya ambayo huhutubiwa na rais wa chama hicho. Kwa vile rais wa TLS ni Tundu Lissu, na ameshindwa kuhudhuria kutokana na kuwa mgonjwa, jina la Tundu Lissu, halikutajwa popote!. Swali la kujiuliza, ni kutotajwa huku kutokana na kusahaulika tuu, Lissu amepuuzwa as if he doesn't exist, or ameepukwa kutajwa kwa makusudi?.

Kwenye ratiba ya maadhimisho hayo, kulionyesha kuna mahali rais wa TLS, angepaswa kutoa salamu. Kwa vile rais wa TLS, Mhe. Tundu Lissu, ni mgonjwa kwa shambulio la risasi, aliyekuja kuzungumza nafasi ya rais wa TLS, ni Makamo rais wa TLS, nikitegemea, alipoanza kuzungumza, kwa vile aliyepaswa kuzungumza sii yeye ni rais wa TLS, hivyo anaongea kwa niaba ya rais wa TLS, then, kistaarabu tuu, alipaswa kusema anazungumza kwa niaba ya rais wa TLS ambaye ni mgojwa. Huyu Makamo rais wa TLS, aliposimama kuzungumza, alisimama na kujitaja kuwa anazungumza kwa niaba yake!. Ratiba inasema mzungumzaji ni rais wa TLS, wewe sio rais wa TLS, unasimama kuzungumza badala ya rais wa TLS, ilibidi kumtaja rais wa TLS as an excuse ndipo uendelee!.

Naibu Spika, Tulia Akson, amemuwakilisha Spika ametajwa kuwa yupo anamuwakilisha spika. Naibu DPP ametajwa kumwakilsha DPP, Naibu Mwanasheria Mkuu ametajwa kumwakilisha Mwanasheria Mkuu, kwa nini huyu Makamo rais wa TLS akajitaja yeye ili hali kwenye ratiba aliyeandikwa ni rais wa TLS.

Aliposimama mgeni rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano, naye katika maelezo yake, akamtaja rais wa TLS na kujikwaa, akamtaja Makomo rais wa TLS.

Huku kutotajwa kabisa kwa rais wa TLS, Tundu Lissu. ni oversight tuu ya kusahaulika, au ni omission kuwa Tundu Lissu asitajwe popote.

Rais katika hotuba yake, akatoa pole kwa mhimiliwa mahakama kwa kifo cha Jaji Robert Kisanga ambaye aliishastaafu siku nyingi, kama mtu aliishastaafu siku nyingi na kufariki, mhimili huu unapewa pole, vipi kuhusu shambulio la rais wa TLS ambaye hadi sasa anauguza majereha ya shambulizi, hatajwi popote, wala hata kumtakia uponywaji wa haraka!.

Amini usiamini, kama Tundu Lissu, angekufa kwa shambulio lile, hotuba ya TLS ingemtaja, na kile aliyehutubia, angetoa pole kwa TLS kwa kuondokewa na rais wake, lakini kwa vile Lissu yuko hai, amenusurika, hadi marehemu wastaafu wanapewa pole, lakini walio hai wanaohitaji kuombewa tuu uponyaji wa haraka, wamesahaulika, kama sio kuepukwa!.

Kama huku sio kusahaulika, bali ni kuepukwa, then bandiko hili, ndio taarifa ya awali, kuwa urais wa Tundu Lissu kwenye TLS, unaofikia kikomo miezi miwili ijayo, Mwezi April, 2018, wanasheria watakutana na kumfuta rasmi kazi Tundu Lussu kama rais wa TLS, na inawezekana kabisa, jina la Tundu Lissu likaingia kwenye kumbukumbu za TLS kuwa Tundu Lissu ndie rais wa TLS ambaye he did almost nothing, tangu achaguliwe, kwa kudumu kwa miazi mitatu tuu TLS, ba baada ya hapo, akashambuliwa, hivyo kumaliza Kipindi chake chote cha urais akiwa hospitalini.

Pamoja na kwamba Tundu Lissu ni mgonjwa na yuko hospitalini, bado yeye ndie rais halali wa TLS!. Kuumwa hakumfanyi Tundu Lissu asiwe rais wa TLS, hivyo he was worth mentioned, na kutakiwa uponyaji wa haraka!.

Get Well Tundu Lissu, pole sana, umesahaulika mapema!.

Paskali
Paskali wanasheria ni wapuuzi sana kuruhusu taaluma yao ikojolowe na tundulissu kujineemesha kisiasa. Walipewa nafasi ama wachague taaluma yao au wamchague Tundulissu aliyekwisha kuikojolea taaluma ya sheria. Wakamchagua tundulissu wakaamua kuikojolea taaluma yao. Haya ndiyo waliyotaka.
 

Zumbe Mtana

JF-Expert Member
Sep 15, 2011
2,598
2,000
Kilichofanywa na Spika wa Bunge, kumvua Lissu ubunge wake, sio mwanzo bali ni mwisho, mpango wa kumuengua Lissu ulianza siku nyingi kabla, uzi huu ukiwa, ni sehemu ya mpango huo.
P
Pascal Mayalla mbona unajikanganya Ngosha?

Katika uzi wako mwingine unaonyesha kwamba Spika amezingatia Kanuni na taratibu zao ambazo Lissu amezikiuka, katika uzi huu unaonyesha kwamba Huu Ni mpango Maalum ulioandaliwa toka kitambo ili kumuondolea Lissu ubunge kwa Lugha rahisi unakubali kwamba hizi ni hujuma za Makusudi kimkakati zilizopangwa kumuondolea Lissu ubunge.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,964
2,000
Leo ni Tundu Lissu day, ilikuwa arejee, leo, japo hakurejea, tunamuadhimisha kwa kumtafakari kwa sababu


Leo siku ya tarehe 7/Sept. 2019 ni siku ya kumbukumbu ya miaka miwili toka Mh.Tundu Lisu aliposhambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana. Mpaka leo bado wasiojulikana hawa bado hawatajulikana na uchunguzi mkubwa, makini na mkali wa Jeshi letu adilifu la polisi, unaendelea kuwabaini wasiojulikana hawa, hivi sasa kuna mashuhuda wawili muhimu sana, wanasubiriwa wao tuu kuhojiwa ndipo taarifa rasmi ya polisi kuhusu maendeleo ya uchunguzi huu ndipo ilatolewa.


Tuvute subra.

Get well soon Mhe. Tundu Lissu and welcome back home.

P
 

V Kweli Tupu

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
954
1,000
Wasiojulikana mpaka leo bado hawajulikani. Na wale wanaodhaniwa hawapo pia?
Leo ni Tundu Lissu day, ilikuwa arejee, leo, japo hakurejea, tunamuadhimisha kwa kumtafakari kwa sababu


Leo siku ya tarehe 7/Sept. 2019 ni siku ya kumbukumbu ya miaka miwili toka Mh.Tundu Lisu aliposhambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana. Mpaka leo bado wasiojulikana hawa bado hawatajulikana na uchunguzi mkubwa, makini na mkali wa Jeshi letu adilifu la polisi, unaendelea kuwabaini wasiojulikana hawa, hivi sasa kuna mashuhuda wawili muhimu sana, wanasubiriwa wao tuu kuhojiwa ndipo taarifa rasmi ya polisi kuhusu maendeleo ya uchunguzi huu ndipo ilatolewa.


Tuvute subra.

Get well soon Mhe. Tundu Lissu and welcome back home.

P
 

Alphonce Kagezi

JF-Expert Member
Sep 29, 2015
304
250
Neno (Wasiojulikana)lina ukakasi na lina ibua maswali mengi yasio na majibu yalio sahihi.
Kimsingi makoso ya nayohusu uharifu dhidi ya binadamu yanapotokea uchunguzi wake wakati ukiendelea neno wasio julikana lisitumiwe sana kwani hili laweza kuwa chaka kubwa la kuuficha ukweli wa tukio na kutengeneza au kupanda mwendelezo wa uharifu dhidi ya binadamu matendo ambayo huweza kutengeneza fikira Kali za chuki ndani ya jamii ama kutengeneza visasi vya kimya kimya kati koo na koo ,jamii kwa ujumla.
Sio neno zuri kulitumia (wasiojulikana)huku maisha ya watu yakihatarishwa ana kupotea
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,964
2,000
Wanabodi, mimi nilidhani Lissu hatarejea
Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela!

Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali, "Kwa Mliomsikia Tundu Lissu Kwenye Hard Talk, Jee Unadhani Atarejea Nchini?. Mimi kwa upande wangu, I seriously doubt kama atarejea, na ikitokea kweli akarejea, then Tundu Lissu atakuwa ni shujaa mwenye uthubutu na ushujaa mkubwa kuliko hata ushujaa wa Nelson Mandela!.

Nimesema hivyo kwa sababu nimemsiliza kwa makini Tundu Lissu, him being a Lawyer, kwa yale aliyoyasema, kwa tuhuma alizoshusha bila ushahidi, I seriously doubt if Tundu Lissu will ever return home during this era, na ikitokea kweli akarejea, then Tundu Lissu atakuwa ni shujaa kuliko Nelson Mandela.
Hongera zake.

Paskali
Final Update
Tundu Lissu leo amerejea nyumbani Tanzania, hivyo naomba kuthibitisha humu kuwa Tundu Lissu ni Jasiri na Shujaa Kuliko Nelson Mandela.

Hivyo sasa, kufuatia kurejea huku, ule ushauri wangu nilioutoa kwake kabla hajashambuliwa, sasa utekelezwe.

Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!

Shujaa Kamanda Tundu Lissu, karibu nyumbani.
Mungu ni mwema amekutendea muujiza, hivyo endelea kutimiza ndoto yako, Mungu aliyekuponya ni Mungu mwenye uwezo, anaweza kabisa kulifanya "Jiwe Walilolikataa Waashi, Likafanywa Jiwe Kuu la Pembeni"

I wish him all the best.
Paskali
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom