Wakuu natumaini wote wazima humu ndani,nina mpenzi wangu anasoma chuo kimoja huko mkoani mimi nipo Dar.
Usiku wa tarehe 1 nilimpigia muda wa saa 4 usiku na simu yake muda wote iliita bila kupokelewa,nilimtafuta mara nyingi na baadae nikaamua kulala,ilipofika saa 6 usiku alinitafuta na nilipomwuliza kwanini hakupokea simu alidai alikuwa darasani na aliweka simu silent coz anajiandaa na mitihani ya kumaliza semester.
Nilimkumbusha kuwa tulikubaliana asiweke simu silent na kwanini amevunja makubaliano?.Aliamua kunikatia simu na kuzima kitendo kilichoniudhi sana.Sikujali sana maana sikutaka kumkera kipindi hiki cha mitihani asubuhi nilimpigia hakupokea tena,mchana nilimpigia hakupokea na nikasema akikuta missed calls zangu atanitafuta hakufanya hivyo na mimi niliamua kukaa kimya mpaka sasa.
Kiukweli nampenda sana huyu msichana na leo nimemkumbuka sana ila sitaki kumtafuta maana nitampa kichwa kwa kuruhusu aendelee kufanya makosa zaidi,nishaurini nifanyeje pia samahani kwa kuwachosha kwa maneno mengi na naombeni msitumie matusi kuchangia maana ni vyema tukaheshimiana.