Siku ya nne sijampigia mpenzi wangu

Siku ya nne sijampigia mpenzi wangu

Kaka kubali unampenda sana huyu dada na ni wewe ndio unahangaika sasa, usisikilize maneno ya watu nakukanya, watu wapo kwenye computer zao wanakwambia endelea kuuchuna wakati wewe unaumia, wenzako wako na wapenzi wao poa tu! By the way mbona inawezekana wewe ndio umeshamwagwa hapo kaka, kwa mazingira hayo wala usilete ukidume hapo, yeye ndio hapokei simu zako na wala hakutafuti, hayo ya kusema utampa kichwa zaidi au ukimtafuta ataendelea kufanya makosa zaidi yanatoka wapi ndugu yangu, hakikisha kwanza bado ni wako ndio useme haya. Ni kama alikuwa anakutafutia sababu tu huyo na ameshakata kamba huyo kaka.
 
lete namba yake nijaribu kwa simu yangu tuone kama atapokea!!
 
Wakuu natumaini wote wazima humu ndani,nina mpenzi wangu anasoma chuo kimoja huko mkoani mimi nipo Dar.Usiku wa tarehe 1 nilimpigia muda wa saa 4 usiku na simu yake muda wote iliita bila kupokelewa,nilimtafuta mara nyingi na baadae nikaamua kulala,ilipofika saa 6 usiku alinitafuta na nilipomwuliza kwanini hakupokea simu alidai alikuwa darasani na aliweka simu silent coz anajiandaa na mitihani ya kumaliza semester.Nilimkumbusha kuwa tulikubaliana asiweke simu silent na kwanini amevunja makubaliano?.Aliamua kunikatia simu na kuzima kitendo kilichoniudhi sana.Sikujali sana maana sikutaka kumkera kipindi hiki cha mitihani asubuhi nilimpigia hakupokea tena,mchana nilimpigia hakupokea na nikasema akikuta missed calls zangu atanitafuta hakufanya hivyo na mimi niliamua kukaa kimya mpaka sasa.Kiukweli nampenda sana huyu msichana na leo nimemkumbuka sana ila sitaki kumtafuta maana nitampa kichwa kwa kuruhusu aendelee kufanya makosa zaidi,nishaurini nifanyeje pia samahani kwa kuwachosha kwa maneno mengi na naombeni msitumie matusi kuchangia maana ni vyema tukaheshimiana.
huyo tayari kashakutana na wenye boom...wanafinance breakfast,lunch, dinner and sex..so mtoe kwenye group la first lady wako to group la vipoozeo...
ila kama unhamu sana ya kupigiwa naye basi its simple jus mtumie vocher feki lazima atapiga kuuliza mbona haiingii?
 
Pole sana, huyu dada ashakuacha amepata mwingine we achana nae ipo cku atakuja gundua alikosea na wakati huo utakua ushapata anayekupenda,. Ucmpigie tena achana nae,.
 
Hebu acha ubinafsi si keshakuambia anajiandaa na pepa? Stress za nini?
 
Utapata heart attack siku sio nyingi ww, chamsingi "onyesha upendo" wako kwake mpigie ujui kipi kinacho m7bsh awe kmya huwez jua anakupima or wat....!
Na hzo sheria za kijinqa ooh usiweke silent n ujinqa mpe m2 uhuru mwonyeshe una mwamin hii kubana banwa ndo wenq wana cheat makusud bhas 2 akuonyeshe huwez kumchunqa. Kumbuka sheria zipo ili kuridhsha baadhi mambo na si kuabudiwa.. Open ur mind...
 
Wakuu natumaini wote wazima humu ndani,nina mpenzi wangu anasoma chuo kimoja huko mkoani mimi nipo Dar.Usiku wa tarehe 1 nilimpigia muda wa saa 4 usiku na simu yake muda wote iliita bila kupokelewa,nilimtafuta mara nyingi na baadae nikaamua kulala,ilipofika saa 6 usiku alinitafuta na nilipomwuliza kwanini hakupokea simu alidai alikuwa darasani na aliweka simu silent coz anajiandaa na mitihani ya kumaliza semester.Nilimkumbusha kuwa tulikubaliana asiweke simu silent na kwanini amevunja makubaliano?.Aliamua kunikatia simu na kuzima kitendo kilichoniudhi sana.Sikujali sana maana sikutaka kumkera kipindi hiki cha mitihani asubuhi nilimpigia hakupokea tena,mchana nilimpigia hakupokea na nikasema akikuta missed calls zangu atanitafuta hakufanya hivyo na mimi niliamua kukaa kimya mpaka sasa.Kiukweli nampenda sana huyu msichana na leo nimemkumbuka sana ila sitaki kumtafuta maana nitampa kichwa kwa kuruhusu aendelee kufanya makosa zaidi,nishaurini nifanyeje pia samahani kwa kuwachosha kwa maneno mengi na naombeni msitumie matusi kuchangia maana ni vyema tukaheshimiana.
Haya mambo ya kuchuniana kwenye simu, huwa nayaona kama ya kitoto. Lakini siku hizi ndio yamekuwa kama fasion. Mtu akikasirika basi the best option ni kutopokea simu. Ila sioni kama ni sawa kwa watu ambao ni matured na mnapendana kwa dhati. Mara nyingi mtatafuta suluhu, badala ya kuchuniana.
Mimi ninavyoona hapo kuna walakini kwenye mahusiano yenu. Nakushauri mpigie kama unampenda, ila nenda naye kwa umakini.
 
sidhani kama kungalipo mapenzi apo cha msingi kaa kmya na utafte altenative hapo mda si mrefu itakuwa hstoria! Kupenda si kaz ila kumpata akupendae kaka!

Mijitu yenye hekima kama hii sikujua bado ipo duniani yani hapo jamaa keshamwagwa hakuna priority kwenye maisha zaidi ya akipendacho mtu sasa kama shule au mitihani ni moto kuliko mupenzi huo ndio mwisho wa njia
 
huyo tayari kashakutana na wenye boom...wanafinance breakfast,lunch, dinner and sex..so mtoe kwenye group la first lady wako to group la vipoozeo...
ila kama unhamu sana ya kupigiwa naye basi its simple jus mtumie vocher feki lazima atapiga kuuliza mbona haiingii?
hahaaaa! Nimeipenda hii!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom