Habari wakuu,
Huu ni uzi ambao wadau wanaweza kuweka uzoefu wao ilikuaje siku ya kwanza kuingia kazini? Ulifika kazini muda gani? waliompokea walikuaje? Mambo yapi yalikufanya uzoee mazingira ya kazi haraka nk nk
Mimi siku ya kwanza kufika kazini nilifika saa kumi na mbili na dk 20, wakati muda wa kuingia kazini ni saa moja na nusu. Hii ndio ilikuwa ajira yangu ya kwanza.
Aliyenipokea na kunifundisha kazi alikuwa jamaa mmoja mhaya anaitwa Shumbusho, jamaa tulitokea kuelewana sana. Alinifundisha kazi vizuri na kunifanya nijenge kujiamini lakini kwa bahati mbaya tulikuja kugombana baada ya mwaka mmoja baada boss kuonekana ametokea kunielewa zaidi na kuanza kunipa overtime alizokuwa anapewa yeye.
Wewe unakumbuka nini kuhusu siku ya kwanza kuingia kazini?