Siku Sheikh Rocket alipiga adhana mbili ndani ya msikiti na sokoni

Siku Sheikh Rocket alipiga adhana mbili ndani ya msikiti na sokoni

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
22,454
Reaction score
32,980
SIKU SHEIKH ROCKET ALIPOPIGA ADHANA MBILI MOJA KIBLA MASJID BADAWY NA NYINGINE NDANI SOKO MJINGA KISUTU

Sikupata kujua wala kuwaza kwa bali kuwa rafiki yangu mmoja alikuwa rafiki wa Sheikh Rocket tena rafiki yake wa kukaa, kuzungumza, kutembeleana nyumbani na kula pamoja.

Huyu sahib wangu ni Mhandisi wa sifa na kajenga majumba ya yanayopamba jiji la Dar es Salaam.

Amemfahamu Sheikh Rocket Masjid Badawy yeye bado kijana mdogo.

Huyu sahib wangu wa miaka mingi toka udogoni yeye kanipa mengi ya Sheikh Rocket lakini kwa sasa napenda niliweke hili moja hadharani sote tufaidi nami sitatia mkono wangu nitakiweka In Shaa Allah kisa hiki kama alivyoniandikia:

''Siku moja, enzi za Msikiti wa Badawiy ukitazamana na soko la Kisutu, aliadhini adhana kwa ajili ya swala ya Adhuhuri msikitini.

Alipomaliza akaenda kusimama katikati sokoni Kisutu akaadhini.

Alipomaliza akawaambia watu wa sokoni: " Msishangae, nimekuja kujivua dhima, msije mkasema hamkusikia nilipoadhini msikitini.

Maana nyinyi wengine hapa hizi nyanya, vitunguu, maboga nk. ndiyo miungu yenu.

Kama si hivyo twendeni tukaswali."

Inasemekana kuna baadhi walimfuata na wakadumu na swala.
 
Haya matakataka yako unaandikaga hayana hata wachangiaji sababu ya udini wako we mzee ni mpumbavu kuwahi kutokea...
 
1. Huwa siwezi na sina tabia ya kukebehi imani ya mtu, iwe bakwata, cct, tec, pentecost, answari sunna, TECDEMA, BUDHA NA WENGNEO.

2. lakn leo nmepita kapa
 
Nilikua masasi mwaka Jana kikazi, ila nilifungua biashara yangu dar, nikawaambia wenyeji, narudi Dar kwenda kufanya biashara, lakini kama inavyofahamika changamoto za biashara. Ukifanya mzaha unakua mshirikina.
Ndipo nikapewa anwani ya kufika kwa sheikh rocket.
Maneno ya Nyangao. Nikamuona kwa mara ya kwanza na ya mwisho. Umri ulikua ushamtupa mkono. Akanifanyia Dua na kujipatia maji Nije kutumia nifikako.
Jana nimepata taarifa za msiba wake nimeumia sana. Nilipanga kurudi kwake ili kumpa mrejesho kwa Dua aliyonifanyia.
 
Haya matakataka yako unaandikaga hayana hata wachangiaji sababu ya udini wako we mzee ni mpumbavu kuwahi kutokea...
Haya matakataka yako unaandikaga hayana hata wachangiaji sababu ya udini wako we mzee ni mpumbavu kuwahi kutokea...
Yoso,
Bahati mbaya sana kuwa unaona naandika ''matakataka.''
Napenda kukufahamisha kuwa sijapata kuandika ''takataka,'' wala sijapata kuandika udini.

Nimeandika sana historia ya Waislam wa Tanganyika, historia ambayo haikuwapo kabla.
Historia hii imepokelewa vyema hapa JF.

Nimechaguliwa Mwandishi Bora Jukwaa la Historia kwa miaka miwili mfululizo 2021 na 2022.
Kwengineko nimepewa tuzo zinafika nne kwa uandishi wa historia.

Ikiwa wachangiaji hawako huenda hawavutiwi na niandikayo na huwezi kumlazimisha mtu kupenda ambacho roho yake hakipendi.

Kitabu hicho hapo chini sasa kinakwenda toleo la tano toka kilipochapwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1997.

1769028322706.png
 
Nilikua masasi mwaka Jana kikazi, ila nilifungua biashara yangu dar, nikawaambia wenyeji, narudi Dar kwenda kufanya biashara, lakini kama inavyofahamika changamoto za biashara. Ukifanya mzaha unakua mshirikina.
Ndipo nikapewa anwani ya kufika kwa sheikh rocket.
Maneno ya Nyangao. Nikamuona kwa mara ya kwanza na ya mwisho. Umri ulikua ushamtupa mkono. Akanifanyia Dua na kujipatia maji Nije kutumia nifikako.
Jana nimepata taarifa za msiba wake nimeumia sana. Nilipanga kurudi kwake ili kumpa mrejesho kwa Dua aliyonifanyia.
Shehe Rocket hajawahi kuishi Nyangao, yeye makazi yake ni Mumburu kilomita chache kati ya Nanganga na Nangoo.
 
Back
Top Bottom