siku palapanda ikilia mtu mzima money stunna nitanyakuliwa kama hivi

soma hayo maneno hapo stiil ni long process sio unavofikiri na waliokufa je !si inasemekana watafufuliwa inamaana wataendaje?

Wateule (watakatifu) waliohai na waliokufa tu ndio watakaonyakuliwa. Waliohai ambao watakuwa hawajaonja mauti ndio hao watakaokutwa wakiwa wanafanya shughuli zao za kila siku na itatokea mteule atanyakuliwa akimuacha mwenye dhambi. Wakati huo huo wafu watatoka makaburini na kupaa mawinguni wakiungana na wateule waliohai. wote watabadilishwa miili yao na kuvaa miili isiyo haribika. Kitendo hicho kitakuwa cha kufumba na kufumbua - yani ni mara moja.

Watakaobaki hapa ndio watakaopatwa na dhiki kuu na shida ya ajabu. Mpinga Kristo atajidhihirisha wazi na atatawala dunia.

Ni vizuri tukajipangia utaratibu wa kusoma na kuyaelewa maandiko. Kila asomaye na aelewe.
 
hivi huko kwa SIR GOD hakutakuwa na JAMII FORUM?? kama ikiwepo nani atakuwa moderator??? au INVISIBLE?????
 
walokole bwana!!huko mbinguni kumbe tunaenda na nguo zetu visuruali vilivyobana vinguo vifupi ,mabegi mgongoni eeee .kweli bado sana injili haijahubiriwa na yesu wenu kurudi bado sana.injili haijaeleweka watu wanakula sadaka tu

mara zote hapa ndio huwa unaniudhi...unapenda sana kujihesabia haki na ndio maana huwa naamini wewe ni Mp..re
 
Wateule (watakatifu) waliohai na waliokufa tu ndio watakaonyakuliwa. Waliohai ambao watakuwa hawajaonja mauti ndio hao watakaokutwa wakiwa wanafanya shughuli zao za kila siku na itatokea mteule atanyakuliwa akimuacha mwenye dhambi. Wakati huo huo wafu watatoka makaburini na kupaa mawinguni wakiungana na wateule waliohai. wote watabadilishwa miili yao na kuvaa miili isiyo haribika. Kitendo hicho kitakuwa cha kufumba na kufumbua - yani ni mara moja.

Watakaobaki hapa ndio watakaopatwa na dhiki kuu na shida ya ajabu. Mpinga Kristo atajidhihirisha wazi na atatawala dunia.

Ni vizuri tukajipangia utaratibu wa kusoma na kuyaelewa maandiko. Kila asomaye na aelewe.

Tupia basi nukuu ili tuoanishe.........!! au ni maoni tu, tumpelekee Jaji Warioba ?
 
Kuna wengine wanasema wao watarithi majumba, wakati sisi tumenyakuliwa mawinguni kumlaki BWANA wetu YESU KRISTO
 
Tupia basi nukuu ili tuoanishe.........!! au ni maoni tu, tumpelekee Jaji Warioba ?

1 Wathesalonike 4: 15 .... sisi tuliohai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake BWANA , hakika hatutawatangulia waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko na sauti ya malaika mkuu na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tuliohai, tuliosalia tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani.

1 Kol 15: 51 - 54 - Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalalala sote, lakini sote tutabadilika. Kwa dakika moja, kufumba na kufumbua wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa wasiwe na uharibifu nasi tutabadilika. Maana shart huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.

Umeelewa hapo? Haya si yakupeleka kwa Warioba ni ya kujifunza na kuzitambua nyakati na maisha yajayo.
 
Back
Top Bottom