Siku nne tu!

micka jac

Member
Joined
Apr 4, 2014
Posts
49
Reaction score
20
Habari za asubuhi, ni siku nne tu ndizo zilizobakia. Kiukweli inaniathiri kwa mawazo niliyonayo. Nimesoma kwa shida hapo awali na leo mwishoni nafikia kukata tamaa kwa kukosa kulipia mtihani. Tarehe 31 ndio mwisho wa kulipia. Sijui nini hatma yangu kiukweli. Wapo walioniambia najidhalilisha na wapo waliotaka niwape reference number lakini kimya mpaka leo. Wacha nijidhalilishe kwakuwa ni mhitaji kweli. Na laiti ningekuwa wa kudanganya nisingekuwa naendelea kujidhalilisha kama wengi wasemavyo. Nina shida kweli ndugu zangu. Endapo nikishindwa kati ya siku ya leo au kesho, sitaweza tena. Nawaomba kwa dhati ndugu zanguni... Nawaomba sana.
 

yaani katika sehemu zooote wewe umekuja kutumbukia MMU?!!!!...nina mashaka huenda bumu lote wametafuna wadada.
 
hivi kwanini shida hazina adabu,ah pole mwaya
 
Unatakiwa ulipe sh ngap..na tayar una sh ngap!
 
Reactions: Mbu
Unasoma wapi? hitaji lako kamili ni sh.ngapi? shule yenu ina phone number? sio mobile. kwa sasa uko wapi?
 
Reactions: Mbu
Kama uko serious tuma account number ya shule pamoja na student number pamoja na kiasi unachodaiwa.... vinginevyo sahau!

Niko serious, ila ulipiaji wake inatakiwa niambatanishe reference number pamoja na form ambayo nilifanyia mtihani wa kidato cha pili. Na jinsi ya ulipiaji wake una hatua kadhaa.
1. Unalipia katika ofisi za posta.
2. Unarudi na risiti mpaka shuleni. Kisha umasajili masomo unayofanyia mtihani.
3. Unasubiri form isainiwe na mkuu. Na hatua ya mwisho ni kuirudisha katika ofisi za posta kwa ajili ya kutumwa baraza la mitihani (NECTA). kwa hakika siwezi kudanganya hata mara moja. Nimekuwa nafanya hivh tangu tarehe 8. Siwezi kuongopa kweli
 
Ni mitihani ya bodi au ni ipi?Pole sana jmn,ningekuwa na uwezo ningekusaidia
 
elfu 57 ila nina kiasi cha elfu 30.

.....dahh, pole sana dogo.
Shida hazina adabu, usojiumize sana kichwa na maelezo marefu.

Elfu 57/= yaonekana kidogo kwa aliyenayo, ila ni pesa ndefu kwa asiyejua pa kuipata.
King'asti, umeandika kwa busara,
Will be back.


#MosKwito !
 
Last edited by a moderator:
Ukizaliwa mwanaume kila kitu kwako ni shida, shida huzidi zaidi ukizaliwa mwanaume kwenye familia masikini!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…