Anaweza kuwa na sifa zote hizo, wakati una muoa, lakini akishaingia tu ndani akawa pasua kichwa kuliko hata yule mwanamke uliyemtoa bar!!!acheni kudanganyana, kwenye ndoa hakuna fomula, eti akiwa hivi ndio atakuwa vile, ni kumuomba Mungu tu!!
Kuna jamaa yangu alikuwa bosi bima,(NIC) huko kanda ya ziwa alimuoa barmaid , alionekana kituko toka kwa marafiki zake, na jamaa zake, ila hadi leo wana zaidi ya miaka 15 na watoto 3, na wanaishi maisha ya amani na raha, wale wenzake sasa waliooa wasomi, wengi wao sasa wana ndoa zaidi ya 3!!!