Siku mbaya JF

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,212
Reaction score
871,650
Huanza kama utani kabisa na bila kutarajia ni kama ajali isiyo na kinga hukuipanga wala kutarajia
Siku mbaya JF inaweza kukuta kwenye post! Unaweka uzi wako mzuri tu halafu anakuja mtu huko na stress zake ama hater na kuanza kukuchokonoa
Ama kwenye uzi wa mtu mwingine wewe ukiwa mchangiaji tuu.. Anajitokeza hater ama mtu mwenye stress zake na kuanza kukuchokona alimradi tu ukasirike umseme maneno mabaya akuripoti uchezee ban

Siku mbaya JF jitahidi sana usichokozeke
Siku mbaya JF jiyahidi usikwazike
Siku mbaya JF jitahidi usimjibu mtu vibaya
Sana sana unachoweza kufanya ni kumripoti
Sana sana unachoweza kufanya ni kumtupa kwenye ignore list na kumpuuza mazima, kumpotezea na kumnyamazia asije akakuharibia siku yako kwenye mengine

Wapo watu ukiwashinda kwenye hoja moja wanakurudia na ID nyingine
Wapo watu wapo hapa kwa ajili tu ya kusumbua wengine
Wote hawa ni wapuuzi wakupuuzwa na kutupwa kwenye jalala la ignore list

Kuna kukubaliana kwenye hoja ama kutokubaliana! Ikifika hatua hiyo hakuna haja ya kupotezeana muda mnakubaliana kutokubaliana

Maisha ni mafupi kuanza kukasirikiana na watu usiowajua hata sura!
Wapuuzi hawajibiwi lakini ikibidi hujibiwa sawasawa na upuuzi wao

Je ulishawahi kuwa na siku mbaya JF? Ulitoka salama?[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Me ninao watatu nishawatupia kwenye ignore list

Gents
Hyperkid
Mpwayungu
Kila mmoja na sababu zake ingawa nimegundua nisiwe serious sana nita wa unblock muda sio mrefu michango yao haiathiri maisha yangu labda kisaikolojia ni kama kuvunjiwa heshima hii ipo sana jf ya siku hasa sisi vijana tunajisahau kama tupo na nyie wazazi wetu wazee wetu


Ila wengine wote sina baya nao sana sema mi nisichopendaga kaka mshana ni ile kufanyiwa bullying mfano mshana wewe unajua changamoto zangu labda za ulevi muda mrefu sasa sipendi kuja kutegemea kwenye uzi mwingine usio na hoja zA pombe nikute labda umenitaja kama kufukua kaburi me napenda jf mpya kila siku ya kujadili hoja japo na mimi pia nina mapungufu asante kunikumbusha nijitahidi nisimkwaze mtu mwingine.
 
nilipo natembelea ban kwa madaha na mikogo kama yote sina gubu wala nini,
bwenyenye flani hivi aliniripoti 😜
 
asante kunikumbusha nijitahidi nisimkwaze mtu mwingine[emoji419][emoji375][emoji1545]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo nilivyokukera kumbe niliharibu siku yako mkuu wangu, nisamehe sana!
Hatujawahi kuwa na baya kivile mkuu wangu! You have my respect [emoji1545] kutofautiana hoja na mitazamo ni jambo la kawaida na kuna maeneo huwa tunakubaliana kutokubaliana [emoji3][emoji1545]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka sasa nishakula bann mbili
Ila kuna hawa members kama GENTAMYCIME GENTAMYCINE Mpwayungu Village FaizaFoxy ndo wanaongoza kwa siku mbaya umu jf
AlhamduliLlah sijawahi kuwa na siku mbaya, siku zote kwangu ni siku kama siku nyingine.

Imani za kichawi na kishirikina zenye kuamini kuna siku mbaya na nzuri.

Muujiza wa idadi katika Qur'an

Neno "shahr" (mwezi) limetajwa mara 12 katika Quran, kama vile idadi ya mwezi ilivyo katika mwaka.

Neno "yawm" (siku), kwa umoja, limetajwa mara 365 katika Quran, kama vile idadi ya siku katika mwaka.

Neno "ayyam" (siku), kwa wingi, limetajwa mara 30 katika Quran, kama vile idadi ya miezi ilivyo katika mwezi.

Mfano mwingine:

Neno "salawat" (sala) limetajwa mara 5 katika Quran, na idadi ya sala za kila siku lazima kwa kila Muislamu ni: A- Subh, A-Duhr, Al-Asr, Al-Maghrib, Al-Isha.

Soma zaidi: The miracle of numbers in the Quran - FUNCI - Fundación de Cultura Islámica
 
Hatujawahi kuwa na baya kivile mkuu wangu! You have my respect [emoji1545] kutofautiana hoja na mitazamo ni jambo la kawaida na kuna maeneo huwa tunakubaliana kutokubaliana [emoji3][emoji1545]

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilikuwa natania mkuu, hakuna aliyenikera na sijui kama nimekera mtu though najua kuna miandiko huwa haipendwi by default.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…