Siku kama ya leo 1995, Serikali ya Mkapa ilimtia msukosuko Dkt. Remmy Ongala kwa wimbo wake kuhusu Mwenyekiti wa CCM

Huu wimbo kabla Mrema hajahama chama.

Hapo alikua waziri wa mambo ya ndani na naibu waziri mkuu katika serikali ya Mwinyi..
Wengi wamesahau au pengine wengi walikuwa wadogo.

Bunge lilikuwa la chama kimoja, lakini Mrema alikuwa siyo mpiga meza kama hawa wa sasahivi.

Kuna kitu kinaitwa “kusimamisha shilingi”, Mrema alikuwa akifanya hivyo, yani kukataa hoja/muswada usipite bila maswali muhimu kujibiwa. Kwa nyakati za chama kimoja, hilo lilikuwa jambo la ajabu sana kwasababu wote walikuwa kama rubber stamp tu.

Kwakweli Mrema was a “fiery brand politician”
 
Kaka sidhani kama uko sahihi siku kama ya Leo huo mwaka Mkapa hakuwa na serikali ata urais alikuwa bado
Mwinyi alikuwa ndo anamaliza muda wake
Unajua uchaguzi ulifanyika tar ngapi huo mwaka na mkapa aliapishwa lini kuwa rais baada ya kushinda urais?
Je 27 /10/1995 alikuwa tayari ni rais?
Baada ya kuwa rais
 
Waligeukana na Mabere Nyaucho Marando. Wakati huo nilidhani kuwa Marando alitumika na ccm zaidi. Kulitokea mgogoro mkubwa sana ambapo kikao kikaitishwa kule Raskazone Tanga, ambapo Mrema alitolewa bastola wakati wa kikao ikabidi walinzi wake wamfiche chini ya meza.

NCCR Mageuzi ikauwawa rasmi, chama kikaanza kukosa mwelekeo. Kikagawanyika, baadaye akaunda TLP.

Nadhani alipoona uzee unakuja na hitaji la matibabu ya maradhi yake, akaona ni bora alambe miguu ya viongozi wa serikali ili asinyimwe mafao yake na kulipiwa matibabu yake. That’s my guess.
What the hell is he suffering from? He is scary. Mrema hakuwa mla rushwa nchi ingenyooka hii.
 
Pengine ulikuwa mtoto mdogo i don’t know. Lakini Mrema alitingisha mbaya kabisa. Yeye ilikuwa ni a one man show.

Nyomi yake ya kufa mtu hata hawa UKAWA sidhani kama wanafikia.[/QUOTEAchankabisa ninkura yamhu ya kwanza Mrema.alishinda
 
Wimbo umejaa mahitaji ya watu na kero ambazo Leo rais Magufuli a najitahidi kupambana nayo Hongera Magufuli rais wa wanyoge
 
Wimbo huo naupataa sana, kuna sehem anazungumzia tume ya mil .12 kuchunguza upotevu wa mil.4
Tume inachunguza uadilifu/integrity ilikuzuia vitendo kama hivyo kutokea mbeleni. Kuunda tume ya uchunguzi siyo biashara ambayo lazima ufanye cost/ benefit analysis..... tume huchunguza tabia au vitendo no matter vidogoau vikubwa ambavyo potentially vinaweza kuingiza nchi kwenye hasara
 
Siwezi kufikia kiwango cha Mrema, mrema anavyotajwa calibre yake enzi hizo na wa siku hizi itakuwa ana ugonjwa mkubwa si bure

Wanasiasa wa Tanzania Kiza kitupu.
Mrema, Lipumba, Slaa, nayule wapemba Hamad Rashid Nimechoka nao kabisa. Ni watu walaminika wanapigania haki baadae wakawa wachumia tumbo.
 
Kwa wahenga tu sikiliza wimbo wa dk remmy ongala wa -Mrema, ambao alisema kuwa ccm imemchagua fundi viatu kuwa mwenyekiti na hajui taratibu za chama,
Maneno hayo ni kuanzia dk ya 3
Pitia video


Tunaposema fisiemu haijawahi badilika watu hawaelewi... nyimbo ni zilezile matendo yaleyale...
Maendeleo hayana vyama
 
Pengine ulikuwa mtoto mdogo i don’t know. Lakini Mrema alitingisha mbaya kabisa. Yeye ilikuwa ni a one man show.

Nyomi yake ya kufa mtu hata hawa UKAWA sidhani kama wanafikia.
uwanja wa mashujaa moshi mrema alijaza watu 95 hadi arusha road ikawa haipitiki.
 
Back
Top Bottom