Philipo Kidwanga
JF-Expert Member
- Jul 12, 2012
- 2,042
- 599
utafungiaje mwanahalisi ukiacha al-huda shame on governiment.hawajui lipi lifanywe nalipi liachwe na kwa kipindi gani.... Mpaka tufike 2015, kutakuwa na migomo mingi sana kama serikali itaendelea na tabia ya kuku anakunya, bata anaharisha! Double standards! Ni kwamba watu wengi wanazidi kugundua serikali yao imeshindwa kutawala (ombwe la uongozi), imeelemewa na imekosa uongozi ktk masuala ya msingi. Matokeo yake, kila mtu anaibuka na kuanza "kuongoza" jamii au jumuiya yake kwakuwa hatuna uongozi unaotungoza watu wote kama watanzania.
Hivi ni nani anayejua kama watanzania wote watahesabiwa wakati wa sensa mwaka huu? Kuna viongozi wa dini wameshahamasisha wafuasi wao kutoshiriki sensa. Umesikia kiongozi wa juu (waziri mkuu, rais) akilizungumzia hili? Haya mabilioni yaliyokopwa ili kuendesha sensa ndo kusema yatapotea bure? Jamii zingine zinaona na kujifunza kuwa kumbe inawezekana kuidindia serikali-unategemea migomo itaisha leo?
Kuna propaganda kwamba kuna vyama vya upinzani vinachochea vurugu na uvunjifu wa amani nchini. Wafuasi wao wanapigwa na kupewa kesi sehemu mbali mbali nchini. Well and good! Lakini kwa sasa, kila mtu anajuwa kwamba kama kuna kitu kitatuletea machafuko makubwa muda si mrefu basi ni religious extremism. Serikali haioni vitisho na chuki inayotangazwa na vyombo vya habari vya kidini. Imelala. Eti ndo demokrasia. Demokrasia gani kwa vyombo vya dini lakini sio madaktari wanaodai haki zao? Kuna demokrasia gani wakati wapinzani wanapigwa, wanauawa na kubambikiziwa kesi? Double standards! Kweli binadamu anajisaidia wakati kuku anakunya!