Samahani kwa kuchelewa kujibu.
Najibu kama ifuatavyo
Rais hadi sasa sikuweza kufahamu lakini kwa tafiti zangu niliweza kujua wapo viongozi wa masuala mbalimbali nafikiri ndio watakuwa mawaziri.
Kuhusu uzuri na urembo wa mabinti/wadada wa Nibiru ni wa aina yake, nafikiri uzuri wa hapa kwao haijafikia hata 30%
Sikubahatika kushuhudia au kuona kumbi ya starehe lakini naona wana dance yao imekaa kiTurkey hivi.
Michezo mingi kwao ni kiteknolojia nilishuhudia michezo ya kushindana kasi kwa kutumia Hover Boards. Na kwa taarifa yao walitanabaisha wao ndio walioleta Hover duniani (Earth).
Kuhusu kifo kwao sikuweza kufahamu lakini naona itakuwa inachukua muda hadi kufa.
100% wanaamini Mungu na wanadai wanaamini uwepo wa Mungu aliyeumba Nibiru na Mataifa mengineyo (Planets) na viumbe mbalimbali lakini Xuzer alisema hamjui.
Kuhusu dini sikuona kabisaa lakini katika maombi kila baada ya kukamilisha jambo lao pangwa hukasanyika na kunyoosha mikono juu huku wakishukuru. (Niliona hili wakati wa kukamilisha vifaa vya usafiri wa anga.)
Shukrani kwa maswali mazuri.