Siku 28 nilizokuwa katika sayari ya Nibiru

Siku 28 nilizokuwa katika sayari ya Nibiru

isajorsergio

Platinum Member
Joined
Apr 22, 2018
Posts
4,152
Reaction score
6,601
Siku 28 zilizopita nilifanikiwa kujikuta katika sayari ya Nibiru (Sayari inayofichwa na kutoelezwa na wenye kuamini Physics)

Sayari hii ya Nibiru ni sayari yenye asili ya 'Gold Dust' muonekano wake umeelekea dhahabu, tunaweza kuona dunia ikiwa ni maji na ukijani fulani hata kwa macho yetu wenyewe (Blue, Sky Blue na Green). Ndivyo ilivyo Nibiru ni dhahabu kitaswira huku anga lake likiwa na muonekano wa Ginger Ale hivyo kufanya sayari hii kuwa (Gold, Ginger Ale, Perish Yellow na Light Orange)

Asilimia 90% ni asili ya jangwa huku udongo wake ukionekana kuwa tofauti na huu wa Dunia (Earth). Udongo/Mchanga wa Nibiru ni wa aina yake ukiinama na kuelekeza kiganja chako kwa centimeter kadhaa unaonekana kufuata mkono wako kama vile sumaku zina attract to each other.

Nibiru inawaka na kumelemeta kwa rangi mbalimbali katika viunga vyake, rangi nyingine sikuwahi kuziona hapo mwanzo, zikisindikizwa na taa ang'avu katika maeneo mbalimbali.

Nibiru kama sayari na viumbe vyake wanaamini wao ni wamoja hivyo kupelekea sayari hii kutokuwa na mataifa, nchi wala majimbo. Lakini wakiwa na eneo kuu linaloitwa NIBIRII, huu ni kama mji mkuu ambao masuala ya kiteknolojia, mawasiliano na benki imehodhiwa hapo.

Mifumo na labda nitumie neno taasisi zote zinaendeshwa na uongozi mkuu, katika sayari hii hakuna private sector wala institution yeyote. Katika sayari hii ya Nibiru kauli mbiu (slogan) ni "Cinévase" ikimaanisha "Move One" huku shughuli kuu zikiwa ni kuhusu teknolojia na tafiti mbalimbali.

Kilichonishangaza Nibiru ni viumbe mbalimbali kufanya kazi kwa umoja, mshakamano na ufanisi wa aina yake. Huku nikistaajabu kuwashuhudia wanadamu wakiwa katika maumbile ya utofauti kidogo na haya tuliyozoea maana wao wanaonekana na mvuto wa aina yake ni vigumu kutofautisha wa jinsia ya kiume na kike, huku nyuso zao zikionekana zenye furaha na tabasamu la ajabu muda wote pia inaonekana hawana chuki, ubinafsi, dharau, uongo, unafiki wala husda katika nafsi zao.

Viumbe wengine nilioweza kuwatambua kwa haraka ni Sungura, Swala, Ostrich, Paka na ndege wa aina mbalimbali. Sungura wa Nibiru wanaongea na sio tu kuongea bali huongea lugha nyingi, sungura hawa wanaheshimika kwa kiwango kikubwa sana ingelikuwa duniani basi tungelisema kwa kiwango cha Standard Gauge.

Nibiru inaonyesha hufanya kazi kwa jitahada na ubunifu mkubwa na hilo utaweza kulishuhudia ukifika NIBIRII kwa uzuri na mandhari ya maeneo yale. Mifumo ya ujenzi, usafirishaji na uchuuzi ni tofauti na kwetu (Earth), Nibiru hakuna fedha/currency yeyote wala kubadirishana bidhaa maana uongozi mkuu hutoa vitu vyote sawa kwa viumbe wote. Nilishindwa kuelewa wanatumia Ubepari, Ujamaa au Uliberali.

Nibiru jengo refu ni kama ilivyo Benki kuu ya Tanzania, hakuna rami na hutumia matofali maalum yenye nembo yao (Court of Arm).

Katika sayari hii ya Nibiru hakuna mwizi, jambazi wala kibaka na wao wanadai hawana polisi bali vyombo vya usalama kujilinda dhidi ya watu na viumbe kutoka maeneo tofauti. Nibiru hakuna mimba za utotoni katika hili nilitoa machozi na kustaajabu. Maajabu machozi hayadondoki chini wao wanakwambia ni "Move On" na furaha ni asili yao.

Siku niliyofika alikuja kijana aliyejitanabaisha kama Xuzer° Nasen aliyeambatana na sungura Zeqvi BR mwenye rangi ya Dark Tan. Binafsi nilijaribu kutumia Kiingereza nikidhani ni universal language lakini Xuzer° Nasen alinambia nitumie lugha yoyote ninayoweza kuimudu. Baada ya kujitambulisha pia nilidokeza kwa kusema "ooh napenda sungura, naweza kumbeba?" Na hapo Xuzer° Nasen akaanza nieleza kuhusu sungura kisha kumuomba sungura Zeqvi BR ajitambulishe na sungura bila hiyana alijitambulisha na kuniruhusu kumbeba huku akiniuliza masuala mbalimbali kuhusu Dunia huku akionekana kuwa na haiba ya kuongea kwa haraka lakini maneno yenye maana. Tukiwa tunatoka eneo lijulikanalo kama Artymaric Nib'Nibirii (Eneo lenye kazi za sanaa nyingi na zenye kupendeza) na hapa ndio reception.

Niliulizwa na Zeqvi BR, "Dunia inafananaje?" Kisha kunitoka na kwenda kwenye bustani yenye matunda nisiyo yafahamu nakurudi kwa kuruka juu ya mikono yangu huku akiwa na fungu (bunch) la matunda hayo madogo yenye ladha ya kipekee ambayo sikuwahi kuionja kamwe.

Nilimjibu Zeqvi BR, "Dunia ni ya tatu na ni nyumbani kwa viumbe wote ni pazuri, kiuhalisia ni ya kijani na blue kwa asilimia kubwa, na nyumbani nimewafuga ndugu zako" ghafla Zeqvi BR alinitoka na kwenda kwa Xuzer° Nasen na kuongea kwa upole "Mbona uyatendayo hayakufanani?, Itakuwaje unadai unatupenda lakini ndani umetufungia?"

Ilinibidi kusema "Hapana duniani tunaendeshwa na mifumo ya kurithishana na kukariri, binafsi nimekuta mkifungwa kwa madai ya msitoroke" na muda wote huo Xuzer° Nasen akiwa kimya.

Zeqvi BR aliuliza, "Ukifungiwa wewe usitoroke utajihisi vipi?, Kwani rafiki yako anaweza kutoroka kwako?"

Niliweza kumjibu "Binafsi napenda kuwa huru hivyo sitopendezwa na kufungiwa na rafiki yangu hawezi nitoroka maana atakuwa ananipenda na kuniamini".

Zeqvi alitanabaisha "Iwapo hutaki kutendewa jambo fulani basi jizuie usiweze mtendea mwenzako, hamna maana ya kumfungia rafiki yako ilhali unampenda nakuomba ukifika katika dunia basi wafungulie ndugu zangu na uwaeleze uwepo wangu huku"

Muda wote baada ya Zeqvi BR kuyasema hayo nilibaki nikiwaza na kufikiri jinsi raia waishio Ulaya, Asia na America wanavyo ishi na viumbe mbalimbali ndani mwao bila kuwatenga wala kuwafungia isipokuwa Afrika.

Mengine niliyoweza kuyashuhudia Nibiru ni mfumo wa kipekee na tofauti katika ufundishaji. Elimu ya Nibiru inaongozwa na kitu wanaita Fervyartc Nibiru huku elimu ikiwa na ngazi ya miaka 6 (Miaka hii ya Dunia) ambayo kwao sikufanikiwa kutanabaisha inahesabiwa vipi. Lakini kiuhalisia kuna miezi miwili inaonekana angani mwezi wa Nibiru na huu wetu wa (Moon) huu wa Moon unakasi zaidi uangaliapo angani na ukipita mara 4 hapo Mwaka umefikia tamati.

Nibiru kuna Majua manne yenye kupishana kwa nyakati tofauti na yanadhihirika yakikaribiana kwa theluthi chache mwisho wa ncha.

Nibiru hakuna kubeba daftari wala bag, shuleni projector na madaftari ni vioo vyenye rangi asili ya Gold vinavyo akisi mwanga hewani na mhusika kuchakata kazi zake mara moja. (Refer: Muziki wa RedOne, Daddy Yankee na French Montana - BOOM BOOM)

Kwa Nibiru hamna maskini, mnyonge, tajiri wala beberu. Lakini kwa uhalisia wa dunia wote ni matajiri.

Mambo ni mengi sana kiasi nashindwa hata kuyaelezea labda nikipokea maswali yenu.

Shukrani Taslim!



 
Naomba link ya movie mkuu maana nahisi hujaeleza vizuri
 
Back
Top Bottom