Sikizeni enyi masheikh na maaskofu!

Tujiulize swali fupi, kwani sie tunaotoa maoni hapa, haya maoni na mijadala hii kwa nini haikufanyika hicho kipindi cha nyuma? Je, nasi tulaumiwe kwa kukalia maoni hayo hadi leo hii?

Umenena!
 
Yote mnayosema ni ubatili mtupu! Sisi huku mitaani tunapeta tu, wakristo kwa waislamu tunajichanganya bila shida yoyote. Hao Maaskofu na Mashehe ni njaa zao tu zinawasumbua!
 
Yote mnayosema ni ubatili mtupu! Sisi huku mitaani tunapeta tu, wakristo kwa waislamu tunajichanganya bila shida yoyote. Hao Maaskofu na Mashehe ni njaa zao tu zinawasumbua!


umesema jambo moja la kweli sana; yaani kinachofanywa sana siku hizi ni kujaribu kupigania roho za maskini kwa kutumia udini. Lakini, kinachonisumbua mimi zaidi ni ukimya wa watu fulani.
 

Kumshika mkono fisadi na kumnadi kuwa panga la zamani makali yale yale

kumtetea Mkapa kwamba tumuache mzee wetu apumzike wakati wakristo kina Mpendazoe Kimaro walisimama kidete Mkapa awajibishwe

kujiuzuru Lowasa ni ajali ya kisiasa

Epa richmond tangold dowans iptl

Na madhaifu mengi yaliyo dhahiri
YOTE HAYO NI KWELI ANAPIGWA VITA NA MAASKOFU? au anajipiga vita mwenyewe hadi waumini wanaona madhaifu hayo labda wewe mpaka uambiwe na shehe hili zuri hili baya huna akili ya kupembua!

MBONA MNATUCHANGANYA?
 
......... wewe hiyo hamna ! .......... mbingu na ardhi hutetemeka kwa kumwita "mtu" ni MUNGU !!!

Dogo maalim Kombo mbona mbingu na nchi haija tetemeka na watu toka zama za mtume mpaka mtume kafa bado watu wana itikadi hivyo? na Allaah haja warudi au kwa sababu wanasema NI MTU KWELI NA MUNGU KWELI?

Achana na hizo tuungane tujadili hatma yetu na vizazi vijavyo!
 
Huu utapiamlo wa udini utaifikisha wapi Tanzania? Viongozi wa kweli wa kidini hawaweki maslahi binafsi mbele, kinachoongelewa hapa ni ubinafsi tu hakuna dini, viongozi wa kweli wa kidini hukemea maovu bila kujali nani anaongoza, uraisi wa Kikwete unamnufaisha vipi muislamu wa kawaida? Watanzania wengi wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha badala ya kuongelea masula ya kimsingi, tunakwepesha hoja na kuangelea mambo ambayo hayana maslahi kitaifa. Dini ina nafasi yake ndani ya jamii lakini ni hatari inapotumika kuendeleza maovu. Tuangalie mfano hai Tunisia waliomuondoa madarakani Beni Alli si waislamu bali watunisia waliopinga udhalimu wake. Dini na siasa haviendi pamoja, mashekhe na maaskofu/mapadri mnaotaka kujiingiza kwenye siasa vueni kanzu na majoho vinginevyo mtakuwa wanafiki.
 
Yote mnayosema ni ubatili mtupu! Sisi huku mitaani tunapeta tu, wakristo kwa waislamu tunajichanganya bila shida yoyote. Hao Maaskofu na Mashehe ni njaa zao tu zinawasumbua!

kweli kabisa..
 
Ni ukweli usiopingika kuwa watanzania wengi wamepata mwamko wa kutafuta na kuhoji mambo mbalimbali yanayoendelea katika serikali yao baada ya uongozi wa mkapa. Nadhani hii ni baada ya uhuru mkubwa wa vyombo vya habari katika uongozi wa kikwete. Katika uongozi wa Nyerere na Mwinyi hakuna anayezungumzia madudu yaliyokuwa yanafanywa na serikali zoa akiwemo mwanakijiji. Napenda kumkumbusha ndugu mwanakijiji kwamba, kabla maaskofu hawajasimama na kuomba radhi kwa kutozungumzia mauaji ya pemba na mwembechai, Wkristo na waislam wote waombe radhi kwa kutozungumza chochote katika uongozi wa Nyerere na Mwinyi, baadae ndio wakristo waombe radhi kwa kutowazungumzia wa mwembechai na pemba. Lakini, Ni kwanini waislam wanaangalia udini wa viongozi katika kukemea na wasiwakemee kama viongozi wa werikali bila kuangalia ni dini gani?? Kwanini tusiangaliane na kukemeana kama watanzania badala ya kuangalia dini zetu? Waislam ni moja ya jamii zilizoumizwa na uongozi fisadi wa mkapa, kwanini wasimkemee kama kiongozi wao wanasubiri wakristo wamkemee kama mkristo? Huu ni ujinga na udini usio na maana.
 
Kawni mwenzangu una kiwango gani cha elimu?
Tz tunatumia sheria za muingereza amabzo mtu yeyote hana hatia mpaka apatikani na kosa na mahakama (Every body is innocent until proved guilty). Ktk nchi inayofuata utawala wa sheria kama tz ni makosa kuwahukumu akina Mramba na wenzake kuwa ni mafisadi wakati mahakama haijathibitisha hilo.

Jk alichokifanya ni kuwapeleka mahakamani,tambua kuwa katika utawala wa sheria Rais hatakiwi kuingilia mahakama kwani ni mihimili tofauti.Kazi ya mahakama ni kuwahukumu. Lakini wengine wenu kwa ufinyu wa uelewa mnataka jk awaweke ndani tu kwa tuhuma,huo si utawala wa sheria.
Suala la maaskofu kumpiga vita jk hilo sio siri kwani hatuishi mbinguni tunaishi hapahapa tz tunapata habari yanayoongelewa makanisani,kumbuka tuna mchanganyiko wa familia moja kukuta waumini wa dini mbalimbali hivyo kuna mambo ambayo ni vigumu ndugu yako wa damu kukuficha hata kama mko dini tofauti.Mbona sijawahi sikia maaskofu wakisimama na kusema kuwa Mkapa ashitakiwe kwa makosa aliyofanya akiwa Rais?
 

Kwa mtizamo wangu "Ni heri kinachoua MWILI ambao hata hivyo UTAKUFA kuliko kinachoua ROHO ambayo haifi". SUALA LA USHOGA AMBALO MAASKOFU WANALIFANYA HATA HAPA TANZANIA LINAUA ROHO KWA KIWANGO KIKUBWA HASA KATIKA MAZINGIRA AMBAYO WANAWAKE NI WENGI KULIKO WANAUME.
Pia suala la kuushabikia mzinzi na Mwasherati kama ilivyotokea kwa Dr. Slaa linawatoa kabisa kwenye kushulikia Roho na Ufalme wa Mbingu kwa Ujumla. Kwa hiyo kundi la MAASKOFU linabaki kuwa ni kundi MASLAHI TU. Ndiyo maana wanaanaglia sana opportunity ya nani yupo Madarakani.
Kwa upande wa MASHEIKH wao wako zaidi katika kutengeneza ROHO zaidi kuliko masalahi. Mfano ni pale walipofanikiwa kuwaandaa waumini kumpinga MWINYI katika suala la Kondomu hata ikifikia kumpiga. Suala la Hamisi Dibagula ni mfano mwingine na Mabucha ya Nguruwe. Na pia wameonyesha kutomshabikia Dr. Slaa hasa kutokana na Tabia yake ya Uasherati. Katika suala la maslahi nadhani masheikh yapo mambo muhimu yakitekelezwa hawana tatizo na utawala uliopo hata kama ni dhalimu. mfano ni OIC, Kadhi n.k. Kwao wao IMANI inatangulia halafu Usalama wa Nchi kisha Utawala. Kwa MAASKOFU wao Maslahi ya kanisa kwanza, Utawala, imani si suala lenye kipaumbele - kila mtu aende kivyake halafu mwisho ni usalama wa nchi.

Na hapo ndipo tofauti inapokuja kati ya MASHEIKH na MAASKOFU.

Maswali ya Msingi:
1.0 Nini jukumu jukumu la Masheikh na Maaskofu?
2.0 Ya Kaisari mpe Kaiasari na ya Mungu mpe Mungu inamuhusu nani??
 
Mipishano ya mawazo at a manageable level huleta maendelea , hivyo JK awahi kuyaweka sawa haya makundi ya maaskofu na Mashehe/Imaam kabla mgogoro haujafika hatua ya pili (i.e unmanageable). Katika hatua hii ya awali naamini ataweza kupata suluhu ya kwanini kundi moja linawanyima haki zao wengine (kama ni kweli , maana kama ni hivyo hata JK anakosa hizo haki) etc
 
ndugu zangu,

nimeisoma hii thread lakini nadhani kuna kitu bado sijaelewa vizuri. tukisema maaskofu tunajua ni kiongozi wa taasisi fulani katika dini za kikriso na ama anachaguliwa kidemokrasia au anateuliwa kwa vigezo fulani.

hawa mashehe ni kina nani? wanaongoza taasisi gani? wanapatikanaje? wanasomeaje huo ushehe? kama wanaongoza taasisi fulani je zinatambulika na serikali na jamii? je, inawezekana muislamu yoyote akavaa kanzu na barakashehe akajiita shehe, na tukalazimika kuchukulia kauli yake kwa uzito sawa na ile ya Pengo au Laiza?
 
Kwa mtizamo wangu "Ni heri kinachoua MWILI ambao hata hivyo UTAKUFA kuliko kinachoua ROHO ambayo haifi". SUALA LA USHOGA AMBALO MAASKOFU WANALIFANYA HATA HAPA TANZANIA LINAUA ROHO KWA KIWANGO KIKUBWA HASA KATIKA MAZINGIRA AMBAYO WANAWAKE NI WENGI KULIKO WANAUME.
Pia suala la kuushabikia mzinzi na Mwasherati kama ilivyotokea kwa Dr. Slaa linawatoa kabisa kwenye kushulikia Roho na Ufalme wa Mbingu kwa Ujumla. Kwa hiyo kundi la MAASKOFU linabaki kuwa ni kundi MASLAHI TU. Ndiyo maana wanaanaglia sana opportunity ya nani yupo Madarakani.
Kwa upande wa MASHEIKH wao wako zaidi katika kutengeneza ROHO zaidi kuliko masalahi. Mfano ni pale walipofanikiwa kuwaandaa waumini kumpinga MWINYI katika suala la Kondomu hata ikifikia kumpiga. Suala la Hamisi Dibagula ni mfano mwingine na Mabucha ya Nguruwe. Na pia wameonyesha kutomshabikia Dr. Slaa hasa kutokana na Tabia yake ya Uasherati. Katika suala la maslahi nadhani masheikh yapo mambo muhimu yakitekelezwa hawana tatizo na utawala uliopo hata kama ni dhalimu. mfano ni OIC, Kadhi n.k. Kwao wao IMANI inatangulia halafu Usalama wa Nchi kisha Utawala. Kwa MAASKOFU wao Maslahi ya kanisa kwanza, Utawala, imani si suala lenye kipaumbele - kila mtu aende kivyake halafu mwisho ni usalama wa nchi.

Na hapo ndipo tofauti inapokuja kati ya MASHEIKH na MAASKOFU.

Maswali ya Msingi:
1.0 Nini jukumu la Masheikh na Maaskofu?
2.0 Ya Kaisari mpe Kaisari na ya Mungu mpe Mungu inamuhusu nani??

3.0 Kilele cha USOMI (DR, Masters, PHD) ni mtu kuwa Shoga , Basha, au Mwasherati?
4.0 Je, Watanzania tunaona fahari ya kuwa na viongozi wa kiimani wa aina hii?
 

Mashiekh wanasoma elimu ya kiislamu hadi kuqulify kuwa sheikh,lakini haitoshi kusoma tu bado jopo la Masheikh linalotambuliwa na waislam linawapitisha kwa kufanya mtihani maalum wa usheikh.Ngojea nikupe kidogo taaluma za walioshiriki kuongoza tamko hilo.
1.Sheikh Profesa Juma Mikidadi (PHD)
2.Sheikh Kundecha.Degree ya Dini
3.Sheikh Aba Saleh.Degree ya Dini pia na Diploma ya ualimu wa sekula
4.Sheikh Al Hadi Musa.Degree ya Dini
5.Sheikh Dr.Hamduni Suleiman Degree ya Dini na( PHD) South Africa
6.Sheikh Dr.Tego.Degree ya Dini na (PHD) Muslim College London
7.Shiekh Juma Doga.Degree ya Dini Madina University
8.Sheikh Muhammad Idd.Degree ya Dini
NEED I SAY MORE?
 

Weweee, Acha ujuhaaa! Marehemu Fares Kabuye akiwa bungeni alikataza hii kitu!

Jokes!
 
Kadogoo,
Wito kwa maaskofu kuomba msamaha kama sharti la muungano kwa madai ambayo uhalali wake si thabiti ni kigingi kingine kufikia muungano huo. Viongozi wa dini kwa pamoja wakate shauri kuomba msamaha kwa kunyamazia uovu kisha waazimu kuanza safari ya pamoja ya matamko dhidi ya uovu. Kama viongozi wa dini wote kwa nyakati tofauti wanaamini kuna vitendo vya upendeleo ambavyo vilitendeka au vinatendeka kutokana na kiongozi wa nchi aliyekuwepo au aliyepo madarakani bila shaka udhaifu wa udhibiti wa mamlaka ya kiongozi mkuu unajipambanua kwa uwazi zaidi. Matamko ya pamoja yatazika hisia za hatuko pamoja na katiba mpya itadhibiti mwanya kwa watawala kupenyeza upendeleo.
 
 

umekuja vizuriii mwishoni umejchanganya

Huyu askofu au shehe katiba ya nchi inamruhusu kushiriki siasa
Pia ni kiungo kati ya binadamu na Mungu.

Utamkwepea wapi mtu wa dini
Hata siku moja Huwezi kumkwepa!
Mwizi unapo mkemea wewe ni mwizi acha Wizi sidhani kama atafurahi mwanangu.

Ukisikia kelele vueni majoho ujue hapo fisadi limebanwa kiukweli

siasa haina unifomu eti joho kanga au suti pia haina ubaguzi wa aina yeyote

Tumeanza kukua sasa mwanangu!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…