Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,021
- 156,477
Weka picha mkuu
Fikiri mimi maskini,
Uvivu wangu nyumbani,
Ukiwa huu njiani,
Nakufa hapa kwa nini?
Sadiki sasa ashiba,
Chakula kingi kwa baba,
Nirudi tena kwa baba,
Nakufa hapa kwa nini?
.............................................
.................
Naomba radhi nimekosa,
Nitakuwa mtoto mwema sasa,
Shambani tena sitakosa,
Baba na mama nisameheni.
Nitalima kama Sadiki,
Nitalima wala sichoki,
Na nyumbani tena sitoki
Baba na mama nisameheni.
Kama umekumbuka jambo hapa bila
shaka wewe si wale waandikao 'x'
badala ya 's'
Asante, umenikumbusha mbali!, nadhani hiki ni kitabu cha "Someni Bila Shida-3" Someni kwa Furaha" ndio vilikuwa vile vya darasa la kwanza na la pili, vya "JUMA NA ROZA".Fikiri mimi maskini,
Uvivu wangu nyumbani,
Ukiwa huu njiani,
Nakufa hapa kwa nini?
Sadiki sasa ashiba,
Chakula kingi kwa baba,
Nirudi tena kwa baba,
Nakufa hapa kwa nini?
.............................................
.................
Naomba radhi nimekosa,
Nitakuwa mtoto mwema sasa,
Shambani tena sitakosa,
Baba na mama nisameheni.
Nitalima kama Sadiki,
Nitalima wala sichoki,
Na nyumbani tena sitoki
Baba na mama nisameheni.
Kama umekumbuka jambo hapa bila
shaka wewe si wale waandikao 'x'
badala ya 's'
mkuu mie nikafikiri baada ya hapo ungeendelea na....
karudi baba mmoja toka safari ya mbali,
kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili...
watoto wake wakaja ili kumtaka hali,
wakataka na kauli iwafae maishani!
Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
roho naona yachinjwa, kifo kina nikabili,
kama mnataka mali, mtayapata shambani.
Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
kama tunataka mali, tutapataje shambani?
Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
kama mnataka mali mtayapata shambani.
Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
kama mnataka mali, tutayapata shambani.
Shamba wakapalilia, bila kupata ajali,
mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
wote wakashangilia, usemi wakakubali,
"KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI".
Pasco
Asante, umenikumbusha mbali!, nadhani hiki ni kitabu cha "Someni Bila Shida-3" Someni kwa Furaha" ndio vilikuwa vile vya darasa la kwanza na la pili, vya "JUMA NA ROZA".
Not sure anymore!.
Pasco
King'aa, ni goat chop ya wapi?, isije kuwa njia ya Kawe!, isije kuwa pale na Mlalakuwa JKT?.Pasco umenikumbusha Enzi zile nna maakili ile mbaya. Nikisoma kitu sisahau. Nikisoma kitabu all interesting quotes zinakaa kichwani day!
Hapo najilia spring rolls na goat chop na chai. ....
King'aa, ni goat chop ya wapi?, isije kuwa njia ya Kawe!, isije kuwa pale na Mlalakuwa JKT?.
Pasco