Sikilizeni, hakuna Simba bila Yanga na kinyume chake. Mngejua?

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Mwanzoni mwa kuinukia kujua mpira na kufuatilia ilikuwa naumia sana pale timu ninayoipenda kufungwa au kuwa na habari mbaya kama migogoro na mifarakano.

Nimefuatilia kwa muda mrefu mpaka nilipokuja kungundua Kuwa Timu za SIMBA na YANGA ni habari nyengine hapa Tanzania. Kwa kweli nilipata tabu sana.

Unaweza usiamini ukipata habari za ndani kabisa kuhusu umuhimu wa hizi timu. Ukiachilia mbali historia za kuanzishwa kwake lkn zimebeba mwelekeo mzima wa kile kinachoitwa " Political Footbal" itoshe kusema kwamba

"Simba na Yanga zinatumika kuweka udhibiti wa kiutawala hapa Tanzania na ni instruments muhimu ya kubadili mwelekeo wa nchi pale inapohitajika. Yanayofuata kuanzia hapo yote ni Planned"

Hiyo sentensi ipigie mstari hapo juu.

i. Utashangaa kwa nini kunazuka migogoro kwa kupishana kila wakati baina ya timu hizo mbili

ii. Utashangaa namna namna wanavyopatikana viongozi na kuenguliwa wengine na namna mifumo ya chaguzi inavyofanya kazi.

iii. Utashangaa namna timu hizi zinavyopewa nafasi na fursa kuliko nyengine na.

Nilikuwa sijui haya, nilishangaa kipindi fulani kuwa na timu pekee zinacheza usiku na sio saa nane mchana. Ni zaidi ya sababu unazozijua wewe.

Kumeaminishwa hizi timu ndio zinabeba Taifa lakini utashangaa timu zinazochipukia sizipate fursa sawa za kuliwakilisha Taifa hata pale Uongozi wake na mipango kuwa thabiti. Mwisho unabaki kuwa mtazamaji tu.

Simba na Yanga ziko chini ya Mfumo maalumu wa Udhibiti kwa manufaa ya Nchi. Amini haya maneno, Ukishamaliza hapo, ndio ujue viongozi wetu wamepangana wengine washabikie Simba au Yanga. Usishangae.

Tofauti na siasa, ambapo chama kisichotakana na historia yetu ni dhambi kuungwa mkono na mfumo lakini huku sawa tu ilimradi ni mechanism ya kufikia malengo ya kusonga mbele nchi kiutawala.

Hili somo ni gumu lakini wenye kunielewa wataelewa.

Huko tuache. Kuna Uchumi na maslahi binafsi ya wakubwa, ndaro na mauza uza mbali mbali.

Simba na Yanga ni zaidi ya unavyozifahamu.

Ndio nikasema Bila simba hakuna Yanga na kinyume chake. Huko mbele tutaelewana.

Kwa leo inatosha.

Kishada
 
Kuna ka ukweli flani kwenye hoja yako.

Ngoja waje wakuzi wa mambo waendelee kutujuza.
 
Wasioelewa haya mambo watakupiga mawe lakini huo ndo ukweli.
Hizi timu ni mali ya serikali na zinatumika kwa maslahi ya watawala
 
Kila lisemwalo kwa hapa Tanzania usidharau kwa asilimia zote...maana kama taarifa za ndaaani kabisa na nyeti za serikali zinavuja itakua hili? Uwezekano wa hoja hii upo
 
Back
Top Bottom