Hoja ya bandiko hujaijibu.wazanziabari wanaokufa Dafur DRC wale ni nani SMZ au JMT wacheni upumabvu
kama wenzenu wamekuzidini kete mlie tu
Hatuna wivu wa biashara ya bangi inayofanywa na SMZ. Hatuna kabisa.
Waziri wa miundo mbinu keshaitetea sisi tunasema bendera yetu kufungia tani za bangi haifai!
Inachafua sura ya nchi na hata znz. Hivi OIC(Shirika la dini) wakisikia znz inafanya baiashara ya bangi watakuwa happy kweli,
Yetu ya Tanzania ambayo imetumika katika kufungia zigo la bangi lililopaswa kufungwa na bendera ya Zanzibar, au nimekosea?Mkuu tuweke wazi,bendera yenu ipi uliokusudia?
Ulinzi na usalama pia. Mkatae muungano wa mkataba au serikali 3. Mkishindwa hayo mtakuwa chini ya JMT mtakae msitake.
Waziri wa miundo mbinu wa znz hakulaani wala kuonyesha kuchukizwa na meli iliyosajiliwa na ZMA taasisi ya SMZ.Mkuu futa kauli yako sisi hatufanyi biashara ya bangi
Wadanganyika punguzeni umbulula,kwanza rejesheni tanganyika yenu ndipo mropokwe.
Ulinzi na usalama pia. Mkatae muungano wa mkataba au serikali 3. Mkishindwa hayo mtakuwa chini ya JMT mtakae msitake.
Huwa ninajiuliza sana lakini sipati majibu hivi kati ya Tanganyika na Zanzibar ni nani huwa anang'ang'ania huu muungano.
Unafanya spinning ukwepa hoja ya bandiko. Huko unakotaka twende kwasababu una 'ujuzi' nako mimi siendi. Mada si matusi wala kashafa, ni juu ya waziri wa zanzibar kuwananga waandishi wa habari wa Tanzania kwa kuandika habari hizi na wala si wa duniani ambako meli imeonekana ikiungua moto na juu bendera ya JMT ipo.Mkuu leo ndio umenifumbua macho kumbe wale wazungu kutoka uk nyinyi ndio mume watupia tindikali na nyinyi ndio manchoma makansa ndio njia yenu ya kuwafanya mabwana zenu wa ulaya wajue kuna nchi inaitwa zanzibar sisi tunategemea nguvu za Mwenyezi Mungu tu
Mi nlijua nyie wasomi kumbe wadanganyika! Umewahi kuona wap mume akibadilisha jina? Pili Nguruvi, soma ebu, bendera ya zanzibar haitambulikani kimataifa, kwaiyo meli yoyote iliyosajiliwa Zanzibar ama tanganyika lazima ipeperushe ya tanzania. Kisha tambua, hio ni ya tanzania sio ya tanganyika. Ebu leo tutizame, meli hiyo mmiliki nani? Usikute myanganyika mwenzenu. Lakini kwa nini ilaumiwe zanzibar kwa kosa hilo nakudai eti tunaichafua tanganyika? NI CHUKI ZENU TU. watanganyika wangapi wamekamatwa na unga na huandikwa tanzania? Mbona hamusemi hilo kuwa linatuchafulia na sisi?
Kauli ya Waziri wa Mawasiliano na Miundo mbinu wa SMZ, Rashid Seif Suleiman ya kuvilaumu vyombo vya habari vya Tanzania BARA ilinishangaza sana.
Ni kweli kabisa kuna kitu viongozi wetu waasisi wa 'muungano' walikiona kama kilikuwa ni cha muhimu sana kuziunganisha nchi zetu, lakini vile vile makosa ya kutokuelimishwa na kutoshirikishwa kwa wananchi wengi katika kufikia uamuzi huo ndiyo yamechangia kwa kiasi kikubwa kuwa chanzo cha mitikisiko na utegemezi katika 'muungano'.
Imedhihirika kuwa viongozi wakuu waliokuja baada ya marehemu Sheikh Abeid Amani Karume na pia Wazanzibari wengi hawakutaka kuendelea kuwepo muungano na kwa sababu hiyo ilibidi viongozi wetu wawabembeleze kihoja na ilipobidi pia yalitumika mabavu ili waendelee kuwepo mwenye 'muungano' . Hii ilipelekea wananchi wengi wa Zanzibar na pia wachache wa bara kuamini kama viongozi wakuu wa bara walikuwa na ajenda fulani za siri ambazo kuzitimiza ilibidi tuwaombe na kuwashinikiza Wazinzibari waendelee kuwepo kwenye 'Muungano'.
Fikra na mitazamo hii imekuja kujisimika zaidi pale badhi ya viongozi wakuu wa Zanzibar walipotiwa misukosuko pale walipohoji uwepo wa muungano na manufaa yake.
Kwa sasa wanafanya kila wanachotaka bila kujari mshikamano, sheria na taratibu za nchi wakidhani kuwa Tanganyika inawahitaji sana zaidi ya wao kuihitaji Tanganyika.
Hata kujitoa kwao katika sheria za Jamhuri ya muungano zinazohusu usafiri wa majini za mwaka 2003 na kuunda sheria zao za bahari na usafiri na kuwa chini ya Zanzibar Maritime authority((ZMA) mwaka 2006 ilikuwa ni katika mwendelezo wa fikra hizo.
Waswahili wanasema, mdharau mwiba mguu huota tende!.
Tumezidharau na wakati mwingine kuzipuuzua chokochoko za 'muungano' kwa muda mrefu huku tukiwadekeza Wazinzibari kwa kuwapa kila kile wanalichokuwa wanakitaka na matokeo yake kwa sasa tunayaona. Kwa sasa imekuwa chao ni chao lakini chetu pia ni chao na wakati mwingine wanataka wakichukue chote.
Tulianza muungano vibaya na inavyoonekana pia tutaachana nao vibaya, na kwa maana hii, dawa ya muungano kwa sasa siyo serikali tatu kama baadhi ya watu wanavyodhani, bali ni kuachana kabisa na muungano ili pande zote zipate ukweli halisia kama kuna umuhimu katika muungano. Hatutakuwa wa kwanza wala wa mwisho katika kuvunja muungano kwa sababu kuna nchi zimevunja muungano na zikapiga hatua zaidi za kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Hata katika ndoa, watu wanapokinzana sana, huwa wanafikia maamuzi ya kuachana ili kujipima na kuona umuhimu wa wao wakiwa pamoja au wakiwa single (space) na wakipatwa na reality, wengi wao hurudiana tena.
Unafanya spinning ukwepa hoja ya bandiko. Huko unakotaka twende kwasababu una 'ujuzi' nako mimi siendi. Mada si matusi wala kashafa, ni juu ya waziri wa zanzibar kuwananga waandishi wa habari wa Tanzania kwa kuandika habari hizi na wala si wa duniani ambako meli imeonekana ikiungua moto na juu bendera ya JMT ipo.
Narudia waziri hakuona tatizo katika mzigo huo wa tani 30 zenye bilioni 125 thamani. Tatizo lake kubwa sana ni kwanini hanari hizi zimeandikwa! Hapo unaweza kuona jinsi ambavyo zigo la bangi ya Zanzibar lisivyousa hisia bali mashambulizi kwa waandishi wa Tanzania bara kwa kuandika.
Hoja ni kwanini SMZ yenye ZMA ambazo si sehemu ya JMT kwa makusudi kabisa wameamua kutumia bendera ya JMT kufunikia tani 30 za zigo la bangi. Hili ndilo lipo mbele yetu na linakera sana.
Hatuna kero na bilioni 125 za mapato, kero ni kutumia bendera yetu kufungia zigo la uhalifu na waziri wa SMZ kutoonekana hata kujali yarabi!
Waziri anaita waandishi wa habari kulaani waaandishi hao na si tani 30 za zigo la bangi, hii inaingia akilini kweli.
Kama inaingia kwanini tusidhani mzigo huo ni wa biashara na waziri alikuwa anatetea masilahi ya nchi, why?
Je, ni wazanzibar au ni vibaraka?
Hapa kuna issue ya muungano watu wanachanganya. Hili si suala la muungano.Mkuu Nguruvi3 Hivi kama muungano usingekuwapo unadhani malalamishi ya kuchafuliwa kwa tanganyika na nchi ya zanzibar, na sio Tanzania kama unavyoandika ingetokea?
Nb tanzania ni pamoja na tanganyika na zanzibar yenyewe. Na kama jibu nila unadhani ni nani wa kulaumiwa? Walioasisi Muungano au wanaondeleza muungano?
Wazenji Siwapendi kwa Tabia zao