Sijui utarudi lini kaka

innocentmollel

JF-Expert Member
Sep 11, 2014
1,702
746
Yapita miaka minne sasa tangu kaka ulipo ondoka nakusema waenda tafuta maisha kaka nchi za wenzetu,tangu ulipoondoka kaka mkeo alibadilika utafikiri ana mume na watoto wawili uliomwachia awaangalie kipindichote ambacho hautakuwepo,kaka mkeo alianza kuwa mlevi,alianza kurudi na wanaume nyumbani kaka mimi nikawa nawalaza watoto mapema ili wasione ujinga ambao mama yao alikuwa akifanya.

Kaka kwa mambo ya mkeo aliyokuwa akifanya na starehe alifukuzwa kazi katika ile bank alipokuwa akifanya kazi ya umeneja, kaka mkeo akawa ana helaa tena za kutumia katika starehe zake ndipo akaanza kutumia akibà ya watoto ya kuwasomesha uliyowaekea ili wasipate tabu maana ulikuwa ukiniambia {Inno mdogo wangu maisha hayatakuwa mazuri siku zote ,IPO SIKU SITAKUWEPO} Daaaa sasa ndio naamini usemi wakoo.

Mkeo alikula bata kilaa sehemu ya starehe watoto walikosa ada hvyo ilibidi niwachukue na kuondoka nao pale nyumbani japo mkeo aligoma kata kata mimi kuondoka nao ilaa niliforce nikaweza wachukua na kumwacha ale maisha awevyo, kaka namshukuru Mungu nimepigana kwa uwezo wangu wote na wa Mungu nimeweza kuwarudisha shule now wanasoma yule mkubwa yupo darasa la nne ,na mdogo yupo la pili na wote wanasoma shule ambazo ulitamani wasome.

Kaka mkeo alifikia uamuzi hadi wakuuza nyumba ila nilipambana sana nashukuru Mungu nilishinda kesi kaka kwa ajili yakuwatetea watoto haki yako kaka,katika sikuu ambazo sitazisau ni pale mkeo baada ya mimi kushinda kesi ya nyumba alinitumia watu waniue kama Mara tano ilaa namshukuru Mungu aliniokoa na sasa napigana na wanao wasome sana.

Kaka niliumiaa pale siku nimekaa nikiwa nafanya shughuli zangu ndipo nilipataa taarifa kaka kumbe umefarki huko nchi za wenzetu ndipo kampuni uliyokuwa ukifanya kazi ikafanya utaratibu ukarudishwa ukiwa umelala kaka si kama ulivyoondoka nililia sana pia wanao waliliaa sana ,kaka ulipofarikii haikuchukuaa hata miakaa miwilii mkeo naye alifariki kwa UKIMWI daa! Leo watoto wamebakii yatima,ilaa kaka uko ulipo nakuakikishiaa nitawatunza wanao mpaka wakiri mimi ndio baba yao. R I P KAKA.
 
Dah pole ssna. Inawezekana shemejiyo alijua status yake, sasa kwa ubinafsi wake akaamua 'kuponda mali kifo chaja'. Inauma sana kuwa na ndugu aso thamini hata wanawe. Ninatumaini watoto wote hawana maambukizi
 
Kila jambo linalotokea maishani mwetu liwe baya kwa macho na hisia zetu au zuri, Mwenyezi Mungu anakuwa ameliruhusu kwa makusudi maalumu ambayo ukiendelea kuwa mtulivu kwake utakuja kuyaona na kumuelewa.
So ndugu mollel mshukuru Mungu sana kwa jambo hilo kwa maana anayo sababu nzuri sana uyapitie na uwatunze hao watoto.
Mwamini atakulipa sawa na mapenzi yake
 
Dah pole ssna. Inawezekana shemejiyo alijua status yake, sasa kwa ubinafsi wake akaamua 'kuponda mali kifo chaja'. Inauma sana kuwa na ndugu aso thamini hata wanawe. Ninatumaini watoto wote hawana maambukizi
Mungu n mwema watoto aliwazaa kabla ajaanza kuponda raha na kupata maambukizi ambayo yalimsababishia kifo ,watoto wapo salama kabisa na mshukuru mungu wanaendelea na masomo yao
 
Back
Top Bottom