Sijui nianzie wapi?

kaka tujulishe kabila la huyo mwanamke ingawa sio vizuri lakini tujulishe tu
 
asante kiongozi, nitakutafuta
 
Mkuu nashukuru sana, hicho ulichosema nilikifanya mapema sana, nikajikuta nipo vizuri that why nikaja jamvini kupata msaada wa kimawazo nisonge vp kuanzia hapa.
 
nipo hapa mjini mkuu, mji ambao wanaume hatuna thamani tena eti kwa kua tulijifungia ndani kuogopa panya road

Hapana mkuu, Hapo mnajipenda na kutunza amani ya nafsi zenu !!
back to topic....
Hivi sasa weka kipaumbele kuwa watoto wako ndiyo wana umuhimu zaidi hivyo ongeza ukaribu nao. Kuhusu wee mwenyewe jipange vizuri na kwa utulivu ili uweze kuendelea na kazi/ajira yako bila confusions !! Subiria mitihani hii unayokabiliana kwa nguvu moja bila kutereeka. Mimi na amini hakika utashinda.
Itakapo wadia time muwafaka utapata mwenza mwema. Good luck Mr.Kahema
 
mkuu Mimi nakushauri kitu kimoja, tafuta house girl au ndugu yoyote anayeweza kuwalea wanao vizuri, ishi nae pale home.madogo waende shule wakitoka wanakuta msosi na Cares zingine

jenga utaaratibu Wa kurudi home mapema , ili madogo wakuone before they retire to bed, baada ya hapo unaweza kunyoosha miguu kwenye ki pup cha Jiran hapo.
suala LA kuoa sasa hivi achana nalo kabisa, na Kama wewe ni mtumiaji Wa gambe, this is the time to quit or punguza kabisa coz unaweza jikuta unakunywa Sana kupunguza stress, kumbe wajiharibia.
make sure that ukiwa na nafasi japo weekend then wapeleke madogo matembezi kidogo,being close to the children will make you forget their mum and other women.
ukizidiwa kimwili, I mean damu ikichemka then unaweza kuchepuka once in a blue moon bhana usiogope lakini usiende kwa Mke Wa mtu au hookers,tafuta single mother ambae Hana shida ya mwanaume Wa kumlea Bali Wa Ku share nae life experience tu, wapo wengi Sana.
jenga mapenzi mengi Sana kwa watoto, ili wasije wakakuuliza mama yuko wapi au baba tunamtaka mama, yaani wasi m miss kabisa.am talking from experience brother.
wakati unafanya haya mungu atakuwa anakufunulia njia ya kumrudia mkeo au kutafuta mbadala wake.usikurupuke kumrudia au kupiga chini for good.
 
Kuwapeleka bording sio mbaya ila uyo mwanamke kama ukiamua kusamehe usame moja kwa moja sio kutengana vitanda itakuwa bado hamuwatendei haki watoto ata mausiao yenu yanaweza kuishia pabaya zaidi kwa iyo ushauri wangu mm watoto bording fanya kazi kwa ajili ya wanao baadaye sana ndo utafuta ubavu mwingine. Kwani ukitafuta sasa atakuletea drama zingine
 
kwa ufupi tu dada yangu, mimi na huyu binti tulikutana hapa mjini, tukawa marafiki na hatimaye tukaoana, binti alikuja mjini toka kwa wazazi wake akaja kuishi kwa uncle wake ambaye ni swahiba wangu wa karibu. kiufupi huyo rafiki yangu ana familia yake nzuri kabisa na background yakwao naijua fika maana tumesoma,tumekua wote so haikua taabu mimi kumjua huyo binti kiundani zaidi. na kwa kweli ndani ya miaka yote hiyo sikua na tatizo naye kimaadili kwa kua hakuonyesha hilo waziwazi, mengine yapo japo ni madogo madogo. lakini kitu ambacho nikuweke wazi tu dada yangu ni kwamba nilimuamini sana na nikampa uhuru sana huyu binti kiasi kwamba hata alipokua akiniaga kwenda sehemu sikuhitaji kumuulizax2 ilo labda ndio kosa langu kubwa.
ukitaka kujua mengi tafadhali ni PM
 

i can feel the pain you are undergoing brother, am married and I once trusted my wife to that extent comrade.
anyway kuna ushauri Wangu nimekupa hapo juu.changanya na zako then fanya kazi mkuu.
 
asante sana kiongozi
 
Pole sana.

Swala la kusamehe msamehe kwa moyo mmoja kabisa ili wewe ubaki mwepesi na uweze kuendelea na maisha yako bila kuwa umejawa na hasira/chuki ambavyo vitakuumiza wewe badala ya aliyekuweka kwenye hiyo nafasi. Na asikudanganye mtu KUSAMEHE SIO KURUDIANA. Na hapo kwenye kurudiana au la usitake kushauriwa na watu kwasababu mwisho wa siku wewe ndo utatakiwa kuishi na matokeo. Yani fuata moyo wako, kama uwezo wa kumsamehe na kurudiana nae unao haya, kama huwezi MSAMEHE kisha mwache aende zake. Hapo maamuzi ni yako wewe na sio yetu watazamaji.

Tukija kwenye swala la kuoa, hilo hutakiwi hata kulifikiria kwa sasa. Its way too soon. Usije ukalogwa ukaoa chap chap ili tu upate mtu wa kukulelea watoto, utaishia kulia tena mbeleni. Chukua muda wa kupumzisha moyo na akili yako huku watoto wako wakiwa your primary focus.

Ningekushauri wakae na mama yao utoe matumizi ila kuna sehemu nimesoma kwamba alishawahi kukimbia akawaacha watoto wote hadi huyo mdogo kwahiyo huyo hata hawajali watoto kwahiyo hilo jukumu halimfai. Wala sikushauri uwapeleke boarding kwasababu binafsi naamini watoto wanahitaji sana mapenzi na ukaribu wa wazazi katika ukuaji wao. Hapo nyumbani angalau utaweza kuwasaidia ku-cope na hiyo hali iliyopo kwa sasa kuliko huko boarding. Huko hamna aneenda kujali hisia zao, baadae utashangaa tu watoto wako sio wale uliokuwa ukiwafahamu mwanzo. Kwahiyo tafuta ndugu yako wa karibu ambae mnaelewana na unajua ni mzuri kwa watoto umuombe aje kuishi na nyie alafu uajiri na dada wa kazi. That way utakuwa na mtu atakae hakikisha watoto wanaishi maisha yanayokaribiana na yale ya nyuma au hata bora zaidi bila kumchosha sana na kazi.

Usitafute shortcut ya namna gani ulee watoto wako utaishia kujilaumu baadae. GOOD LUCK.
 
kwa miaka hiyo hutogegeda tena ??
 
Mkuu nashukuru sana, hicho ulichosema nilikifanya mapema sana, nikajikuta nipo vizuri that why nikaja jamvini kupata msaada wa kimawazo nisonge vp kuanzia hapa.
Rudia kusoma mchango wangu kuna way forward step by step......Ila uwe mbayuwayu.
 
maya amempenda sir chief akiwa na watoto watatu na ijumaa wanafunga ndoa. na maya atajifungua mapacho soooo jiongeze. ila pole inauma

yule kapenda koz mpendwa kafiwa sio kaacha! ni feeling mbili tofaut coz kwa mwanamke mwenye akili ukimwambia mwenzio alinicheat atakuuliza kwanini? then mnavyoendelea kuishi atakuja akwambie ndo maana hata mama fulan alikuwa anakucheat!!!

inahitaj hekima ya ziada sana hapa!
Mungu akusaidie Kahema
 

I love this, haitofautiani Sana na ushauri Wangu kwake..though yako imeenda deep Sana na Ina ushauri nzuri Sana.
asante kwa ushauri wako kwa memba mwenzetu , ni Wa busara Sana , hope atachanganya na zake then atafanyia kazi.
Mimi pia kuna mawili matatu nimeya absorb from your ushauri .thanks
 
Mimi naona upate muda wa kutafakari na kumshirikisha Mungu akusaidie kwa hili. Watoto wapeleke bording ya karibu kiasi kwamba uwe unaenda kuwaona kirahis. Mdogo kama mama yupo mwambie akusaidie kumlea wakat hujachukua uamuz kip ufanye. Unahitaji mda wa kutulza akili kabla ya uamuz wowote. Maamuz ya haraka huku una hasira yanaweza kukupeleka kwenye shida zaidi. Pole sana!
 
Kahema sina hata haja ya kuku pm maana jibu nimelipata kua uhuru mkubwa uliompa ndio umesababisha yote haya. alijisahau kwa ufupi. binadamu hachungwi lakini panapowezekana kua mkali kidogo. Nina marafiki wenye waume zao, wanakaa bar mpaka ma usiku anakuambia mume wangu hana neno.. excuse me... hana neno vipi? eti tunatafutana wakati wa kurudi nyumbani, sasa kwanini msitoke pamoja? Marafiki hawa wanachepuka kupita kiasi maana mume nahisi nae anachepuka kivyake. hata kama mmebaki kua kaka na dada maana kuna muda fulani kwenye ndoa inakua hivi, lakini heshima ni kitu cha bure. Pole sana Kahema, unaweza ku consider ushauri wangu wa mwanzo. wanawake si wachepukaji lakini wakiamua hawarudi nyuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…