Mbaya zaidi kiongozi, wakati wa purukushani hii, huyu wife alishawahi kuwakimbia hawa watoto sio chini ya mara tatu. alidiriki kuondoka nyumbani zaidi ya siku sita, hiki hasa ndo kilichonifanya nisiwaze hata mara moja kumwambia aondoke kwangu. haikua rahisi na ni mengi sana nimeyaona sijayaweka hapa. najuta kumfahamu huyu mwanamke
Unaweza msamehe ila ukaamua kutoshare tendo, mkawa mnalea watoto wenu kila mtu chumba chake ila matumizi ya nyumbani hakikisha unatoa. watu waelewa wanaishi ivo ili kuwatunza watoto, japo yataka moyo
Kahema oa huyu amejileta mwenyeweNi wanawake wachache wenye mioyo hiyo..kama mimi
Mkuu Kahema tuliza wahka ...its not the end of life !! You are still young at 35 yrs Life ndo taamu sana na wengi wanakutamaani !! tafuta kwa makini utapata na umpromise Love yako penzi jema akikaa na wanao vizuri!! utafanikiwa tu.... Halafu usifikirie ya nyuma ongoza mbele maisha yana songa mbele... "aliyemwaga mboga mwenyewe asikupotezee moods zako!! Hakuna kusamehesamehe..kwani hakuheshimu watoto wala hata ndoa yake!!
Wanajamvi,
natumaini muwazima wa Afya,
Nimeona nije kwenu walau mujue yanayonisibu, sio kitu kipya hapana, ila
kimeniweka kwenye mazingira magumu sana, japo najitahidi kufanya kila
linalowezekana walau upepo huu upite.
kifupi ni hivi Mama wa Watoto wangu (Mke) nimeamua kumrudisha kwao baada
ya kugundua hakua mwaminifu kwangu ie niligundua anamahusiano ya
Kimapenzi na Watu wengine Nje ya Ndoa, nilifanya uchunguzi wa kina
nakugundua uchafu huo, baada ya mikimiki ya hapa na pale alikiri mbele
ya wazazi wake kua yote niliyowaeleza ni ukweli mtupu. baada ya
mashauriano ya muda mrefu nilifikia uamuzi wa yeye aondoke kwangu. hili
halikua gumu sana kuamua kwa kila kitu kilikua wazi
So issue yangu kubwa ni nini nifanye baada ya hapa, ukizingatia
yafuatayo:
1. tuna watoto watatu , mdogo kabisa ana miezi 9
2. hawa watoto nawapenda sana na mpaka sasa naishi nao
3.mimi mwenyewe umri umekimbia am 35 yrs now
4. mama watoto kila siku anapiga simu kuomba msamaha( japo najua kabisa
jasiri haachi asili)
5. najiuliza hata kama nikitaka kuoa tena, will it be fair to my
children?
6. nina watoto 3, will it suit me kuoa mwanamke ambaye hajazaa? ataweza
kulea kwa upendo hawa watoto?
7.je nikioa mwanamke mwenye mtoto/watoto tayari si atataka naye awalete
waishi kwangu? huu mzigo utaniua
8.je ni haki niwapeleke boarding hawa watoto ili mi niishi peke yangu?
kiukweli nipo njia panda, tafadharini yeyote anayeweza nisaidia
kimawazo nitashukuru
asanteni!
never never,
worse enough hajawahi hata siku moja kunieleza kua simridhishi haja zake, Kazi nilipiga vizuri hilo hata yeye alikiri.
Ushauri wangu
1. Cheki DNA unaweza kuwa unaumiza kichwa kulea watoto wa wanaume wenzio..kama kipimo kitaonyesha watoto sio wako..mpe mama yao awapeleke kwa baba zao.
2. Usimrudie...embu fikiria mtu anayetembea na wanaume ovyo..hizo ni bidii za kutafuta ngoma..sasa huo utu wake unatoka wapi..achana nae.
3. Maumivu ya moyo yapo na ni kwa sababu mlikuw wapenzi ..yataisha..
4. Kama DNA itaonyesha hao ni watoto wako weka utaratibu mzuri ,wa malezi..kama wana jf walivyoshauri.lakini yeye asihusike..atawapa maneno mabaya watoto..na hiyo itawaathir sana.
5. Hili ndio lingetangulia point zote hapo juu..muombe sana Mungu akuongoze
hapana , nipo naye mimi. kwa hari ilivyokua haikua rahisi hata kumuacha huyo mtoto kwa mama yake kwani kulikua na kila dalili ya murder.
mmh ushauri mgumu mno
Msamehe tu.........,
wanaume wana mioyo migumu ya kusamehe tofauti na wanawake
Asante, nitaufanyia kazi ushauri wako.
ila swala bado lipo pale pale, baada ya hayo yote then what shall I do? should I sacrifice my happiness so that my children are happy? or should I keep on searching till god say yes? totally confused.
Inawezekana my dia
Mi ndugu yangu walifanya hivyo though at the end of the day waliachana
Aiseee mkeo ana hatari yani anacheza rafu mbele ya refa?