Sijui la kuamua

Sijui la kuamua

kwani mpenzi wako na boss tu ndo wapo night shift? kama ni hivyo nenda kazini na mkeo....
 
Kwanz mkuu ni kazi gani ndo unaweza kuwa rahisi kidogo watu kukusaidia kwa mawazo maana kuna kazi hata mm binafsi sitakushauri ukubaliane naye
 
Mpe nafasi ya kufanya kazi kwa uhuru utaona matunda yake mwanamke anayejitambua hana tabu kwani akiwa na tabia mbaya siyo night tu hata asubuhi anakutengea chai yeye anchepuka hivyo toa nafasi na muamini.
 
ndo hivo mkuu wacha wakulie manzi wako wewe si unaeka imani ya kupigiwa basi acha upigiwe...
 
imani ni moja ya nguzo muhimu sana katika kupata majibu ya kila jambo
MKUU kuwa na IMANI na mKeO%
IMANI YAKO ITAKUPONYA!
 
Maskini hachagui Kazi...usimuachishe kazi wala kumuacha...jitahidi uwe unampa maneno matamu kabla hajaenda kazini..ikiwezekana msindikize......mfanye akiwa kazini awaze nyumbani.

ndio The Boss....
 
Last edited by a moderator:
Usimfikiria mabaya.. Mwache ajishikuze huku unamtafutia nyengine ...
 
Habari wana jamvi? Jamani nimekuja walau nipate ushauri akili yangu itulie. Shemeji yenu baada ya kula msoto wa muda mrefu bila ya kibarua, hatimaye siku ya nne leo ameanza kibarua, hakika kila aombaye atapewa muhimu uvumilivu.

Sasa tatizo kaambiwa leo kuwa kuanzia kesho aanze night. Kidume roho imedunda. Naujua udhaifu wa watoto wakike kwenye usingizi hasa ukizingatia kuwa. Kazi zenyewe ni za kibongo bongo. Mawazo yangu yakanituma itakuwaje pale shemeji yenu kabanwa usingizi saa8 za usiku then boss wake atumie nafasi hiyo kumhadaa.

Wenzangu ambao wake,wachumba zenu huwa wapiga 9t naombeni ushauri tafadhali, sina la kuamua nimuache huyu dada, au nimwambie aache kazi, au nivumulie? Nawakilisha,.

Aaaaah!!!we vumulia tu mkuu na kuwa na imani na yeye kama anakupenda kweli!!mvumulie tu shemeji
 
Maskini hachagui Kazi...usimuachishe kazi wala kumuacha...jitahidi uwe unampa maneno matamu kabla hajaenda kazini..ikiwezekana msindikize......mfanye akiwa kazini awaze nyumbani.

Mmmhhhh it sound good....... ila kumsindikiza kazini ni shida amuamini tu
 
Kama Wewe Ni Mdhaifu Na Mkeo Ndo Umwone Hivyo??Kama Unaona Boss Anafaidi Sana Uwe Unaenda Naye Hiyo Night Shift Umlinde Ndio Wasimuhadae
 
yani hakuna kitu kizuri kama kumuamini mchumba/mke/mume, muwazie mema hutaumia moyo, kaa mbali na simu yake usipende kushikashika, kuweni jamani, yani una relax tu. sasa unajipa magonjwa ya moyo bure utakufa halafu utamuacha.
 
Aiseeee. Wivu ukizidi husababisha maangamizi. Kwanini umfanye mke wako cheap kiasi hicho? Mtadumu kweli kwenye ndoa yenu!!? Kwanini usimwamini? Au kuna udhaifu wake wa kugawa hovyo hovyo unaufahamu umeshindwa kutueleza? Kama ni hivyo; basi mke wako hafai. La sivyo muamini. Vinginevyo utakufa kabla ya wakati kwa presha inayotokana na wivu.
 
yani hakuna kitu kizuri kama kumuamini mchumba/mke/mume, muwazie mema hutaumia moyo, kaa mbali na simu yake usipende kushikashika, kuweni jamani, yani una relax tu. sasa unajipa magonjwa ya moyo bure utakufa halafu utamuacha.

na ukimuacha anahamia kwa boss
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom