Sijui la kuamua

Sijui la kuamua

Craig

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2013
Posts
1,676
Reaction score
3,143
Habari wana jamvi?

Jamani nimekuja walau nipate ushauri akili yangu itulie.

Shemeji yenu baada ya kula msoto wa muda mrefu bila ya kibarua, hatimaye siku ya nne leo ameanza kibarua, hakika kila aombaye atapewa muhimu uvumilivu.

Sasa tatizo kaambiwa leo kuwa kuanzia kesho aanze night. Kidume roho imedunda. Naujua udhaifu wa watoto wakike kwenye usingizi hasa ukizingatia kuwa. Kazi zenyewe ni za kibongo bongo.

Mawazo yangu yakanituma itakuwaje pale shemeji yenu kabanwa usingizi saa8 za usiku then boss wake atumie nafasi hiyo kumhadaa.

Wenzangu ambao wake,wachumba zenu huwa wapiga naombeni ushauri tafadhali, sina la kuamua nimuache huyu dada, au nimwambie aache kazi, au nivumulie?

Nawakilisha.
 
Mwache apige kazi mwenzio mke wangu mjeda kila week anakua zamu mara 3 hila ni mwaminifu sana kaa na wife mweleweshe kua siku hizi mchepuko ni ushamba basi naisi atakuelewa ndugu
 
Habari wana jamvi? Jamani
nimekuja walau nipate ushauri akili yangu itulie. Shemeji yenu baada ya
kula msoto wa muda mrefu bila ya kibarua, hatimaye siku ya nne leo
ameanza kibarua, hakika kila aombaye atapewa muhimu uvumilivu.

Sasa tatizo kaambiwa leo kuwa kuanzia kesho aanze night. Kidume roho
imedunda. Naujua udhaifu wa watoto wakike kwenye usingizi hasa
ukizingatia kuwa. Kazi zenyewe ni za kibongo bongo. Mawazo yangu
yakanituma itakuwaje pale shemeji yenu kabanwa usingizi saa8 za usiku
then boss wake atumie nafasi hiyo kumhadaa.

Wenzangu ambao wake,wachumba zenu huwa wapiga 9t naombeni ushauri
tafadhali, sina la kuamua nimuache huyu dada, au nimwambie aache kazi,
au nivumulie? Nawakilisha,.

ni kazi kweli ila nakuomba vumilia uone kwanza maana kazi kaipata kwa shida.pole
 
Hii nayo kali. Eti wanawake tuna udhaifu kwenye usingizi? Mpaka ifike mahali boss anakuhadaa? I'll be damned!!
 
Wasiwasi wako nini si ndo kazi alikuwa anataka amepata mara tu ushataka ushauri hata wiki kazini hajamaliza,muache afanye kazi kikubwa ni uaminifu tu ukishaweka negativity kwa huyo mpenz wako hata akiingia asubuhi kazini bado utahisi unaibiwa
 
Kazi gani hiyo mkuu ya kumuweka sadaka mkeo? Na unajua dada zetu walivyo hawatakiwi kupewa uhuru zaidi fikiri kwanza
 
Habari wana jamvi? Jamani nimekuja walau nipate ushauri akili yangu itulie. Shemeji yenu baada ya kula msoto wa muda mrefu bila ya kibarua, hatimaye siku ya nne leo ameanza kibarua, hakika kila aombaye atapewa muhimu uvumilivu.

Sasa tatizo kaambiwa leo kuwa kuanzia kesho aanze night. Kidume roho imedunda. Naujua udhaifu wa watoto wakike kwenye usingizi hasa ukizingatia kuwa. Kazi zenyewe ni za kibongo bongo. Mawazo yangu yakanituma itakuwaje pale shemeji yenu kabanwa usingizi saa8 za usiku then boss wake atumie nafasi hiyo kumhadaa.

Wenzangu ambao wake,wachumba zenu huwa wapiga 9t naombeni ushauri tafadhali, sina la kuamua nimuache huyu dada, au nimwambie aache kazi, au nivumulie? Nawakilisha,.

angalia maisha mkuu,kwa hali tuliyonayo sasa weka akilini muda wote kuwa shemeji yetu anachepuka.haijalishi akiwa nyt au day.akili yako iset iwe inafikiri kuwa huwa anachapwa haijalishi ni muda gani then maisha yaendelee.otherwise utaumiza kichwa tu
 
Kama mkeo ni nurse usiwe na wasiwasi mwache akapige kazi kwa kuwa fani hiyo ina kitu kama wito hivi, na ni nadra sana kumkuta nurse au daktari wakijiingiza katika masuala ya ngono kama ndio hicho unachokiogopa, ukiona hawa watu wanafanya kinyume basi una haki ya kuhoji ni kwa vipi wameingia katika fani hiyo.
 
Naionea huruma hiyo ndoa yako.Kitendo tu cha kufikiria haya yote tayari kina maanisha kuwa ndoa ina mapungufu

Kama huna ushahidi wa matukio ya mke wako kuwa dhaifu kwanini umfikirie hivyo?

Tatizo Hapo sio udhaifu wa Wanawake ila tatizo ni wewe kuwa na fikra potofu na kushusha thamani ya mke wako kiasi hicho,Yani alale tu halafu boss aje apewe P kirahisi!! Mmmh! Suluhisho ni wewe kubadili mtazamo mkuu
 
Kama ni tabia yake hata mchana kweupe ataibia
 
Maskini hachagui Kazi...usimuachishe kazi wala kumuacha...jitahidi uwe unampa maneno matamu kabla hajaenda kazini..ikiwezekana msindikize......mfanye akiwa kazini awaze nyumbani.
 
Maskini hachagui Kazi...usimuachishe kazi wala kumuacha...jitahidi uwe unampa maneno matamu kabla hajaenda kazini..ikiwezekana msindikize......mfanye akiwa kazini awaze nyumbani.

Mleta mada kama nikweli usemayo, fata huu ushauri....
 
tatizo sio wife yetu but wewe ndo tatizo una fikra potofu,umewaza tofauti na huenda na yeye hana hata mawazo hayo,just calm down mwache afanye kazi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom