Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,618
Story ya kweli,
Wanandoa wawili wakiwa kwenye gari lao na mtoto wao mmoja akiwa seat ya nyuma, ni maeneo ya barabara ya uhuru karibu na kituo cha Fire - jijini Mwanza, ghafla kijana mmoja alimwida mwanadada alokuwa ndani ya gari akiwa na mumewe, akafanikiwa kumchomoa ndani ya gari na kuanza kumuhoji huyo aliye naye ndani ya gari ni nani.
Mwenye mke alitoka ndani ya gari na kumwambia kistaarabu kijana aachane na mke wake, lakini alipokea ngumi nzito ya usoni, mwenye mke alijibu mashambulizi na kumchakaza vibaya sana huyo kijana. Sisi kama raia wema tuliingilia kati na bahati nzuri askari wa zima moto wakafika eneo la tukio na kumbeba kijana aloanzisha fujo.
Wakati kijana akijieleza alidai huyo mdada ni mchumba wake na ndo anamsomesha chuo kikuu Tumaini Iringa - sasa amemshangaa kumuona akiwa na mtu mwingine wakifanya shooping.
Naye mwenye mke alitoa maelezo yake na kudai kwamba mke wake wako wote zaidi ya miaka mitano. Mke alipoulizwa akakiri kuwafahamu wote ila akasema kijana aloanzisha vurugu ni rafiki yake tu walikutana chuoni Tumaini. Hapo mwenye mke alimshika mke wake mkono wakaondoka zao na kumuacha huyo kijana akiwa mikononi mwa hao askari wa zima moto,
Swali .....
Wanandoa hao walipofika nyumbani kwao kulitokea nini? Wewe mwanaume ingekutokea wewe ungefanyaje?