sijui ananitafuta nini?

sijui ananitafuta nini?

Kabla haijaisha nshaona mme mwenzio anashuka na mfuko ulojaa kuku,nyama na mbogamboga huku akipokelewa na mama mkwe!!akifika atambusu huyo lover wako na kumwambia 'hongera mpenzi',sasa nawe umeenda shule mimba ikitunga inaweka dalili before 24 hrs!,No wonder walikugongea kwa IQ ndogo...(Natania)pole sana.
 
naendeleaa..
akaanza kutapika baada tu ya kunywa chai mi nikajua malaria ndo imepanda ikabidi nimwaishe hosptli nikampigia mamake sim akaja wachukua vipimo mi nikaondoka kwa ahadi ya kurudi baadaye kwa kuwa nilitakiwa kwenda kuripoti kazini kumbuka ni karibia miezi mitatu nilikuwa nje kikazi.
niliripoti sikukaa sana niliomba mapumziko kwa kusingizia uchov wa safari nikakubaliwa niliporud sikumkuta binti wala mama yake nikapiga sim wakanambia wako home.
nikaenda mpaka kwao make alishantambulisha kwa hiyo wananijua hata kwenye mahitaji madogo madogo ingawa siyo ya kila siku nami nimo.
nilipofika mama akankaribisha wakati binti amelala chini ya mti shem wangu akanipa kiti nikakaa karb na mchumb wangu nikamuliza vp vipimo vinasemaje?
akanambia amepima ikaonekana dalili ya mimba, basi moyoni kwa kweli nilihisi furaha nikajisemea ntaenda kuandika tarehe niliyompa mpenzi wangu mimba.
wakati tunaendelea na mazungumzo ya hapa na pale na Shem mama akiwa ndani Mara nkasikia honi ya gari

sasa endelea mwenyewe mfyuuu
 
naendelea...
likaingia mi baada ya kuona kwa kuwa ndugu zake nawfaham nikajuwa nimmoja wao labda kaingia.
nikaona shem yaani mdogo wake ananyanyuka haraka na kuingia ndani hakukaa sana akatoka mwenye gari tayar keshfika mahali tulipo tukasalimiana tena kwa uchangamfu kana kwamba ananifaham.
nikashangaa kumbe nikweli ananifaham baada mazungumzo ndipo nkagundua nilishawahi mhudumia ofcn.
tukiwa kwe mazungumzo cm yangu ikaita nikapata dharura nikaaga nikawaacha pale. tuliendelea na uhusiano kwa ahadi ya kuoana baada ya kujifungua lakini kuna vitu vili change wakati mwingine tukiwa out cm yake ikipigwa haipokei kwa baadhi ya calls akitoka ata kwenda "msalani" anaiacha nikichukua kuangalia nakutana na password hapo sina ujanja.
nikapata safari kikaz kwenda mbeya ni usiku nfika Moro make niliamua kusafr usiku akanpigia kwa kweli niliona cm ila nilipuuzia kwa mnajili nkifika mikumi ntampigia.
nilipofika mikumi nkampigia cm haipokelewi nikaendelea napiga kimya haipokelewi nikaendelea nikijua cm iko silence amelala.
asubuhi nimepiga haipokelewi nampigia shem akapokea anasema haloo imekatwa nikavumilia pamoja name hayo nikam text hakuna jibu nikajitetea hakuna jibu.
baada ya siku moja nikarudi break ya kwanza kwao nikamkuta yeye na mdogo wake wako kwa room yao hali niliyo mkuta nayo nilijikuta nafurahi hadi shem akashangaa ingawa najuwa alijuwa kilicho nifurahisha kumbe siku ile ananpigia cm alikuwa hosptl.
nilipomsalimia kimya nikamuliza shem tatizo nini make nimejitetea kutopokea cm sieleweki basi nikamwomba anipe kichanga angalau nibebe aksnambia amelala nikaona ananizingua nikamchukuwa nikawa namwangalia akanyanyuka kunisihi nimrudishe mtoto eti nitambemenda.
nikamuuliza nini maana kubemenda jibu ukikuwa utajua, akamchukua akamlaza naye akaendelea kulala na kuniambia kama ungejua umuhim wa mtoto ungepokea cm wanaojua umuhim wa mtoto walipokea nikamuuliza unamaana gani? maana yangu ni hiyo.
basi kwa kweli alinchanganya nikatoka nikaenda hadi nyumban shem akawa ananisihi nimsamehe dadake labda ni hasira tu.
nilikaa hata kazin sikuripoti nikjilalia kwa kuwa cm nayo ilikuwa haina charge nikaweka nililala hadi jioni kuja kuamka cha kwanza kuangalia waliontafta wakat nmelala nikaichukua nikakuta pmoja na missed call pia na sms nikafungua ya kwake nayo in some a hivi:samahani kwa kukudanganya huyu mtoto siyo wako na naomba ukae mbali mimi.
ingawa iliniuma sikutaka ufafanuzi kesho yake nlikwenda hadi kwao moja kwa moja hadi chumban kwao ckuongea na mtu yeyote nilimkuta amelala nikamfunua mtoto wakati ananshangaa nikamwambia asante nikamtakia kila la kheri nikatoa laki mbili
nikamwekea mtoto kwe nguo nikaondoka.
sasa mwaka umeisha anapiga cm sipokei akaandika sms anaomba tukutane namimi simpendi tena. naomba wadau mnishauri jinsi ya kumjibu bila kumuumiza ASANTENI..
 
Kataaa maneno usikatae uwito! Nenda kamsikilize anasemaje
 
any way mkuu kamuone ila ujue ana mtu tayari sii ajabu anataka kukuchuna jihadhari na hilo na kamwe usirejeshe mahusiano ya kimapenzi we baki ulivyo na kama una mpenzi mtambulishe kwake ili akuheshimu na aheshimu hisia zako pia
 
Asikupotezee muda huyo ni majanga, cheza naye mbali.
 
Hahahaaaa Mpaka umekuja kuomba ushauri Hapa ni kwasababu bado una mpenda ila unajivunga. Unatafuta comfort juu ya maamuzi yako ya kutaka kuonana naye

Samahani kwa kukukatisha tamaa maana nitakacho kisema hapa naamini ni Tofauti Na wewe ambavyo unajisikia.

"Achana naye,kimbia mbio na muogope kama ukoma,usithubutu kujenga Naye ukaribu,delete na block mawasiliano naye".

Nimeweka Kwenye quote Kwa msisitizo. Kazi Kwako sasa
 
​huu ----- sasa yaani nikae nasubiria kila wiki gazeti la shigongo
 
luckyline yaani mi nimeumizwa we unasema story za kutunga nyie ndiyo wale wale msio misimamo kwenye mahusiano mfyuuh.
Usijipendekeze kwake.

Mwandikie msg "Samahani ila sitaki kukudanganya. Mimi sio wako, kaa mbali na mimi"alafu tulia. Kama ana akili atakutumia kahela kadogo kwa M-pesa/Tigo pesa ili muwe sawa.
 
Last edited by a moderator:
Nenda kamsikilize anasemaje alafu utuletee mrejesho..
 
Back
Top Bottom