Sijawahi yaelewa kabisa madirisha ya aluminium, yamekaa kifakefake sana

Hii ni ya Aluminium au PVC?
Aluminium hiyo wameweka mikato katikati inaonekana kama pvc
Screenshot_20210911-185802_Instagram.jpg
 
Wengi wanaenda na trend tu,una hoja ambayo hata mie nimekuwa nayo.

Unakuta dirisha limekatwa tena 1ft partition isiyofunguka huko juu hivyo linafunguka 40% pekee.

IhwMY6Q6_400x400.jpg
 
Kwa kweli hii trend mpya ya madirisha ya Aluminium binafsi sijaielewa kabisa. Naona kama hayako classy kulinganisha na ya mbao nzuri kama mninga.

Muonekano wake haunivutii kabisa, naona kama ni kitu fake kinachong'aa. Shida nyingine ni yanafunguka nusu. Dirisha la mbao unalifungua full kabisa.

Bila shaka wenzetu walianza kutumia madirisha ya namna hii kwa sababu ya uhaba wa mbao na bei kubwa ya mbao na si uzuri wake.

Unayaonaje madirisha haya? Na huku kwetu dirisha la mninga na la aluminium ya ukubwa sawa lipi ni bei kubwa?
unayaelewa madirisha gani aisee, weka na picha.
 
Wakuu...

Kama kuna mtu anajua wanapotengeneza vigae anijulishe... Vile vya udongo kabisa...
Nahitaji kufahamu gharama zake.
 
Mninga ni gharama kubwa, huko rufiji wanachomea mkaa, huku mjini ni dhahabu.
Ushamba uliopitiliza, tumeacha vigae ambavyo haviingizi joto tunaweka mabati ya msauzi, ndio utajua mabeberu walikuwa na akili.

Unatoa dirisha la mbao unaweka la vioo tupu linalofunguka nusu, unahisi unajua kumbe hujui.
 
Mimi siyapendi sababu sehemu ya kuingiza hewa inakuwa nusu dirisha..

Kwa joto la dar alluminium ili ikufae uwe na air conditions vyumbani na sebulen
Zipo dizains nyingi, hata hyo ya kufunga na kufungua dirisha zima kama la mbao tu, so ni wewe kumuelekeza fundi tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom