Mchumia Rungu
JF-Expert Member
- Apr 26, 2013
- 1,434
- 821
Katika ulimwengu wa leo sijaona kitolewacho bure na kama kipo basi wapo waliokilipia. Hii ya Airtel na bure ya WTF naona kama ni zaidi ya wizi! Kabla huduma yao hii haijaja, kila nilipoweka kwa mfano sh. 500/= na kujiunga na kifurushi cha siku, walinipa dk 13 za kupiga mitandao yote, SMS 300 na 125M kwaajili ya mtandao wa internet.
Baada ya kuja huduma hii ya bure WTF, zile 125M kwaajili ya mtandao hazikai utakuta zimeisha ndani ya muda mfupi na kisha huduma yao inayoitwa ya bure ya WTF haipatikani tena! Hapa nafikiri kuna kawizi wanafanya ila wamekosea setting zao. Na nisilogwe nikaunga (tethering) katika computer, hizo mega byte 125 zit aishi kwa speed ya ajabu wakati awali nilikuwa nafanyia kazi kwa muda wa kutosha kabisa.
Tafadhali wadau tufahamishane kwa walioina huduma hii msaada. Natamani kufuta setting za Airtel internet lakini sijui nianze wapi. Simu ninayoitumia ni HUAWEI Y300. Sitaki kuuhama network huyu, Airtel. Nimeanza nanyi ndg zangu hapa JF lakini pia kama sitapata ufumbuzi nitawaendea wahusika ofisini kwao.
Natanguliza shukrani kwa majibu yote yatakayo kuja.