Hivi ni kweli Zuku na Airtel hushirikiana kusumbua wateja?

pye Chang shen

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
11,038
5,259
Hii itakuwa ni zaidi ya mara tano au sita kusumbuliwa na hawa jamaa,

Iko hivi kin'gamuzi cha zuku kimeisha, wanakutumia msg zaidi ya kumi kwa siku wakikutaka ulipe fasta ili usikose huduma,na kwa kuzingatia siku hizi kila kitu ni internet.

Unajikamua kupitia airtelmoney unalipa shs 69,000/=

Unasubiri zaidi ya saa huduma hamna, unapiga simu zuku kuulizia, wanakujibu malipo hayajafanyika, unapiga simu airtel wankwambia oooh tunaomba radhi malipo yako yananin'ginia hewani kwahiyo subiri masaa 24 ya kazi hela yako itarudi.

Unasubiri wiki nzima hakuna malipo kurudi wala huduma ya zuku, je huu sio uhuni?

Ni leo tu nimeongea na wahudumu wawili wa zuku, wakanijibu mbovu pamoja na kunikatia simu, nikiruhusiwa naweza kuweka majina yao hapa, sasa nauliza mie si nadai hela yangu? Wananiambia nenda airtel, nako nikajibiwa mbovu pia baada ya kupiga simu.

Hivi nataka ushauri nifanyeje? Au nichukue hatua gani?

Roho inaumaaaaaa mjue.

Hela ngumu mtaani na hawa jamaa wanatuibia mchana kweupeeeeee

Update:
Leo jioni muamala umefanikiwa kutumwa zuku na kazi zimeanza kama kawaida

Ahsante airtel ila line yenu najitoa.
 
Masaa 24 yalipopita nikaulizia nikaambiwa ni masaa 24 ya kazi, yaani siku tatu,
Hivu kweli nikae siku tatu wakizungusha hela yangu bila kunilipa interest?
 
Nimeamua nisubiri hela yangu, ikirudi tu, natupa kule line ya airtel naweka voda.

Na zuku nimeamua kujitoa na sasa nafunga ctv cable fibre.

Sitaki tabu na wezi mie
 
Hii itakuwa ni zaidi ya mara tano au sita kusumbuliwa na hawa jamaa,

Iko hivi kin'gamuzi cha zuku kimeisha, wanakutumia msg zaidi ya kumi kwa siku wakikutaka ulipe fasta ili usikose huduma,na kwa kuzingatia siku hizi kila kitu ni internet,
Unajikamua kupitia airtelmoney unalipa shs 69,000/=
Unasubiri zaidi ya lisaa huduma hamna, unapiga simu zuku kuulizia, wanakujibu malipo hayajafanyika, unapiga simu airtel wankwambia oooh tunaomba radhi malipo yako yananin'ginia hewani kwahiyo subiri masaa 24 ya kazi hela yako itarudi,

Unasubiri wiki nzima hakuna malipo kurudi wala huduma ya zuku, je huu sio uhuni?

Ni leo tu nimeongea na wahudumu wawili wa zuku, wakanijibu mbovu pamoja na kunikatia simu, nikiruhusiwa naweza kuweka majina yao hapa, sasa nauliza mie si nadai hela yangu? Wananiambia nenda airtel, nako nikajibiwa mbovu pia baada ya kupiga simu,
Hivi nataka ushauri nifanyeje? Au nichukue hatua gani?
Roho inaumaaaaaa mjueeeeee
Hela ngumu mtaani na hawa jamaa wanatuibia mchana kweupeeeeee
Pole sana iliwahi kunikuta, mimi nilikuwa nalipia king'amuzi cha Dstv way back 2018 niangalie world cup. Ukipiga Dstv unaambiwa hela iko pending tigo, ukicheki na tigo unaambiwa subiri masaa 72 hela itarejeshwa.

Ile hela mpaka leo sijarejeshewa. Fanya hivi wapigie customer care wa Airtel na zuku kisha warekodi, halafu wasanue kwenye page zao mfano FB nk.
 
Pamoja sana
 
Nenda mahakama ufungue kesi ya madai na fidia. Watakulipa parefu mno. Nilisha kutwa na Hilo. Sikuwa na haraka hata. Niliwafungulia kesi wanikuja kunibembeleza. Ila niliwambia acha mahakama iamuwe. Walinilipa Hela ndefu sana
 
Na ushahidi ninao wa jinsi kazi ilivyosimama kwa uzembe wao, kama hilo linawezekana ni bora sana,
Kama uko free unaweza kuniongoza njia za kupita kidogo japo kwa kuanzia
 
Back
Top Bottom