Sijawaelewa Airtel na bure yao ya WTF!

Utahamia mtandao gani wakati yote ina matatizo yanayofanana?

Hahahahaha! Mkuu mpaka sasa naona ni nafuu kidogo ya Vodacom maana hata mawasiliano haya nafanya kupitia Vodacom. Hawa wenye bure, ni bure kabisa!
 
Asante sana Mkuu! Hapa kinachoumiza ni udanganyifu unaofanyika. Na kama nilivyosema ulimwengu wa leo hakuna bure na kama ipo basi wako walioilipia unayodhani ni bure. Kinachosikitisha ni zile megabyte 125 kupotea ghafla ili hali mwanza nilikuwa nazitumia kwa muda mrefu!

Unasemje bure wakati unasema mwenyewe umesema unalipia jero?

Wakati ulipokuwa unatumia zaidi ulikuwa mji/jiji gani lakini ulipohamia Mwanza ikawa tofauti?
 
Unasemje bure wakati unasema mwenyewe umesema unalipia jero?

Wakati ulipokuwa unatumia zaidi ulikuwa mji/jiji gani lakini ulipohamia Mwanza ikawa tofauti?

Mkuu, jero ni gharama ya dk 13, SMS 300 na 125M. Shida hapo ni hizo megabyte huisha ghafla. Bure inayodaiwa ni hiyo huduma ya WTF. Aidha siko Mwanza na sijasema hivyo!
 
Hii mitandao ni full kizungumkuti, bora mimi natumia nokia tochi sipati adha hizo za internet sijui WTF,,,,,,,,

Ningekuelewa kama ungeniambia umerudi hapa petu pa zamani. Sitaki kukumbuka hii kitu.
ImageUploadedByJamiiForums1399141729.620391.jpg
 
Mkuu, jero ni gharama ya dk 13, SMS 300 na 125M. Shida hapo ni hizo megabyte huisha ghafla. Bure inayodaiwa ni hiyo huduma ya WTF. Aidha siko Mwanza na sijasema hivyo!

Ahsante mkuu.

Nina jamaa yangu anatumia hayo makitu sana anasema kweli hawapukuti MBs unazopewa.

Aidha hapo kwenye Mwanza nilifanya utani tu nilijua kabisa ni typing error badala ya mwanzo uliandika mwanza.
 
Ooh! Nashukuru sana kwa updates hizo. Nafikiri kwangu iko shida. Nimekosa muda wa kufika ofisi za Airtel kupata ufafanuzi. Lakini nadhani nitawaona kwani kwa sasa hatuwezi kukwepa huduma zao, japo ni gharama lakini zinaturahihishia mambo. Ni kweli, katika haraka na hasira unaweza kuandika hata matusi na usijue. Nashukuru kwa kunisoma vile nililenga kusema. Asante!
 
Back
Top Bottom