Sijaona mahala Spika Tulia Ackson alipoisigina Katiba ya JMT. Mnaolalama mnalalama bila kutumia busara

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Kwa taifa letu katiba ndio mwanzo na mwisho juu ya uendeshaji wa nchi. Kugawa madaraka ya mihimili na kuwapa wananchi haki zao.

Hii ni kwa sababu taifa letu lina katiba iliyoandikwa. Yaani written Constitution.

Haina ubishi kuwa ni kwa mujibu wa katiba ya JMT mbunge akifutwa uanachama basi ubunge wake unakoma. Na hii ni kwa mujibu wa ibara ya 71(1)(e) ya katiba ya JMT.

Lakini ibara ya 107A(1) ya Katiba ya JMT inasema wazi kabisa na kutanabaisha kuwa Mahakama ndio kitakuwa chombo pekee cha kutoa haki.

Sasa mlitaka Spika Tulia ndio aseme Mdee na wenzake sio wabunge? Suala lipo mahakamani?

Muwe mnatumia akili sometimes.
 
Wewe kweli changi wa malunde
Nini kilitangulia kati ya kufukuzwa uanachama, kutolewa bungeni na kwenda mahakamani????.
Ivi jambazi akiwa jela huku anatumika kufungua Afu akaamua kukata rufaa huwa anatolewa kwanz jela rufaa yake ikisikilizwa?
Unajua taratibu za rufaa? Mfano wako hauko relevant. Mpuuzi mkubwa
 
Badala ya kuniita mpuuzi mkubwa ungeelezea hizo taratibu za rufaa ili siku nyingine nisiwe mpuuzi. Vinginevyo unadhihirisha uchangu wako.
Matusi hayasaidii sana.
Ulishaona mtu kapigwa mvua akikata rufaa anaachiwa papo hapo?
 
Unachokisema wewe ni kuhalalisha uvunjifu wa sheria! Unafanya hivyo kwa sababu unazozijua na wanaokutuma ! Japo mm siyo mpuuzi kama unavyoniita.

Alifukuzwa wabunge kina Ngwali wa Cuf pale bungeni. Waliachwa waendelee na ubunge huku rufaa zao zikisikilizwa?
Labda itakuwa walichelewa kukata rufaa. Au kupinga kutimuliwa
 
Labda itakuwa walichelewa kukata rufaa. Au kupinga kutimuliwa
Hawakuchelewa kukata rufaa. Lengo la siasa za wakati huo ilikuwa ni kukigawa Cuf lipumba na maalimu
Sisi sote ni watanzania tunafuatilia mambo tupo hapa hapa nchini na shule tulienda bila kufeli wala kuiba mitihani.
Nasari alifukuzwa ubunge na alienda mahakamani? Aliruhusiwa kuingia bungeni akingoja maamuzi ya mahakama?
 
Mimi nazungumzia katiba inavyosema. Hayo mengine weka ushahidi hapa sio kuaharisha maneno praaaaaa
 
Mimi nazungumzia katiba inavyosema. Hayo mengine weka ushahidi hapa sio kuaharisha maneno praaaaaa
Niweke ushahidi wa picha labda! Najua unajua ila unajifurahisha tu. Wale wabunge wa Cuf waliruhusiwa kukaa bungeni huku wakisubir uamuzi wa mahakama?
Yule sabaya alitolewa kwanza nje akisubir rufaa yake?
Kama jibu hapana manake wale walitakiwa wawe nje ya bunge mpaka mahakama itakkapo amua vinginevyo.
Hapa tungesema spika havunji katiba .vinginevyo ni ujinga tu
Wapi? Weka hapa huo ushahidi?
Ushahidi? Ulitaka sasa niweke na hukumu ya mahakama labda
 
Back
Top Bottom