Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,742
- 40,874
Na. M. M. Mwanakijiji
Inawezekana hili jambo lilinipita; kwamba, vyama vya siasa vina vyuo na shule zake na sasa wanafunzi wake wanaanza kuhitimu. Nimesoma kuna mahafali sijui ya CCM mahali gani mengine ya Chadema sehemu nyingine, na labda kuna mahalafi ya ACT, CUF, UDP na vyama vingine.
Nisichoelewa ni kuwa hivi vyama vilianzisha vyuo au shule lini ambapo wanaosoma ni wanachama wao au watoto wa wanachama wao peke yao? Najua CCM iliwahi na bado ina baadhi ya shule za Wazazi, lakini sijajua kama ina vyuo vya wazazi vinavyotoa elimu ya juu. Na sina uhakika kama wazazi wa CHADEMA na wenyewe wana shule au vyuo vyao.
Hivi vyuo na shule za vyama vya siasa ambapo wanafunzi wake ni wanachama wa vyama hivyo tu - ndio hawa wanahitimu - ziko wapi na zinaongozwa vipi?
Ila kama ni shule na vyuo hivi hivi vinavyochukua watu wa kada, na mirengo mbalimbali ya kisiasa kwanini wanaosoma pamoja katika taifa; ni vipi tena kuna mahafali nje ya yale ambayo yanafanywa na shule au chuo kizima kwa wanafunzi wote? Siyo, kwamba tutafika mahali tutakuwa na kuhitimu JKT kwa mirengo ya vyama vya siasa?
Au hiki kinachoitwa "mahafali" kwa ufupi ni maigizo ya kuhitimu ya waliokwisha hitimu na wengine? Kwamba, hawa walishahitimu na kufanya mahafali na wanafunzi wengine ila ili wajione ni tofauti zaidi basi wameandaa mahafali ya kisiasa ambayo hayahusiani na elimu waliyoisoma?
Kama hili ni kweli, itakuwa vibaya nikisema kuwa huku ni kuchizika kwa taifa zima? Hivi wasomi wetu wameshindwa kuona falacy ya kiakili iliyoko kwenye mahafali yasiyo mahafali? Kama kinachofanywa ni sherehe za kuagana au tafrija tu ya watu wa chama fulani kwanini wayaite mahafali haya; kama siyo uchizi wa kisiasa (political insanity) iliyopitiliza tuite nini basi?
Wizara ya Elimu inaruhusu vipi kuwepo na mazingaombwe haya ambayo hata yanaelekea kugawa watu na kuleta migongano wala isiyo na ulazima. Mahafali yafanyike chuoni, au shuleni kwa wanafunzi wote wahitimu. Sherehe nyingine watu wafanye kama sherehe zao tu lakini wasijichanganye wenyewe kuwa ni sherehe nyingine za mahafali kwani hatari yake ni kuendekeza siasa mno hata mahali pasipostahili.
Futilia mbali mahafali ya CCM, ya CHADEMA, ya TLP na madudu mengine haya yanayoitwa "mahafali" ili kuondoa migongano mingine isiyo ya lazima. Wanaotaka kufanya sherehe zao wafanye sherehe zao lakini siyo kurudia mahafali vinginevyo utakuwa ni uchizi wa kitaifa.
Tunaanza kuendekeza mno siasa hadi mwisho tutakuwa na makanisa na misikiti ya kisiasa; masoko na maduka ya kisiasa; na mwisho wa siku tutakuwa "sisi" na "wao" kwenye mambo ya msingi na tutashangaa tumefika fika vipi.
Kama kwenye shule na vyuo vyenu miaka yote ya elimu hamkubaguliwa kupata elimu; vipi kwenye kuhitimu mjibague.
Uchizi wa kisiasa huu.
Labda mnieleweshe umuhimu wake saaaaaaana (kwa sauti ya Baba Mshamu).