Zimesalia Siku 7, Chuo Kikuu Huria hakijatoa orodha ya wanaohitimu, Watumishi wa Serikali tunaweza kukosa ruhusa

Nyakijooga

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
252
454
Mimi ni mmoja wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria (OPEN University -OUT) ambao tunatarajia kuhitimu Shahada Mwaka huu na tayari Chuo kimepanga mahafali yafanyike Mkoani Kigoma tarehe 5 Disemba 2024.

Kinachonikwaza mimi na wenzangu wengi ni kuwa hadi sasa imesalia wiki moja tu kufanyika kwa mahafali hayo, lakini mpaka hawajaweka wazi majina rasmi ya Wanafunzi ambao wanatarajiwa kuhitimu.

Kwa kawaida OPEN huwa wakifanya mahafali yao yanahusisha matawi yote Tanzania nzima, hivyo uwe unasoma Tawi la Mtwara, Lindi, Songwe au Mbeya unalazimika kwenda Kigoma.

Asilimia kubwa ya Wanaosoma OPEN ni Wafanyakazi, wakiwemo wa Serikali na Taasisi binafsi, hivyo kama zimesalia siku chache ambazo ndani humo kuna Public Holiday kama hivi leo (Novemba 27, 2024) pamoja na wikiendi (Jumamosi na Jumapili), wanategemea wahusika watapata ruhusa lini?

Mfano mimi na wenzangu ni Watumishi wa Serikalini, hatujajua kama tupo kwenye listi au la licha ya kuwa tuna vigezo vyote vya kuhitimu, ukimya wa OUT unamaanisha wanataka tukose hayo mahafali?

Inakera sana kuona Uongozi wa Chuo umekuwa kimya, Ijumaa iliyopita kuna majina yalitoka na kusambaa mtandaoni lakini hawakusema kama ndio official au la tena yalikuwa na watu wachache.

Naomba Uongozi wa OPEN University wawajibike katika hili, vinginevyo watatuumiza sisi tunaotoka mbali na Kigoma kwa kuwa hatujui hatima yetu na kama unavyojua taratibu za Serikali kuomba ruhusa huwa zinachukua mchakato mrefu.
 
IMG-20241127-WA0008.jpg

Mtoa mada ni muongo, mimi sio mwanafunzi wa OUT ila niliona hio orodha inatembea kwenye magroup ya WhatsApp.
 
Sasa ndg mheshiwa, magroup ya wasap ni taarifa rasmi?
Wewe ni kilaza, taarifa rasmi imetolewa kwa kufuata utaratibu uliowekwa. Aliesambaza kwenye magroup yao ya WhatsApp alipata huko huko zinakotakiwa kuwekwa taarifa. Mtoa mada atafute hio taarifa.
 
Wewe ni kilaza, taarifa rasmi imetolewa kwa kufuata utaratibu uliowekwa. Aliesambaza kwenye magroup yao ya WhatsApp alipata huko huko zinakotakiwa kuwekwa taarifa. Mtoa mada atafute hio taarifa.
**** wewe
 
Back
Top Bottom