Sijaelewa katuni hii ya Masoud Kipanya. Tusaidiane tafadhali

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,829
21,460
Ninaomba aliyemuelewa Kipanya tafadhali

73E8FD71-D282-4DA9-9C6A-8A432EC54F7B.jpeg
 
Huyo ni mmoja kati ya chawa wengi wa hangaya anaye toboa mtungi ili akinge asali asepe, sikuizi hawalambi wanachota na kukinga, pembeni ni mwenye nyumba anaangaika kujaza mtungi nyumba nzima ipate asali kumbe chawa wamesha toboatoboa vibaya, infact uyo unayemuona anamtungi wake binafsi mgongoni ni Trab and Trat.
 
Kwa kifupi niii, mwenye kuhangaika na mtungi wa maji hakuna afanyalo kama kiongozi. Lazima uwe na uhakika kuwa pakacha unalotaka kuwekea maji halivuji.
 
Huyo mtoboaji ni nani?.
Let’s have a sharp mind through these three guys..Wacha nipunguze sauti ni NAPE,JANUARI & NCHEMBA wakiongozwa na mstaafu wa awamu ya nne JMK anayepinga aweke wazi kuwa sio hao na ikiwa anaowakutuambia ni nani na nani aseme!!
 
Tenga la bluu kubwa ndio serikali halafu mama katoka kuchukua mikopo na misaada nje anaenda analeta serikalini lakini sasa hajui kuna watendaji wake wamejificha serikalini humo humo na mabegi yao wao kazi kubwa ni kutoboa na kuiba ile mikopo bila mama kujua hivo atakuja kupiga hesabu alichokiweka hakipo na hakuna la maana lolote lililofanyika maana awamu yake hii ndio watu wanaiba sana kama wamelaaniwa
 
Mama anajitahidi kujenga nchi ila wafanya biashara wanamuhujumu vibaya sana.
Sahihi mama ana hujumiwa na wafanyabiashara, huyu mwenye begi la Ice cream kama wale vijana wa bakhresa ni kielelezo cha wafanyabiashara

Sasa hawa wafanyabiashara hasa wadogo ambao wana tengenezewa mazingira mazuri ya kufanya biashara lakini wao hawa thamini juhudi hizo
Mama anajitahidi kujenga nchi ila wafanya biashara wanamuhujumu vibaya sana.
 
Let’s have a sharp mind through these three guys..Wacha nipunguze sauti ni NAPE,JANUARI & NCHEMBA wakiongozwa na mstaafu wa awamu ya nne JMK anayepinga aweke wazi kuwa sio hao na ikiwa anaowakutuambia ni nani na nani aseme!!
Mpunguze JMK maana ni buzi lake hawezi muhujumu..

Ila hao wengine ni kweli maana wajuaji mno
 
Let’s have a sharp mind through these three guys..Wacha nipunguze sauti ni NAPE,JANUARI & NCHEMBA wakiongozwa na mstaafu wa awamu ya nne JMK anayepinga aweke wazi kuwa sio hao na ikiwa anaowakutuambia ni nani na nani aseme!!
Kivipi hao uliowataja wanaihujumu nchi?
Ukame ulitaka January afanyeje?
Mafuta dunia nzima yamepanda ulitaka mwigulu afanye nin?
 
Mwanamke:
Mh Rais

Alichobeba na kilichomo ndani:
Jitahada za ujenzi nchi

Pipa kubwa:
Nchi

Meza ya pipa:
Hali mbaya nchi iliyoikalia

Matobo ya kwenye pipa:
Channels za upenyo za kujikatia mali za taifa
ambazo ni kijana anaendelea kutoboa tena

Kijana:
Mhujumu jitihada

Pipa la mgongoni:
Miliki yake binafsi anayotaka kuijaza

Nyundo:
Nguvu na upeo alionao

Tyrone KG
 
Back
Top Bottom