SIJABAHATIKA KUMUONA MZEE MBARAKA MUISHEE

msolopaganzi1954

JF-Expert Member
Nov 20, 2018
764
378
.......dah Miongoni mwa Majuto yangu ni kutobahatika kumuona mzee huyu Gwiji Ya Music Tanzania.
Dah Kibao Kama kile kinachomuhusu MASOUD? HATARI SANA
 
Wenzio alikuja Korogwe chuoni akatupigia live wakati anaelekea Kenya. That was 1978 na ndo hakurudi hai. We were lucky. Mkuu wa chuo wetu walisoma wote na alikuwa rafiki yake.
 
Kaka Acha, Huyu mtu was very Gifted kaka,.
Nimebahatika kuona Kaburi Lake Tu
 
.......dah Miongoni mwa Majuto yangu ni kutobahatika kumuona mzee huyu Gwiji Ya Music Tanzania.
Dah Kibao Kama kile kinachomuhusu MASOUD? HATARI SANA
Nakumbuka siku ya Januari 12, 1979 ulimwengu wa muziki Tanzania ulitikiska kwa simanzi baada ya kusikika kifo cha mwanamuziki huyo, mpiga gitaa muimbaji, mtunzi na kiongozi wa bendi wa miaka mingi na ambaye bendi yake ilikuwa imepiga karibu kila wilaya ya nchini Tanzania. Taarifa ziliingia jioni ya siku ile kupitia redio ya Taifa kuwa nguli huyu alifia katika hospitali katika jiji la Mombasa nchini Kenya muda wa saa 1:55 jioni kufuatia ajali ya gari.

Kwa maelezo ya Zebedee Japhet Kinoka au maarufu kama Super Zex ni mwanamuziki mkongwe, siku ya tarehe 12 Januari 1979 alikuwa anatoka maeneo ya Kisaunikumtembelea Mtanzania mwenzake aliyekuwa na hoteli huko, ambaye pia walitoka kijiji kimoja Maramba huko Tanga. Anasema alipofika karibu na Kongoya Church aliona gari aina ya Peugot 404 nyeupe ikitoka upande wa Bush Bar na kwa spidi kali ikaenda na kuligonga lori moja lililokuwa likitokea upande mwingine.

Ilikuwa mchana kiasi kama saa 7 hivi. Watu wakakimbilia kungalia ajali akiwemo yeye. Na mara moja akamtambua Mbaraka na kuwambia watu kuwa huyo ni mwanamuziki Mtanzania anaitwa Mbaraka Mwinshehe. Katika gari lile kulikuweko watu watatu Mbaraka alikuwa amekaa mbele pamoja na dereva. Dereva (maelezo ya baadaye yalimtambua kuwa alikuwa rafiki wa Mbaraka na mkazi wa Moshi aliitwa Omari Abdi, kuna maelezo mengine kuwa Abdi pia alikuja fia hospitalini si pale kwenye ajali) na abiria aliyekuwa nyuma walikufa palepale, ikalazimika kuanza kukata mabati ili kumuondoa Mbaraka aliyekuwa amebanwa miguu katika gari lile lililoharibika, yeye alikuwa bado hai.

Wakati kazi hiyo inaendelea Zebedee alikimbilia Kengeleni Bar ambapo Jamhuri Jazz Band (Bendi ya Watanzania) ilkuwa ikipiga muziki nakuwambia kuwa mwenzao kaumia sana, nao wakatoka mbio, wakiwemo akina Harrisson Siwale. Mbaraka aliweza kutolewa kwenye gari na kupelekwa kwenye hospitali ya Makadara. Zebedee pia akatumwa kuwafuata wanamuziki wa bendi ya Super Volcano ambao wakati huo walikuwa wakipiga Zambia Bar, wanamuziki walipofika hospitali wakaambiwa watoe damu na wakaanza kukwepa kutoa damu kwa visingizio mbalimbali.

Muda si mrefu Mbaraka Mwinyshehe akafariki. Mbaraka alifarika 12 Januari 1979 akiwa na umri mdogo wa miaka 34 tu. Kwa kuwa mpaka wa Kenya na Tanzania ulikuwa umefungwa wakati huo kutokana na mgogoro kati ya serikali za nchi hizi mbili, mwili wa Mbaraka alisafirishwa mpaka mpakani na kupokelewa na ndugu marafiki na Maafisa wa Wizara ya Utamaduni.

Mbaraka Mwinyshehe alizikwa Mzenga Kisarawe.
 
Ahsante kaka
 
Uko sahihi sana
 
Back
Top Bottom