Niliwahi pata kasheshe ya kufa mtu. Nilikuwa bado mgeni mgeni. Profesa wangu alikuja akanikuta nimekaa sina hili wala lile akaniambia SYB let's go grab some lunch. Sasa nikafikiri kuwa kwa vile yeye ndo kaniambia basi atakwenda kulipa bila shaka.
Tumepiga msosi tumemaliza namwona huyoo amekwenda akalipa bili yake huyoo akatoka nje kunisubirisha. Na mfukoni sikuwa hata na wallet. Kikawa kimbembe!
Ndiyo nikajifunza utamaduni wao. Hata binti ukimtoa out anakuja amejiandaa kulipa nusu labda uwe muungwana umkataze. Na hii inasaidia sana mtu kutoagiza wines ghali hizi za $100+ kisa tu kaona kuna mtu anamlipia. Nilipenda sana utamaduni wao huo.
Sisi huku ukimpata mtu limbukeni ambaye hana exposure ukampeleka sehemu ya maana basi anaona leo ndiyo kapata bahati. Ataagiza vitu ghali ambavyo angekuwa yeye ndo analipa asingevigusa.
Ila kama uko vizuri na ukamhakikishia mtu kuwa aagize cho chote, siyo vizuri tena kuja kumgeuka kama jamaa yetu alivyofanya. Na mabinti wenye uzoefu atamwacha kwanza jamaa aagize na yeye atachukua hints kutoka pale. Na kama wamezoeana anaweza tu kuuliza point blank kwamba una uhakika naweza kuagiza cho chote?