Simiyu Yetu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2013
- 18,949
- 4,643
Mtajibeba mwaka huu poleni sana chadema na mda bado upo mtapata shida sana mwaka huu.Ila wewe wanakutekenya...
Mtajibeba mwaka huu poleni sana chadema na mda bado upo mtapata shida sana mwaka huu.Ila wewe wanakutekenya...
Umeonaefumbo mfumbie mjinga,mjanja huling'amua ng'amuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
Kwaiyo maovu ya serikali yasifichuliwe??
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Umesomeka Mpigilie. Nasikia eti hawa hawa CHADEMA wameamua kuchuja watu/MAWAZIRI watakaonana na Obama kwa kushirikiana na FBI.
Kujichotea mil 140 ruzuku ya chama na kwenda kutumbua na mchumba israeli
Finally nimejua ni kiasi gani vijana wa Lumumba wana uwezo mdogo wa kuchambua na kuchuja hoja. Kwahiyo ninyi kwa akili yenu mmeona mleta hoja anawasifia?? hahah, kweli CCM inawatuma mamburula kutetea chama.Huwezi kupenda chadema wakati inaua watu kwa mabomu.
Narudia tena SIIPENDI CHADEMA na sitakuja kuipenda chadema kama haitajirekebisha.
Nasema hivyo kutokana na sababu zifuatazo.
1. Chadema imekua inaongoza nchi kinyume na taratibu. Tunajua kwamba kwenye uchaguzi mkuu uliopita CCM "ilishinda" uchaguzi huo na kua na "haki" ya kuongoza serikali na vyombo vyote vya usalama.
Lakini kwa masikitiko makubwa CHADEMA wamejitwalia jukumu hilo bila kufuata sheria na taratibu za nchi hii.
Mfano ni pale chadema inapotumia polisi kuwadhuru wananchi na kuwapiga mabomu wananchi kwa kutumia polisi.
2. Chadema kutumia mabavu kuliongoza BUNGE ambapo kisheria ilibidi bunge liongozwe na CCM yenye wabunge wengi, speaker,naibu speaker na wenyeviti wa bunge kutoka CCM.
Hii inajidhihirisha pale ambapo CHADEMA wamekua kimbelembele kutetea maslahi ya wananchi wakati hii kazi ilibidi ifanywe na CCM yenye wabunge wengi+serikali. Huu ni uporaji wa haki ya msingi unaofanywa na chadema kwa wabunge wa ccm.
3. Chadema kwa makusudi kabisa imekua ikiwachonganisha wananchi na serikali yao tukufu ya CCM.
Kitendo cha chadema kufichua maovu ya CCM na kuyaweka wazi kwa wananchi ni uchonganishi mkubwa na unawafanya wananchi kutoipenda serikali yao "halali" iliyopo madarakani.
Mfano mzuri ni list of shame, KAGODA, MEREMETA, DEEP GREEN e.t.c
4. Kitendo kiovu kinachofanywa na chadema kuilazimisha CCM kuacha sera zake na kutekeleza sera mbaya za chadema ni kitendo ambacho hakivumiliki na kinafaa kupingwa na wananchi wote. Wanancchi tumekiamini chama chetu tukufu ccm na tukakipa "kula" za kutosha ili kiingie madarakani na kutekeleza sera zake ilizokua inazinadi majukwaani. Matokeo yake chadema imefanya hila na michezo michafu ya kisiasa na kuilazimisha ccm kutekeleza sera za chadema.
5. Chadema imeiweka nchi rehani kwa kulazimisha USALAMA WA TAIFA kuripoti kwake badala ya kuripoti kwa serikali tukufu ya CCM.
Huu ni uhaini na wapenda haki wote inabidi tupaze sauti kukemea hili suala.
Haiwezekani wanausalama watiifu wafanye mauaji yanayofuata sheria halafu wale wanausalama wasiofuata maadili wakapeleka taarifa chadema. Hii sio sawa kabisa, kunaiweka nchi yetu kwenye hatari kubwa sana.
Naomba niishie hapa ila natoa rai kwa watu wote wenye uzalendo na nchi hii kuipiga vita CHADEMA kwa nguvu zote.
Kaandikishe jina kati ya watu watakaomshika obama mkono..Nasikia wameandaa vijana kuzomea msafara wa obama, watachukuliwa mzega mzega kwenda GWANTANAMO wanafikiri ni wanavyowachezea POLISI wetu.
Mtajibeba mwaka huu poleni sana chadema na mda bado upo mtapata shida sana mwaka huu.
HATA MIMI NAICHUKUIA SANA CHADEMA KWASABABU ETI INALAZIMISHA SENDOFF YAKE TAYARI KWA NDOA YA MKEKA 2015!
1. Kwanza kabisa haipotayari kuona CCM inaachia madaraka kwa namna yoyote ile. Mifano ipo na kwa uchache ni kule Zanzibar pale ambapo CUF waliungwa mkono na wananchi lakini hawakuwahi ongoza dola ikiwa ni pamoja na kupigwa vilivyo mpaka wengine wakatorokea Mombasa na kilichofuata ni ndoa ya mkeka. Angalieni Zimbabwe pale Morgan aliposhushiwa kipigo vilivyo na baadaye wakajifanya wasuluhishane eti mwingine awe rais na mwingine waziri mkuu, huko mbali mno, Kenya hapo Kibaki alipobwagwa alijitangaza jioni jioni na mambo yalipozidi unga akamkaribisha mpinzani wake Odinga kuwa waziri mkuu. Ni kwa mtindo huo hizi vurugu zote mnazoziona kwa wanaCHADEMA, ni mpango mkakati wa kuandaa ndoa ya mkeka 2015. Sasa hivi nyie CDM mnafanyiwa SENDOFF! Na wananchi wote tutashangilia kuwaona mnapendana na CCM kwa sababu mnawalazimisha kuongea uwongo toka bungeni hadi mitaani. Siku si nyingi mtawalazimisaha kuongea ngonjera za vita ili mpate kufunga nao ndoa.
Naamini mpo makini kwani kwa ufahamu wangu serikali za kimkeka zina tija sana kwa maendeleo ya mabwenyenye. Na pia mnawalazimisha CCM kutanguliza maslahi binafsi kabla ya taifa ndio maana miaka 50 baada ya uhuru, mmeilazimisha serikali ya CCM kuamuru baraza la mitahani kuRE-SEAT" mamba ambayo tuliyazoea kwa watu vilaza kama kamanda wetu maarufu nepi na mzee mguu chemba na jamii wanayofanana nayo.
2. CDM mnawalazimisha CCM kuwatia hofu wananchi kuthibitisha usemi wao kwamba vyama vingi vinaleta vita kama nyimbo za ma thread (kamanda wetu maarufu kabla ya yule jamaa aliye ondolewa asubuhisubuhi na mtalaamu wa koleo za teeth za yule mnyama mnee) alipokuwa anazunguka miaka ya 90 kutafuta kura ya maoni juu ya vyama vingi. Kwa taarifa yenu ile kura walikusanya makada wa CCM na mahala pengine watu walitoa maoni yao baada ya kutiwa hofu za kijinga za akina ma thread wakishinikizwa na viongozi wa CDM wa wakati huo.
3. CDM wanailazimisha CCM kuleta vurugu mahali popote ambapo huwa na hali mbaya kisiasa ili kuchakachua matokeo au kufuta uchaguzi. Mtakumbuka mwaka 1995 yaliyotokea DSM na mahali pengine pengi wakati wa chaguzi. Juzi limetokea ARS. Nashindwa kuelewa kama kweli hawa watu wana nia ya dhati na taifa letu, kwani nchi nyingi zilizoendelea wameruhusu mawazo tofauti katika michakato yao ya kuongoza na kundeleza mataifa yao. Ni nchi za kiafrika ikiwemo Tanzania zisizojali maendeleo zaidi ya Ubwenyenye, lakini yote haya CCM wanafanya kwa kulazimishwa na CDM.
4. CCM kwa kuhakikisha kuwa hawana usongo sana na serikali za ndoa za mkeka kama kwa Mugabe kule Zimbabwe, wameanza chokochoko kwamba serikali tatu zinazotiliwa upatu na tume ya katiba zisikubaliwe kwani wanajua kabisa ndani ya serikari ya Tanganyika hakuna nafasi ya serikali za ndoa za mkeka, ahaaaaa hii mijitu!
5. Katika kusimamia hilo watakalo CDM, inasadikika CCM wameongeza jumuiya nyingine ndani ya chama chao iitwayo POLICCM, watu waongooooo, sijui ni kweli?
Nawashauri wapenda amani na wenye nia njema na taifa letu kuliona hilo (ndoa ya mkeka 2015 kati ya CDM na CCM, CDM wakiwa nyumba ndogo kama walivyo wenzao CUF sasa hivi) ambalo pamoja na mambo mengine ya kimaslahi binafsi, lipo nyuma ya pazia. CCM wanapenda nyumba ndogo! lakini kwa hili sijui?
Finally nimejua ni kiasi gani vijana wa Lumumba wana uwezo mdogo wa kuchambua na kuchuja hoja. Kwahiyo ninyi kwa akili yenu mmeona mleta hoja anawasifia?? hahah, kweli CCM inawatuma mamburula kutetea chama.
Naona mleta hoja kawapiga chenga kali sana vijana wa Lumumba!
Umezoea kushikwa sana nini? Au kundi moja na MWENYEKITI WENU?Kaandikishe jina kati ya watu watakaomshika obama mkono..
Chadema wana wafuasi wengi, wewe mtu mmoja usipo ipenda au kuiunga mkono chadema haita yumba kamwe, kwanza hata chama unacho kipenda hukisaidii kwa lolote ilikiwepo porojo ndio nyiiingi,
Sasa mbona mmeingia chaka?Hivi wanachadema huyo ndiye munamwamini kwa propaganda? Tehe teh teh teh. Alivyojikanyaga hapo mara ajikune , mara awashwe sasa nani ambaye hajui kuwa alikuwa anatetea vijisengi vya mtaa wa ufipa?
Kuna watu humu wanasoma headline tu na kuweka comments. Mleta maada yupo wazi kabisa katika hoja zake. Lakini sishangai, maana hata vijana wa Lumumba wameingia chaka ile mbaya.Hebu rudia kusoma kwa umakini jamaa alichoandika alafu linganisha na ulivyojibu. Jifunze kuconnect dots mkuu.
Chadema sijui matamko yao yamewaisha wiki hii sijasikia au watatoa kesho.