Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 54,023
- 43,168
Teh teh teh teh.....usinichafulie mkuu wa chuo changu bhana.
Posta ndo kuna vyuo hivyo?umekaririshwa.....shauri yako.
Basi nakusubiri Magomeni au na penyewe nimekaririshwa, teh teh teh.
Teh teh teh teh.....usinichafulie mkuu wa chuo changu bhana.
Posta ndo kuna vyuo hivyo?umekaririshwa.....shauri yako.
Basi nakusubiri Magomeni au na penyewe nimekaririshwa, teh teh teh.
Mbado...........by Mr Ebbo!
Narudia tena SIIPENDI CHADEMA na sitakuja kuipenda CHADEMA kama haitajirekebisha.
Nasema hivyo kutokana na sababu zifuatazo.
1. CHADEMA imekua inaongoza nchi kinyume na taratibu. Tunajua kwamba kwenye uchaguzi mkuu uliopita CCM "ilishinda" uchaguzi huo na kua na "haki" ya kuongoza serikali na vyombo vyote vya usalama.
Lakini kwa masikitiko makubwa CHADEMA wamejitwalia jukumu hilo bila kufuata sheria na taratibu za nchi hii.
Mfano ni pale CHADEMA inapotumia polisi kuwadhuru wananchi na kuwapiga mabomu wananchi kwa kutumia polisi.
2. CHADEMA kutumia mabavu kuliongoza BUNGE ambapo kisheria ilibidi bunge liongozwe na CCM yenye wabunge wengi, speaker,naibu speaker na wenyeviti wa bunge kutoka CCM.
Hii inajidhihirisha pale ambapo CHADEMA wamekua kimbelembele kutetea maslahi ya wananchi wakati hii kazi ilibidi ifanywe na CCM yenye wabunge wengi+serikali. Huu ni uporaji wa haki ya msingi unaofanywa na chadema kwa wabunge wa ccm.
3. CHADEMA kwa makusudi kabisa imekua ikiwachonganisha wananchi na serikali yao tukufu ya CCM.
Kitendo cha chadema kufichua maovu ya CCM na kuyaweka wazi kwa wananchi ni uchonganishi mkubwa na unawafanya wananchi kutoipenda serikali yao "halali" iliyopo madarakani.
Mfano mzuri ni list of shame, KAGODA, MEREMETA, DEEP GREEN e.t.c
4. Kitendo kiovu kinachofanywa na CHADEMA kuilazimisha CCM kuacha sera zake na kutekeleza sera mbaya za CHADEMA ni kitendo ambacho hakivumiliki na kinafaa kupingwa na wananchi wote. Wanancchi tumekiamini chama chetu tukufu ccm na tukakipa "kula" za kutosha ili kiingie madarakani na kutekeleza sera zake ilizokua inazinadi majukwaani. Matokeo yake CHADEMA imefanya hila na michezo michafu ya kisiasa na kuilazimisha CCM kutekeleza sera za CHADEMA.
5. CHADEMA imeiweka nchi rehani kwa kulazimisha USALAMA WA TAIFA kuripoti kwake badala ya kuripoti kwa serikali tukufu ya CCM.
Huu ni uhaini na wapenda haki wote inabidi tupaze sauti kukemea hili suala.
Haiwezekani wanausalama watiifu wafanye mauaji yanayofuata sheria halafu wale wanausalama wasiofuata maadili wakapeleka taarifa chadema. Hii sio sawa kabisa, kunaiweka nchi yetu kwenye hatari kubwa sana.
Naomba niishie hapa ila natoa rai kwa watu wote wenye uzalendo na nchi hii kuipiga vita CHADEMA kwa nguvu zote.
Hongera mkuu fish sasa ni Jicho-la3,la kwanza ngumu kumeza,la pili mayai sana,sasa la3 hadi mfugo unaishi,kweli evolution ime-take place,pole sana sasa hivi wanaona mbali hadi mihogo pale inapohifadhiwa...Jichola3Umezoea kushikwa sana nini? Au kundi moja na MWENYEKITI WENU?
Kama ndio hivi hawa CHADEMA noumaaa!! Yaani mpaka Kinana wamempandikiza wao? Intelijensia yao basi ni KALI!!Afu CHADEMA imewaelimisha wananchi na kuwaondoa usingizini kiasi kwamba wanahoji mambo tofauti na zamani ambapo kila kitu walikuwa wanakubali tu.. matokeo yake wamesababisha nchi haitawaliki na kumfanya raisi wetu "mpendwa" awe anashinda angani na nje ya nchi kwa sababu kero zimezidi.. Wamewafanya hadi viongozi wetu wa ccm kuacha kueneza sera zetu tukufu na kutumia muda mwingi kujibu hoja za CHADEMA majukwaani. CHADEMA walimtuma Kinana kuwang'oa tembo meno halafu wakampenyeza awe katibu mkuu wa chama chetu afu baadae wakafichua siri ili ionekane ni katibu wa ccm amehusika.. CHADEMA wamefanya hadi serikali "sikivu" inashindwa kutekeleza ahadi zake na matokeo yake viongozi wetu "wapendwa" wanazomewa kila kona. Hawa CHADEMA ndio walimwita waziri mkuu -------- afu wakamwambia jaji afute kesi... Kweli CHADEMA hawafai.. huko Mtwara wamewaagiza JWTZ kuteka na kupiga raia hadi gesi itoke... naunga mguu hoja
Hoja hapa Siipendi Chadema, akili ndogo inaongoza Akili kubwa, Mbowe darasa la saba, Lema darasa la saba wanawaongoza akili kubwa Prof. Baregu, Prof. Safari.
Yani wewe huna akili kabisa unachojaribu kutuambia ni kuwa chadema imekosea kuwaelimisha watanzania wengi ambao haki,rasilimali zao zimekuwa zikiporwa pamoja na elimu ya uraia ambayo wamekuwa wakiipata kupitia chadema na hayo yote unayoyasema ikiwa unamini hivyo basi amini kuwa serikali ya ccm ni dhaifu katika kuongoza na ndio sababu ya chadema ndio yanayong'ara .Mwisho jaribu kuelewa nini maana ya chama kikuu cha upinzani na wajibu wake. CDM UTAIPENDA.
Yani wewe huna akili kabisa unachojaribu kutuambia ni kuwa chadema imekosea kuwaelimisha watanzania wengi ambao haki,rasilimali zao zimekuwa zikiporwa pamoja na elimu ya uraia ambayo wamekuwa wakiipata kupitia chadema na hayo yote unayoyasema ikiwa unamini hivyo basi amini kuwa serikali ya ccm ni dhaifu katika kuongoza na ndio sababu ya chadema ndio yanayong'ara .Mwisho jaribu kuelewa nini maana ya chama kikuu cha upinzani na wajibu wake. CDM UTAIPENDA.
anachojaribu kufananisha huyu mkuu ni kifo na usingizi,katu haviwezi kufanana.