Sigrada Mligo: Inashangaza wanyonge hatuungani kupambana na wenye nguvu

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Akiwakilisha kundi la Wabunge walio wachache bungeni katika msiba wa Hayati Edwin Mtei, Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHAUMMA, Sigrada Mligo, amesema busara na hekima za Mzee Mtei ni nguzo muhimu ambazo wanasiasa wanapaswa kujifunza.

“Mimi binafsi huwa natamani nipate hata robo tu ya busara za huyu mzee, nikiziangalia hata theluthi za busara za mheshimiwa Mbowe niwe nazo, lakini nimeshindwa.

Sisi kama wabunge tulio wachache bungeni, tunamuahidi kwenda kupigania demokrasia ya kweli katika nchi hii, kwenda kuhakikisha nchi hii inarudi kwenye kuheshimiana, tunajadili jambo la kitaifa kwa pamoja.

Ameendelea kusema, "Wanyonge wanatakiwa kuungana kupambana na wenye nguvu, nashangaa sana pale tunapoona wanyonge wanafinyana wenyewe.”
 
Aliungana na Chaumma na samuya, hiyo inatosha, vitu vingine sio vya kulazimisha
Ameungana lini na Samia? Unathibitisha alilosema. Badala ya kuungana kupambana na mwenye dola nyie mko busy kuwafinya wapinzani wengine ili muonekane peke yenu kama wapinzani. Bila kushirikiana na wenzenu, ndoto yenu ya kushika dola itabakia kuwa ndoto.

Amandla...
 
Huyu mligo ameahidi nini hapo?
siwaamini kabisa wana siasa, maana wana siasa kuahidi kipao mbele, kutekeleza kipao nyuma,
ndo maana mi nimechagua kuwapenda wana harakati kama TAL.
 
Akiwakilisha kundi la Wabunge walio wachache bungeni katika msiba wa Hayati Edwin Mtei, Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHAUMMA, Sigrada Mligo, amesema busara na hekima za Mzee Mtei ni nguzo muhimu ambazo wanasiasa wanapaswa kujifunza.

“Mimi binafsi huwa natamani nipate hata robo tu ya busara za huyu mzee, nikiziangalia hata theluthi za busara za mheshimiwa Mbowe niwe nazo, lakini nimeshindwa.

Sisi kama wabunge tulio wachache bungeni, tunamuahidi kwenda kupigania demokrasia ya kweli katika nchi hii, kwenda kuhakikisha nchi hii inarudi kwenye kuheshimiana, tunajadili jambo la kitaifa kwa pamoja.

Ameendelea kusema, "Wanyonge wanatakiwa kuungana kupambana na wenye nguvu, nashangaa sana pale tunapoona wanyonge wanafinyana wenyewe.”
Unawezaje kupambana na mwenye nguvu kama huwezi hata kukataa mifupa anayokutupia?
 
Ameungana lini na Samia? Unathibitisha alilosema. Badala ya kuungana kupambana na mwenye dola nyie mko busy kuwafinya wapinzani wengine ili muonekane peke yenu kama wapinzani. Bila kushirikiana na wenzenu, ndoto yenu ya kushika dola itabakia kuwa ndoto.

Amandla...
Waungane hivyo vyama vingine washike dola. Huyu si ndio alikuwa anatumika na ccm kuibomoa cdm. Alijifanya amepigwa akawa anatembelewa na akina Makala hospitalini
 
Mligo maana yake ni mzigo. Kwahiyo shingo yake imebeba mzigo wa kichwa chenye tui la nazi.
 
Yeye ameungana na wenye nguvu wenzie CCM kuiba uchaguzi kuua na kujitangaza,aache CHADEMA itaungana na wanyonge wa kweli,wananchi wa Tanganyika
 
Waungane hivyo vyama vingine washike dola. Huyu si ndio alikuwa anatumika na ccm kuibomoa cdm. Alijifanya amepigwa akawa anatembelewa na akina Makala hospitalini
Huyu dada alijidhalilisha sana!! Ubunge wenyewe kapewa tu kama hongo maana chaumma haikufikisha 5% ya kura za ubunge. Ndio eti anataka kuungana kupambana na CCM?

Wanalazimisha maridhiano ili iweje
 
Mpuuzi sana huyo dada. Hata ACT ni kama wanajisogeza karibu na cdm, maana kilichofanyika kwenye uchaguzi walioamua kushiriki ni kama wamedhalilika. Na wanajua kabisa cdm walikuwa sahihi kugomea huo uchaguzi, na wanajua kwenye hili cdm ndio wamefaidika. Cdm wasikubali umoja wa mashaka, kila mmoja apambane anavyoona, lakini kuungana na hivyo vyama project ni kutaka kuingia matatizoni.
 
Unawezaje kupambana na mwenye nguvu kama huwezi hata kukataa mifupa unayotupiwa na mwenye nguvu?
Ukiikataa peke yako hautafika popote. Kinachotakiwa ni kuwaconvince wenzako nao wakatae hiyo mifupa. Hilo ndilo analosema Sigrada.

Amandla...
 
Hata mseme nini, ni kweli Sigrada alishambuliwa na mlinzi wa Heche. Ni mtihani wa uongozi ambao Heche alifeli.
Huyu ake

Alizingua sana alipotumiwa na ccm kumtengenezea Heche kesi ya kudhuru mwili
Hata sisi tunakumbuka sana.

Amandla.
 
Ukiikataa peke yako hautafika popote. Kinachotakiwa ni kuwaconvince wenzako nao wakatae hiyo mifupa. Hilo ndilo analosema Sigrada.

Amandla...
Kumshawishi mtu ambaye akipewa hata mfupa anaridhika nao sio rahisi. Mtu ambaye haridhiki na mfupa hata ukimpa ataukataa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom