'Sigara Zimeniua' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Sigara Zimeniua'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Felixonfellix, Apr 29, 2010.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Jeneza la Mzee Albert likiingizwa kaburini huku bango la maandishi 'Sigara Imeniua' likiwa pembeniWednesday, March 03, 2010 11:16 PM
  Mvuta sigara aliyeteseka miaka mingi kutokana na magonjwa yaliyotokana na uvutaji sigara ametimiziwa matakwa yake kuwa atakapofariki jeneza lake na kaburi lake liweke maneno yanayosema 'Sigara Zimeniua'.Jeneza la mzee Albert Whittamore lilizungushwa katika mitaa ya mji wake nchini Uingereza huku likiwa limewekewa maneno 'Sigara Zimeniua'.

  Mzee Albert aliyefariki mwishoni mwa mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 85, aliacha wosia kuwa atakapofariki kaburi na jeneza lake liwekewe maneno hayo ili kuwaonya vijana wasije wakapoteza maisha yao kama alivyopoteza ya kwake kutokana na magonjwa yaliyotokana na uvutaji sigara.

  Mzee Albert aliteseka miaka mingi sana kutokana na matatizo ya mapafu, ugonjwa uliotokana na uvutaji wake uliokithiri wa sigara enzi za ujana wake.

  Bango lilitengenezwa na kuwekewa maandishi ya 'Sigara Zimeniua' kabla ya jeneza lake kuzungushwa kwenye mitaa kadhaa ya mji wa Dover uliopo kilomita 160 toka jijini London.

  Kwenye kaburi lake nako kuliwekewa bango kama hilo ambalo inasemekana litakaa hapo kwa muda wa wiki moja.

  Mzee Albert kabla ya kufariki alikuwa akiwausia vijana kuhusiana na madhara yanayotokana na uvutaji wa sigara.
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  na watakaouwawa na totoz nao waandike mabango!
   
 3. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Na watakaokufa kwa opotunistic diseases za UKIMWI ninaomba sana watoe kibali ili wale ndugu waandike Bango kubwa kabisa "UKIMWI NI MATESO KWA FAMILIA, UKIMWI HAUNA DAWA, UKIMWI NI KIFO. KABLA YA KUWA NA MPENZI PIMENI KWANZA KUPATA UKWELI WA AFYA ZENU NA KILA MMOJA AWE MWAMINIFU"
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Du..Wakuu mmekuwa kikazi zaidi...I get so much encouraged to see people such serious!...Mzee aliamua uamuzi mzuri, na Mungu atamsamehe!
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Ni kweli unaandika TOTOZ zimeniua wosia
   
 6. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  1st L mbona naona kama umechoteka hapa. Kwani ni jinsia moja tu inabeba huo ugonjwa na kuusambaza? hahaa a
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Unaweza pia andika "vidumu vimeniua"
   
Loading...