Jay One
JF-Expert Member
- Nov 12, 2010
- 16,868
- 16,771
Naunga mkono hoja, kwa hali ilivyo hatuhitaji Sensa kwa sasa, labda hadi 2030, serikali ingeshughulikia uchumi wa watu wake na maendeleo mbali mbali, idadi ya watu haina maana kwa sasa. Tuna mambo makubwa ya kitaifa kushughulikia haraka, idadi ya watu haina umuhimu hivyo kwa sasa.Katika mambo ambayo mataifa mengi yanapigana nayo kwa sasa ni kunusuru uchumi wao na kuachana na matumizi yasiyo ya lazima. Uchumi wa mataifa mengi umeathiriwa na mlipuko wa COVID 19 hali iliyopelekea hatua kadhaa za kubana matumizi kufaatwa.
Mwakani taifa letu litafanya zoezi la sensa kwa maana kwamba mabilini ya fedha yatatumika. Miongoni mwa mambo na maswali ya kujiuliza JE NI KWELI KUNA ULAZIMA WA KUENDESHA SENSA KWA DUNIA NA HALI YA SASA?
Nchi hii haijui kama kina mama wajawazito wanapoteza maisha kwa ukosefu wa huduma za afya karibu? PELEKA PESA UKAJENGE MIUNDOMBINU YA AFYA, nchi hii haijui watoto wanakaa chini? Wanasomea chini ya miti? PELEKA PESA HIZO UKAWEKE MIUNDOMBINU YA ELIMU.