Sifa za Mume mwema

Sifa za Mume mwema

Najua,lakini hko kiungo ndicho kinafanya mwanaume atambulike mbele ya Mkewe.
Huwezi kunioa ukawa na adabu zote pasi na kuwa na hko Kidude.
Madame B una maeno mengi kweli, lakini ukiingia ndani ya nyumba wewe ndio wa kwanza kugeukia upande wa pili, leo kichwa kina uma, kila siku sababu na vijisabu kisa...unaogopa duduvule
 
Last edited by a moderator:
Mambo Poa mpenzi,
sijui wewe.
Nauliza hvo sababu U mume mwema hauwezi kukamilika pasi na kuhudumia mwili wa mke.
Na mahitaji ya mke ni pamoja na Unyumba.

Pale namba nne imejieleza...ni pamoja na huduma hiyo...!
 
hawa wanaume hupatikanaje? wanaenda 'kitchen party for men' au ni wa ki-nadharia tu?
 
1. Awe mwenye kumcha Mungu


Mume mwema ni yule anayeheshimu nafasi ya Mungu katika maisha yake, anayemcha Mungu na kuepukana na uovu wa kila aina. Anatambua kwamba Mungu ndiye anayepaswa kuongoza maisha yake na si vinginevyo.
Kumbukumbu 6:5 Nawe mpende BWANA Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.

2. Mwenye kumpenda mke wake kama nafsi yake

Kumpenda mke wake zaidi ya kitu chochote iwe ni wazazi, kazi, biashara, watoto n.k. Mume mwema siku zote huthamini nafasi ya mke katika maisha yake na mara zote mke wake ni namba moja kwake.
Mwanzo 2:24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

Efeso 5: 25,28 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake,..vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.

3. Mwenye uwezo wa kuiongoza familia yake

Inashangaza kuona baadhi ya waume hawawezi kusimama kama viongozi katika nyumba zao. Wanasahau kama Mungu kawaweka kama viongozi wa familia na mke ni msaidizi wake. Utakuta wengine wanaaacha jukumu hilo kwa mkewe kwa kupenda au kwa kutokupenda na wengine wanajikuta wamewafanya wazazi wao au ndugu zao wengine kusimama kama viongozi wa familia.Biblia inaweka wazi kuwa mume ni kichwa cha ndoa, ni lazima kila mume atambue hilo na ahakikishe anasimama kwenye nafasi yake kwa uaminifu bila kujali hali yake, wadhifa, kipato, huduma au chochote kile.


Efeso 5:23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe; kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.


4. Mwenye Kuihudumia Familia Yake

Mume mwema lazima ahakikishe anafanya kazi na kuipatia familia yake mahitaji ya kila siku. Haijalishi mkewe anafanya kazi au la, yeye kama mume anajukumu la kuihudumia familia yake na hii ni sehemu ya uongozi wake. Hapa pia inajumuisha na kuilinda familia yake juu ya hatari zote na kuhakikisha wana furaha na amani ya kudumu. Ili mke na watoto waweze kuwa na amani ni lazima wahakikishiwe usalama wao kimwili, kiroho na kiuchumi.
1Timotheo 5:8 Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.

5. Mwenye kuwafundisha watoto njia inayopasa

Mume kama kiongozi wa familia anajukumu la kuwafundisha watoto njia inayofaa akisaidiana na mke wake. Waume wengi wanafikiri kazi ya kuwafundisha watoto ni ya mama wao ni kutoa tu adhabu pale wanapoona mtoto amekosea lakini hawajishughulishi katika kuwafundisha. Mume mwema lazima alitambue jukumu lake la kuwafundisha watoto neno la Mungu na misingi ya maisha ya mkristo.

Kumbu kumbu 6: 6-7 Na maneno haya ninayokuamuru leo,yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena, uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.

Efeso 6:4 Nanyi wakina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya BWANA.

6. Mwenye kumheshimu mke wake

Imezoeleka kuwa mke ndiye anayepaswa kimheshimu mume, lakini biblia inawataka pia waume kuwahepa heshima wake zao na kuishi nao kwa akili. Haipaswi mume kufanya maamuzi yoyote yanayohusu familia bila kumshirikisha mke wake, yawe madogo kama lini mgeni fulani aje hadi makubwa kama ujenzi au kuanzisha biashara. Mke ni sehemu ya mume hivyo ni lazima mume ampe heshima yake na kuthamini mawazo yake na mchango wake hata kama mke hafanyi kazi ya kuingiza kipato. Kumbuka mke anabeba jina la mume wake na ni sehemu ya mume wake, inahuzunisha kuona waume wengine wakiwadharau wake zao mbele ya ndugu zao au marafiki. Haipasi kabisa kumgombeza au kumsema vibaya mke wako mbele za watu, iwe ni ndugu, watoto au mwingine yeyote.

1Petro 3:7 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe

Asante kwa kutupatia hints za ukwenheeee.... Ngoja nimsake mwenye sifa hizo!!!!!

Barikiwa saaaaaanaaaaa!!!!!!!!!
 
:becky::becky:Ndahani kwani ulidhani sina dini?:biggrin1:

Si kwamba huna dini...la hasha...ila nikapata mashaka inawezekana ndio wale walioasi seminary...they normally go to extremes when they feel like!
 
Si kwamba huna dini...la hasha...ila nikapata mashaka inawezekana ndio wale walioasi seminary...they normally go to extremes when they feel like!

Sijawahi kanyaga hata ardhi ya seminary....!:confused2:
 
hawa wanaume hupatikanaje? wanaenda 'kitchen party for men' au ni wa ki-nadharia tu?

Hakuna kitchen party au ngoma yeyote ile iwezayo kukupa mwenza mwema wa ndoa. Mume/Mke mwema hutoka kwa Mungu

Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye,
bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Mungu

Mithali 19:14

Cha muhimu mshirikishe Mungu katika kila jambo lako. Hapo unajiongezea nafasi ya kupata mke/mume mwema.

Bali yu heri mumewe akipata mke mwema,
hata jumla ya siku zake zitakuwa maradufu.

Mwanamke hodari humfurahisha mumewe,
naye ataitimiza miaka yake katika amani.

Mke mwema ndiye tunu bora,
mcha Bwana atatunukiwa huyo kifuani pake.

Yoshua bin Sira 26:1-3

Mengi hutukuta kwa kupenda kutompa Mungu nafasi. Nani anajua zaidi ya Mungu? Tutaishia kuchagua wenza kwa sura au fedha lakini tusiipate amani wala baraka za familia. Tutambue kuwa si mpango wa Mungu kuishi kwa mafarakano ndani ya ndoa.

Kuna mambo matatu yanipendezayo,
ni mazuri mbele za Mungu na wanadamu:
umoja wa ndugu, urafiki wa majirani,
na mke na mumewe wanaopatana.

Yoshua bin Sira 25:1


 
Madame b,
Dudu, ipi maana ukubwa in relative term, Nina maana kitu Kimora kinakuwa kidogo au kikubwa kutokana na ukubwa au udogo wa Dudu nyenzake.......
 
napendwa kuzidi kazi, biashara, wazazi???
hapana asee siwezi kuusemea moyo wa mtu kwa kiwango kikubwa hivo......

Shida ni tafsiri ya kupendwa kwako. Ulinganifu wa mapenzi kwa kazi na mtu ni shida. Kupendwa zaidi ya kazi hakumaanishi mwanaume awe tayari kuacha kazi wewe utakaposema ACHA.

Umeolewa?
 
Ukwata nilipewa cheti siku namaliza form six ila sikuwahi hudhuria kipindi...................!:becky::becky:

Haaaahaaaa! Ubarikiwe mkuu....maisha yana mambo mengi sana kama haya mambo tunayofanya hapa,lol!
 
Back
Top Bottom