Sifa ya dakika moja yaweza kufanya maajabu

Sifa ya dakika moja yaweza kufanya maajabu

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
42-20699439.jpg

Sifa ya dakika moja yaweza kubadilisha kabisa maisha ya mtu

Leo ningependa kuwasimulia kisa hiki ambacho naamini wote tutajifunza.

Akiwa chuoni bado mwanafunzi wa kozi ya uhandisi Selemani Mtansi alipata kazi ya muda wakati wa likizo yake. Alipata kazi hii kwenye kiwanda kimoja cha kukata magogo na kusafirisha nje kilichoko huko morogoro. Siku moja msimamizi mkuu wa kiwanda hicho alipata dharura iliyomfanya asafiri kwa siku tatu.

Kutokana na kumwamini Sulemani alimuachia madaraka ya kuwasimamia vibarua kiwandani hapo. Labda hii ilitokana na kwamba Sulemani alikuwa mwenye elimu ya juu ukiwalinganisha na wengine waliokuwa kwenye nafasi ya kuweza kuachiwa madaraka. Lakini pia Selemani alikuwa ni mwenye nguvu.

Kabla msimamizi hajaondoka Selemani alimuuliza, 'Je kama atatokea kibarua kunibishia au kukataa amri zangu nifanyeje, kwa sababu kama unavyojua kuna vibarua wakorofi sana hapa kwa sababu mbalimbali?' lakini zaidi pengine alikuwa amelenga kibarua mmoja aliyekuwa akiitwa Popii ambaye alikuwa ni mtu wa kulalamika na kulaani huku akifanya usumbufu wa hapa na pale na kukera sana.

‘fukuza kazi tu, hakuna haja ya kumchekea mjinga'. Msimamizi alimjibu Selemani. Hata hivyo baada ya kufikiri kidogo msimamizi alimwambia, ‘nadhani unafikiria kumtimua Popii kama atakosa nidhamu, hilo bila shaka ni lazima nikiri kuwa litanikera kwani huyu kijana ni wa kuaminika sana kwa kadri ninavyo fahamu kazi hii ya magogo ambayo nimeifanya kwa miaka ishirini hadi sasa'.

Halafu aliendelea, ‘Popii ni mkorofi na anamchukia karibu kila mtu na karibu kila kitu. Lakini kama umechunguza tangu uje hapa yeye ndiye wa kwanza kuja na wa mwisho kuondoka. Hakujawahi kutokea ajali kwa miaka sita sasa tangu amekuwa hapa, na wafanyakazi wote wanakiri kwamba bila yeye ajali nyingi zingetokea. Ana uwezo wa kunusa ajali kwa njia inayowashangaza wengine'.

Selemani alianza usimamizi rasmi siku iliyofuata. Asubuhi hiyo hiyo alimfuata Popii na kuanza kuzungumza naye. ‘Popii unajua mimi ndiye msimamizi kwa leo na siku mbili zijazo?' Popii aligunia kama vile amepigwa na kitu chenye kutia maumivu. ‘Ukweli ningekufukuza kazi muda wowote ambapo tungekwaruzana kidogo tu, lakini sitafanya hivyo'. Alimwambia Popii na kumweleza kuhusu msimamizi mkuu alivyomsifu.

Selemani alipomaliza kuzungumza Popii aliweka chini msumeno aliokuwa ameushika na kuhisi machozi yanamlengalenga na baadae kumdondoka kabisa. ‘kwa nini bosi hakuniambia miaka sita iliyopita?' alimuuliza akimwacha Selemani akiwa ameduwaa.

Vibarua, wasimamizi wengine pamoja na Selemani walishangaa sana kwani baadae siku ile, Popii alifanya kazi katika kiwango cha juu na cha kutisha, kiwango mara mbili ya kile alichokuwa akisifiwa nacho. Siyo kufanya kazi tu peke yake bali alitabasamu akiwa kazini kwa mara ya kwanza.

‘Nitamsimulia mke wangu leo kwamba wewe ni msimamizi wa kwanza kuniambia kuwa mimi ni mchapa kazi, sijawahi kuambiwa hivyo na yeyote kwa miaka sita niliyofanya kazi hapa, wewe ni wa kwanza na hivyo najiona kama nimezaliwa upya' Popii alimwambia Selemani jioni ile.

Baada ya likizo Selemani alirudi chuoni kumalizia masomo yake. Miaka minne baadae alibahatika kukutana na Popii Tanga. Alishangaa pale Popii alipomjulisha kuwa alikuwa meneja kwenye kiwanda kama kile cha morogoro lakini ambacho kiko Muheza mkoani Tanga. Kutoka kibarua mkorofi hadi meneja katika kipindi cha miaka minne ni lazima mtu ashangae.

Selemani hakusita kumuuliza Popii siri ya mafanikio yake kwa kipindi hicho kifupi. ‘Kama ingekuwa siyo yale mazungumzo yako ya dakika mbili kwa siku ile asubuhi kule morogoro ni lazima kuna siku ningeuwa mtu au kujiua mwenyewe na pengine vyote. Zile dakika mbili tulizo simama nawe ukanisifia ndizo zilizobadilisha maisha yangu. Siri ya mafanikio yangu ni zile dakika mbili na kukubali kwangu kubadilika'. Alisema kwa kujiamini.

Mameneja au wasimamizi wazuri wanajua umuhimu wa kuchukua angalau dakika moja kumwelezea mtumishi au aliye chini yake namna anavyofanya kazi vizuri. Unadhani ni tofauti zipi inaweza kupatikana kwa dakika moja ya kumthibitisha mtu kwa ubora wake kwenye uhusiano wowote? Ni tofauti kubwa bila shaka.

Dakika moja au mbili tu! Je umeshawahi kutumia dakika moja kumshukuru mtu kwa utendaji wake au kwa chochote ambacho amekifanya hata kama ni kidogo? Kama bado, kumbuka kwamba unampotezea mtu huyo nafasi kubwa sana ya kubadilika, nafasi ya kumfanya naye ajue au kugundua kwamba anathaminiwa na hivyo kumfanya kutoka kwenye maisha ya ‘bora-liende'. Kama aliyokuwa nayo Popii hapo kabla.

Dakika moja ya kumfahamisha mtu kwamba alichofanya ni kikubwa na kizuri inaweza kubadili kabisa maisha ya mtu huyo. Popii alimuuliza Selemani kwamba ni kwa nini msimamizi mkuu alishindwa kumwambia maneno yale kwa miaka sita aliyokuwa akifanya kazi pale kiwandani? Kushindwa kumwambia kulimfanya kudhani kwamba hana faida na yeye ni mkorofi tu, hivyo akawa anaishi hivyo, akaamua hayo yawe maisha yake.

Watoto wetu, wapenzi wetu, watumishi wetu, jirani zetu (yaani watu tunaokutana nao popote hata kwa dakika moja) wanastahili hata dakika hiyo moja ya kupongezwa kwa kazi nzuri waliyofanya, kwani kuambiwa huko kunaweza kumfanya kuondoka kwenye udhaifu alionao na kuanza kufanya mazuri mengi kuliko mtu anavyoweza kutarajia.

Ni ukatili na kutojali wengine pale tunapoona kabisa mtu fulani anastahili sifa fulani tukanyamaza na kumsifia kimoyomoyo tu. Kwa nini mtu anapokosea tunapenda kumkosoa? Lakini lazima ufahamu kuwa kukosoa huko hakusaidii lolote zaidi ya kuzidi kumpeleka pabaya wakati kumsifu kunaweza kumbadili kabisa.
 
Hii ndio njia bora zaidi katika suala zima la uongozi.
Mwambie mtu kama ni kwa uzuri au ubaya.

Bazazi!
 
Huyo Popii nadhani tuna undugu manake haoni jema kwa hawa mabosi aiseeeee! Ila mimi hata masaa/siku/mwaka hayatoshi kunibadili mrengo wangu wa kushoto!

Life is unfair as it is!!!!! Kwanini wao wawe mabosi na sie tuwe chini yao? Ukishirikiana nao ndo unzidi kuwafanya mabosi afu wewe unazidi kuwa kidampa tu!

Marufuku urafiki wa mabosi na vidampa vyao!!!!!!!! Ukiwa kidampa hutakiwi kumrahisishia bosi kazi, analipwa hele mara 5 yako ili kutatua ugumu utakaojitokeza! So inabidi kuhakikisha Ugumu Unajitokeza mara zote ili hela anayopokea iwe halali! Baaaaaaass!

JST PUTTING THEIR MANAGERIAL ABILITIES AT TEST!!!!!!!!
 
Huyo Popii nadhani tuna undugu manake haoni jema kwa hawa mabosi aiseeeee! Ila mimi hata masaa/siku/mwaka hayatoshi kunibadili mrengo wangu wa kushoto!

Life is unfair as it is!!!!! Kwanini wao wawe mabosi na sie tuwe chini yao? Ukishirikiana nao ndo unzidi kuwafanya mabosi afu wewe unazidi kuwa kidampa tu!

Marufuku urafiki wa mabosi na vidampa vyao!!!!!!!! Ukiwa kidampa hutakiwi kumrahisishia bosi kazi, analipwa hele mara 5 yako ili kutatua ugumu utakaojitokeza! So inabidi kuhakikisha Ugumu Unajitokeza mara zote ili hela anayopokea iwe halali! Baaaaaaass!

Matatizo uliyonayo sio madogo
 
Kaka >>mtambuzi nimepata somo la maana hapa!,nimewakeup!kama nimezubaa vile,sasa nimechangamuka!!
 
Ila mimi hata masaa/siku/mwaka hayatoshi kunibadili mrengo wangu wa kushoto!
Life is unfair as it is!!!!! !
lara 1 sikujua wewe ni mkomonisti.
Lazima ukubali utofauti katika maisha ndio sababu Mungu akaumba weupe na weusi; warefu na wafupi; wanaume na wanwake.

Bila hayo hii dunia isingezunguka katika mhimili wake


Bazazi!
 
Last edited by a moderator:
Hilo kweli Anko hata Mke akipika chakula kitamu nae asifiwe ili aongeze mapishi..
 
lara 1 sikujua wewe ni mkomonisti.
Lazima ukubali utofauti katika maisha ndio sababu Mungu akaumba weupe na weusi; warefu na wafupi; wanaume na wanwake.

Bila hayo hii dunia isingezunguka katika mhimili wake


Bazazi!

Capitalist wanakuhimia its Okay kutokuwa nacho ile yeye anacho! Well ITS NOT OKAY!!!!!!! Yeye aweze ana nini na mimi nishindwe nina nini? Always try to take over your boss's position cause you can if you decide!
 
Capitalist wanakuhimia its Okay kutokuwa nacho ile yeye anacho! Well ITS NOT OKAY!!!!!!! Yeye aweze ana nini na mimi nishindwe nina nini? Always try to take over your boss's position cause you can if you decide!

That is a good arguement. Na hiyo ndiyo iliyomsaidia Popii.
Aliikubali hali yake na kutafuta njia ya kujinasua lakini baada ya kuambiwa ma mtu kuwa anaweza.
Hapo ndipo penye tofauti baina ya wanadamu; wako wanaojijua lakini wengine hadi waambiwe.


Bazazi!
 
Matatizo uliyonayo sio madogo

Matatizo labda anayo MKEO!!!!!!!! Mimi sina tatizo lolote babu wewee! Najiweka mwenyewe mjini kwa raha zangu! Upo hapo!

Back to Topic! Hiyo ideology ya Mtambuzi ni Capitalist of highest decreeee!

Kumwambia mtu its okay na ni busara kumfanyia Mtu mikazi ya ziada kwa moyo na juhudi zoteee ili upewe maneno matupu! Vry Good! Excellent! Kubwa zima linadanganyiwa sifa za kijinga! Give me a breaaaaaak!!!!!!!!!

Fanya kazi kama inakulipa kipesaaa baaaaaaaaaaass! MANENO HATA KWENYE KHANGA YAPO!

Mimi kitu kama hakipo kwenye job description hata kiwe na umuhimu gani sifanyiiiiiiiiiiii daimaaaaaa!
 
That is a good arguement. Na hiyo ndiyo iliyomsaidia Popii.
Aliikubali hali yake na kutafuta njia ya kujinasua lakini baada ya kuambiwa ma mtu kuwa anaweza.
Hapo ndipo penye tofauti baina ya wanadamu; wako wanaojijua lakini wengine hadi waambiwe.


Bazazi!

Popii jinga tuuuu! Kuewa sifa za kijingaa kidogo tu ndo kujitutumua kufanya kazi mara 2!!!!!!!!!! Pathetic!!!!! FANYA KAZI UNAYOLIPWA TUUUUU! Kujipendekeza na kujikombakomba kwa mabosi huku unajiumiza ni Utumwa mambo leo!

Mi nawaangaliaga watu ofisini huku, kinawekwa kizawadi KIFREEZER/ TV LED ya tumilioni tuwili, mnaambiwa haya chuaneni kwa performance hapo mshindi anachuku kitu hicho!!!!!!!! Mnamuingizia over 100Mills kwa ujumla wa jitihada zenu, wkt mmoja tu ndo anapata huto tu zawadi, wengine jasho limewatoka holaaaaa!

Akili ya maana hapo tukubaliane kwa list, tujipange mwezi huu wote tunamuwezeaha flani kuchukua, mwezi ujao flani hadi tunaishaaaa! Hakuna anaetoa jasho n we both win kasoro muajiri! Umoja ni nguvu! Think quicker than your boss!
 
asante mtambuzi nadhani tutafunga mwaka vizuri lakini na uvumilivu unahusika hapa maana unaweza ukakata tamaa leo kua hakuna anayerecognise kazi yako kumbe mtu kapanga akuambie kesho na kukupandisha cheo,maisha bana rahaa.................
 
Mimi kitu kama hakipo kwenye job description hata kiwe na umuhimu gani sifanyiiiiiiiiiiii daimaaaaaa!

lara bana , kama kazi unaifil kuna kugo extra mile, binadam c robot kuishia tu kwenye job descroiption , una bahati mbaya umepata bosi sio leader bt kwa maleader ukienda extra miule utafurahi mwenyewe coz lazima uwe ni sababu ya kumek changes, ingawa mabosi somitme they nid our help tu sio wasaka nyoka,
 
"Ukisifia la Tembo Mgema ulitia maji" ngoja mtu afe tumpe sifa zake,, hivi ndivyo Watanzania wengi wanavyofikiri LOL:smiling:
 
Nakubaliana na wewe kwa 87% lakini 13% nina uzoefu kidogo
::
Nimewahi kufanya kazi na bwana mmoja ambae,alifanya kazi vyema,alikuwa akiwahi kazini ila kila bosi alipomsifia ndivyo wafanyakazi wa chini yake tulivyopata tabu,kiasi kuna wafanyakazi wawili waliacha kazi tokana na utendaji wa msaidizi wa Bosi.
::
Jambo la msingi,kabla hujamsifia yule ambaye anasitahili kusifiwa inabidi umjue ni mtu wa aina gani,wapo ambao wakisifiwa huboresha utendaji wao,na wengine hudhani wanaboresha kumbe wanaharibu..ndio akina tembo akisifiwa mgema hulitia maji au akina kuku mvike kilemba utaona mwendo wake.
::
Saikolojia ya makazini inahitajika kutolewa kwa mabosi wengi ili wafanyakazi wa ngazi ya chini,wasione kazini kama tundu la simba.HOPE elimu hii utaitoa MTAMBUZI ili mimi na akina Lala 1 tusione we are used than being useful in our working places.
=
 
Mimi kitu kama hakipo kwenye job description hata kiwe na umuhimu gani sifanyiiiiiiiiiiii daimaaaaaa!

lara bana , kama kazi unaifil kuna kugo extra mile, binadam c robot kuishia tu kwenye job descroiption , una bahati mbaya umepata bosi sio leader bt kwa maleader ukienda extra miule utafurahi mwenyewe coz lazima uwe ni sababu ya kumek changes, ingawa mabosi somitme they nid our help tu sio wasaka nyoka,

Wewe mimi nimefanya kazi na mabosi maarufu sana nchi hii so dnt Talk to me abt good leadership! Leadership true definition katika private companies a good leader ni yule anae maxmise profit kwa kuminimise cost in relation to maintaining order n peace in work enviroment!

Hiyo in summary ni KUWANYONYA NYIE NA KUMUONGEZEA MUAJIRI!!!!!!!!!!! WTF!!!!

Mimi kila nikiproduce lazima nipime marginal utility ya kazi yangu! Nikiona boss anapata sana nachakachua!!!!! Haiingii akilini wewe uzalishe 100Mil alfu ulipwe 0.01% ya revenue yako na barua kibao za pongezi, miaward ya kutosha acha kwenda dinner na MD!!!!!!! Give me a breaaaaaaaak!!!!!!!!!!

Mi nikizidisha uzalishaji kidogo tu lazima nitikise kibiriti! Natoa altmatum niongezewe au naishia! Sasa mimi nishaongezewa mshahara mara 3 na sina hata mda, na kuna watu wana miaka mshahara ule ule! Kazi kunijungua si bure anapendelewa! Wanamtaka! Blah! Blah!

Kazini usipojielewa unanyonywa vibaya!!!!!!!! Nikipata big deal tu, nikijihakikishia naliclose Lazima nitingishe kiberiti, hapo muajiri chupi lazima imbaneee coz akinikeraa hakuna kuclose deal lolote, na client nampleleka kwa competititor!

Take charge of your life!
 
Back
Top Bottom