Sifa nyingine ya Augustine Mahiga: Yeye ndiye "Shahidi Y" kwenye kesi ya Uhaini ya mwaka 1982/83

Nashukuru sana kwa hii stori maana enzi zile nilikuwa darasa la tatu na gazeti lilikuwa Uhuru naishia kusomaa habari za chakubanga basi
 
Murtaza Lakha alitimkia UK baada ya kuandamwa na tuhuma za tax avoidance. Alifariki dunia mwaka 2010 huko huko Uiengereza

..Murtaza Lakha alitufungua macho baadhi yetu tukaanza kuona kwamba kumbe raia anaweza kuihoji na kui-challenge serikali.
 
JokaKuu katika kesi ya uhaini mimi nilikuwa mshabiki wa Hussein Muccadam(RIP).
Nilikuwa navutiwa sana na ujenzi wake wa hoja. Lakha of course alikuwa ni kiboko na hao ndio walioamsha watu wengi kuhusu ''taaluma ya uwakili'' na umuhimu wao katika kesi.

Bado sijaona wa kiwango cha Marhum Muccadam au Murtaza Lakha. Hawa walikuwa 'next level'
 

..Hawa mawakili walikuwa wanatetea washtakiwa tofauti ktk kesi ile.

..Kwa hiyo ni vizuri wenye kumbukumbu wakatuhabarisha kuhusu timu ya mawakili wa utetezi na washtakiwa waliokuwa wakiwatetea.

..Lakini pia kuna umuhimu wa kuwajua mawakili wa upande wa mashtaka kama William Sekule, Johnson Mbwambo, Kulwa Masaba, na wengine.
 
JokaKuu jambo la kushangaza ni kuwa kesi ilikuwa wakati wa chama kimoja, RTD, Mzalendo, Sundy News, Daily News, Uhuru na Mfanyakazi.

Gazeti kinara lilikuwa Mfanyakazi, liliandika kila neno kutoka mahakamani.
Nilishangazwa sana na uwazi kiasi kwamba hata mambo mengine nyeti yalikuwa yanaandikwa.

Nani anawakumbuka wahariri na waandishi wa Mfanyakazi! Timu ya habari ilikamailika.

Bado sikumbuki vizuri Tamim aliuawa vipi. Sijui kama ilikuwa ukomandoo au walim-set
 

..kuhusu Mohamed Tamimu.

..nadhani alikuwa Captain jeshini.

..kwa kumbukumbu zangu alifuatwa na wanausalama mahali alipokuwa anaishi.

..kama sikosei alipotoka mlangoni kuwaona waliomfuata akaamua kukimbia na kuruka ukuta wa uani alipokuwa akiishi.

..wanausalama walianza kumkimbiza na yeye alielekea eneo la barabara ya Morocco.

..alipofika barabarani akadandia gari lililokuwa limebeba bia ambapo alianza kuwarushia chupa za bia jamaa waliokuwa wakimkimbiza.

..wanausalama walimrushia risasi na kumjeruhi. Inasemekana alikimbizwa hospitali na alipofika huko alikuwa amekwisha kufa.

..kuna wanaosema Tamimu alitoroka jeshini akiwa Uganda na aliingia nchini kinyemela toka Kenya na kuanza kupanga mipango ya mapinduzi.

..Taarifa nyingine zinasema Tamimu alikuwa mlinzi wa Raisi Professor.Yusuf Kironde Lule na taarifa zake zilikuwa zinajulikana na wakubwa zake jeshini.
 
Kulikuwa uwazi wa kuandika habari na uhuru wa Mahakama kuliko sasa hivi.

Japo ilikuwa Serikali ya chama kimoja Majaji hawakuingiliwa na aliyewateua
 
True, hawa wote walikuwa na asili ya India, wapo tunao kina Prof Issa Gullam Hussein Shivji. Murtaza Lakha na Hussein Muccadam walibobea kwenye criminal litigations Shivji amebobea kwenye Katiba.

P
 
Mkuu JokaKuu,
Hao mawakili wa serikali upo sawa kasoro huyo Mbwambo siyo .
Ni Johson Mwanyika ndiye aliyekuwa wakili.
Mbwambo ni mwanahabari.
 
Nani anawakumbuka wahariri na waandishi wa Mfanyakazi! Timu ya habari ilikamailika

Kama sikosei mhariri wa gazeti la mfanyakazi wakati huo alikuwa marehemu HAMID NZOWA na huyu marehemu Richard Ndassa pia akifanya kazi kwenye gazeti lile!!
 
Ukikosa first class kwenye nini?
 

Kiongozi Jokakuu, nadhani William Sekule alikuwa ndiye DPP kwa wakati huo. Hv sasa ni jaji mstaafu. Nadhani sijakosea.
 
Ni kweli Mahiga alikuwa ni hazina kubwa sana ktk Nchi yetu ya TZ katika masuala ya Diplomasia.Ila sielewi kwa nini Mhe.Rais alimbadilisha Wizara.
Wizara ina safari nyingi sana ile na mzee wetu tayari alianza kuonesha kuchoswa na maradhi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…