Sifa na Tabia za Mtu Mvivu Pamoja na Changamoto Zake. Mvivu ni Sawa na Mchezaji Aliyechoka Kufunga Goli Wakati Golikipa Hayupo

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
Sifa na Tabia za Mtu Mvivu Pamoja na Changamoto Zake: Endapo mtu ni mvivu lakini ni mwenye afya, nguvu, hana ulemavu wowote wala matatizo ya kiakili mara nyingi huwa na sifa na tabia bainishwa zifuatazo:

1. Mtu mvivu hupenda kulala na huthamini usingizi kuliko kujituma: Mvivu yeyote hutumia muda mwingi kulala kama ilivyo nafsi yake, jua huchomoza yeye bado yupo kitandani kila siku. Usingizi kwake ni starehe. Mvivu anaependa usingizi, njaa kwake ni sawa maana hutumia muda mwingi kulala kuliko kutafuta mkate (chakula) wake wa kila siku.

2. Mvivu anatatizo la kuahirisha ahirisha kazi na mambo yake: Mtu mvivu huwa na changamoto ya kuahirisha-ahirisha kutimiza, kutekeleza mambo na shughuli zake kwa wakati. Tatizo la kuahirisha-ahirisha mambo kwa luhga ya Kingereza linaitwa “Procrastination”. Tatizo hili huwakabili watu wengi walio wavivu na huchukua sehemu kubwa ya maisha yao. Kuwaza na kusema “nitafanya tu” ndiyo kauli mbiu ya mtu mvivu mwenye tabia ya kuahirisha-ahirisha mambo, kazi, majukumu.

3. Mtu mvivu ni mzembe wa kutupwa; hata kwa vitu au kazi isiyohitaji nguvu na maarifa yeye humshinda:
Mvivu hata ukimsogezea fursa mlangoni kwake umefanya kazi bure.; hata kama fursa zipo kila mahali, mvivu hawezi kuthubutu katika kujisumbua kufanya jambo lo lote, maana yeye kila jambo kwake ni kero na usumbufu. Mtu mvivu ni sawa na mtu asiyeweza kufunga goli katika mpira wa miguu wakati mlinda mlango (goal keeper) hayupo.

4. Mvivu kutumika au kujitumakwake ni kuchungu: Daima mvivu hapendi kutumika na kujituma katika bidii ya kazi. Mvivu hukeleka na huumia pale aambiwapo kufanya kazi au kutumwa kufanya kazi, na huwa mkali au hulalamika sana apewapo majukumu ya kufanya kazi.

5. Mtu mvivu hupenda maisha rahisi, hapendi kujitesa katika bidii ya kutafuta: Mvivu hapendi kujisumbua, kujibidisha katika kazi, wala kuteseka ili hapo baadae afanikiwe na kufaidi matunda yake; bali yeye (mvivu) hupenda maisha rahisi na mepesi. Maisha ya kupanda mlima kwa mvivu ni machungu mno tena ni zaidi ya pilipili kichaa.

6. Mtu mvivu hawezi kuthubutu, kuvumilia wala kuzikabili changamoto ili ayafikie mafanikio: Mvivu ni mvivu hata katika kufikiria, hawezi kufanya kazi, biashara wala jambo lolote bila kusukumwa au kusaidiwa. Mvivu huzungukwa na mashaka, wasiwasi, pamoja na uoga uliokithiri, hivyo hawezi kuthubutu kwenye kazi au jambo linalohitaji ushupavu wa moyo, nguvu, akili na uwezo wa maarifa, pamoja na ustahimilivu kubwa.

7. Mtu mvivu huharibu, hatunzi, hutumia kwa pupa na kwa uharibifu vitu au mali zilizotafutwa na wengine: Kutokana na kutojua uchungu, mateso, usumbufu, gharama na jasho lililotoka katika kuvipata vitu au mali zilizotafutwa na watu wengine; mtu mvivu azikutapo mali hizo au vitu hivyo yeye hutapanya, hufuja, huharibu, hutumia kwa pupa na fujo (mali zilizokwishatafutwa na watu wengine).

8. Mtu mvivu ni mzigo na hunyonya wengine: Tabia ya uvivu, utegemezi, kuombeleza vitu na mali za wengine; humfanya mtu mvivu awe mzigo kwa ndugu, marafiki, jamii hata taifa kwa ujumla. Mvivu ni mzigo mkubwa na mnyonyaji kwa watu wengine wanaojibidisha katika kufanya kazi na kutafuta, wale ambao usingizi, raha wala anasa kwao hazina thamani, maana kila siku, kila saa, kila muda nafsi zao, damu zao, fikra zao huwaza na kusema “kazi tu”.

9. Mtu mvivu hupenda kufuatilia mambo na mafanikio ya wengine: Mvivu asiyefanya kazi; masikio yake, macho yake, miguu yake na mdomo wake huwa makini katika kufuatilia na kusema mambo na mafanikio ya wengine (yasiyomhusu hata kidogo). Kutokana na kukosa kazi, shughuli na mambo ya kufanya, mvivu hufuatilia ya watu wengine na kuyatapanya mtaani au kuyasambaza kwa watu wengine. Tabia hii ya mtu mvivu, huzaa tabia ya umbea, uongo, usengenyaji na kuchunguza chunguza maisha ya wengine.

10. Kazi, mali, na vitu vya mtu mvivu havipo katika utaratibu, matunzo na mpangilio maalumu: Kila jambo, kila kazi, na kila kitu cha mtu mvivu kipo ovyoovyo; hakuna matunzo, hakuna mpangilio, hakuna utaratibu. Mvivu hana kipi kianze na jambo lipi lifuatie baada ya jingine; muda gani jambo au kitu gani kifanyike na kifuatiwe na kitu gani kingine; kazi ipi ifanyike vipi, muda gani na kwa namna gani ianzwe na imalizike; kitu gani kitunzwe na kihifadhiwe kwa namna ipi?

12. Mvivu hapendi wengine wafanikiwe, anataka wabaki kama alivyo yeye: Kushindwa kwake, mvivu hutamani na wengine washindwe ama wasifanikiwe kama alivyo shindwa yeye. Kwa maana nyingine; mvivu huwaonea wivu wale wanaofanikiwa na hujenga kinyongo na chuki juu yao.

13. Mvivu anapenda sana starehe: Ku Hata kama ni mvivu kiasi gani mvivu atatokwa jasho kwenye starehe, iwe ni ofa ya pombe hata kama hana nauli yupo tayari kutembea hata kilometa 2, anaweza kusafisha chumba kikawa kisafi kweli kweli kama ana mgeni wa kumstarehesha, mvivu yupo tayari kutembea umbali mrefu kutafuta rizla za kusokotea bangi, n.k
 
8. Mtu mvivu ni mzigo na hunyonya wengine: Tabia ya uvivu, utegemezi, kuombeleza vitu na mali za wengine; humfanya mtu mvivu awe mzigo kwa ndugu, marafiki, jamii hata taifa
Ndo ubaya wa mtu mvivu.

Mengine ni juu yake
 
Umeongea ukweli mtupu. Kwasasa taifa linalea vijana wavivu kuliko wakati wowote ule. Kuna vijana sasa yupo tayari uzunguke nae kutwa nzima hadi jioni bila shughuli yoyote awe chawa wako. Mradi umtoe pesa ya msosi, na vocha. Anakuwa very comfortable.
 
Umenena kweli mkuu , uvivu ni janga.
 
Ikitokea wameoana mwanamme mvivu na mwanamke mvivu, itakuwaje?
Tuchukulie mwanaume mvivu ni M, na mwanamke mvivu na yeye ni M (maana wote wana uvivu unaofanana). Sasa hawa wawili wameoana; tunaweza kufupisha kama:
M + M = 2M
Najaribu kujiuliza, hapa hali itakuwaje?!
 
Back
Top Bottom