Sifa kuu za mnyama Mamba: Mfalme wa majini na nchi kavu

Mamba mwenye ubabe nchi kavu ni wa aina gani? Nguvu za mamba zipo kwenye mkia na miguu akiwa ndani ya maji, mamba haumi wala hatafuni, mamba kutumia nguvu kukata nyama kwa kutumia nguvu ya mkia na miguu kisha kujiviringisha ndani ya maji kisha huinua kichwa ili kipande cha nyama alichokikata kiteremke kooni na kuingia tumboni kwani hana uwezo wa kumeza kamawalivyo wanyama wengine.
Mkuu nachojua mimi kazi ya mkia wa mamba ni kuogelea na kupiga kona akiwa majini!
Na kazi ya meno ni kung'ata kwani yeye hatafuni na hujizungusha kwa ajili ya kukata kipande atachoweza kumeza

Akiwa pekeyake hupata shida sana kukata
 
Mkuu muelezee kidogo huyu NGOGO
Yule sio mamba wa kama hawa wa kwetu yule anayeuliwa na jaguar ni cayman na sio nile crocodile na nina uhakika jaguar hawezi kupambana na nile crocodile

Kiboko ya mamba ni samaki anaitwa NGOGO
 
Mkuu nachojua mimi kazi ya mkia wa mamba ni kuogelea na kupiga kona akiwa majini!
Na kazi ya meno ni kung'ata kwani yeye hatafuni na hujizungusha kwa ajili ya kukata kipande atachoweza kumeza

Akiwa pekeyake hupata shida sana kukata
Sioni tofauti na nilichoeleza japo mimi nimejikita kwenye ulaji, ili aweze kujiviringisha lazima atumie mkia wake kama nanga na kichwa na miguu kujiviringisha kwa nguvu sana mpaka mnyama akatike hivyo nchi kavu hawezi kufanya hivyo.
 
Nilipewa stori huko vijiji vya Mkuranga, mamba alimdaka mtoto nje ya mto na kukimbia naye uelekeo kwenye mto.

Kaka yake yule mtoto mwenye umri takribani miaka 7 hivi, hakukubali akamshika yule mamba mkia na kuanza kumvuta asiingie na mdogo wake kwenye maji.

Vita ilikuwa pevu, mamba anaburuza na kuyumbisha mkia lkn dogo alikomaa mwisho dogo akaona mkia unamchoropoka huku mamba anakaribia mtoni ,akaachia na kukamata mguu, mamba akaona yanini , akamuachia mtoto.

Dogo naye akaachia mguu wa Mamba na kumchukua mdogo wake lkn akiwa amejeruhiwa vibaya na domo la Mamba.
 
Mkuu muelezee kidogo huyu NGOGO

Huyu samaki ana miba kwenye kichwa chake akikutana na mamba kwenye maji mamba ana mkwepa hawezi kumla kwa maana akimla tu yani akimuingiza mdomoni anatanua miba yake na mamba anakabwa na kupelekea kufa kwa hiyo wana heshimiana mno hata binadamu ukimvua huyu samaki inabidi uwe ana miba mikali mno
 
Mkuu muelezee kidogo huyu NGOGO

Halafu huyu samaki ana supu nzuri sana,mamba ana mkamata huyu samaki endapo tu atamkuta ndani ya nyavu ya mvuvi na hapo utakuta kala mkia kaacha vichwa tu kwa hiyo mvuvi akienda kutoa nyavu mtoni anakuta kuna vichwa tu vya ngogo mamba anakua kala kiwiliwili
 
Mzee mamba mjanja sana,shukrani mkuu
Halafu huyu samaki ana supu nzuri sana,mamba ana mkamata huyu samaki endapo tu atamkuta ndani ya nyavu ya mvuvi na hapo utakuta kala mkia kaacha vichwa tu kwa hiyo mvuvi akienda kutoa nyavu mtoni anakuta kuna vichwa tu vya ngogo mamba anakua kala kiwiliwili
 
Katika heka heka zangu za kula Bata mbuga za wanyama ,tulipita kwenye mto uliokuwa na mamba wengi,familia moja ya watalii waliokuwa gari ya jirani baada ya kuona mamba mtoto wa mtalii alishangaa Sana kuona mamba akawa anamwonyesha baba yake,"Dad ,dad look at that Lacoste...😁wazungu bana...
 
Back
Top Bottom