Sifa kuu za mnyama Mamba: Mfalme wa majini na nchi kavu

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,227
16,178
Mjue Mnyama Mamba kwa undani wake

Mamba ni moja ya mnyama alaye nyama, maisha yake ni majini na nchi kavu tuu, watu wengi hufikiri mamba ni mnyama anayezaa, lakini sivyo mamba ni mnyama anayetaga na hutaga mayai kwa wastani wa 35 mpaka 50, najua utajiuliza sasa huyu kiumbe anaatamia vipi wakati maisha yake ni ya heka heka, ukweli ni huu hutengeneza kiota kwa kuchimba pembezoni mwa mto, na kisha kufukia mayai yake mpaka hapo ambapo mayai yatakapokuwa tayari.

Mayai yake yanapokuwa tayari kwa kutoa watoto, mamba husikia sauti na akiyatoa mayai hayo katika kiota watoto wake hujitoa wenyewe, yaani watoto hutumia nguvu binafsi na kuvunja gamba la yai, kisha hutoka katika ulimwengu mpyaa, kazi ya mama kwa wakati huo itakuwa ni kuhakikisha anawachukua wanaye na kuwapeleka majini, ambapo huwabeba kwa kutumia mdomo wake.

Wakati huu wanyama wote ambapo huliwa na mamba ndio wakati ambapo hulipiza kisasi, mfano kenge, mijusi wakubwa pamoja na ndege, humtegea anapopeleka watoto wa awamu ya kwanza wale wanaosaria hujeruhiwa vibaya, au kubebwa kama chakula na wanyonge wa Mamba, na mamba hujisikia tabu sana kiasi kwamba anapoibuka katika maji huwatizama kwa jicho la Shari sana.
Watoto wa Mamba ukiwaona katika udogo wao ni wanashangaza sana, hutokaa ufikirie kwamba ndio hao wafikapo ukubwani hufikia urefu wa futi 13 na zaidi, na uzito wa kilo zaidi ya 1000, ni viumbe ambao huonekana wadogo sana unaweza hisi labda ni kenge tuu.

Kwa taarifa yako Mamba ni miongoni mwa wanyama wakubwa sana duniani, meno yake yamejipanga kama msumeno, ana macho makubwa, ngozi ngumu na mkia mrefu ambao humsaidia katika kuwinda, hupendelea sana kukaa kwenye maji lakini jua lichomozapo na likaribiapo kuzama hupendelea sana kwenda kuchukua vitamin.

Ajabu la mnyama huyu ni moja, pamoja kwamba wanyama wanaokula nyama tuu ndio huishi muda mfupi, lakini yeye maisha yake ni marefu anaweza kugonga miaka 50 na zaidi kabisa, muone vile na sura yake mbaya vile vile lakini ni mnyama ambaye anafahamu anafanya nini na kwa wakati gani, Dume huwa refu na zito kuliko jike.

CHAKULA CHAKE

Chakula kikuu cha Mamba ni nyama tuu, hutafuna samaki, wanyama wadogo wadogo nk, hapo ni wakati umri ukiwa bado Mdogo, lakini umri unapoongezeka mnyama mamba humuwinda moja kwa moja nyumbu, hawa huwakamata kiurahisi kwa sababu ya ujinga wao wanapovuka MAJI au kunywa maji, Twiga anapofata maji, Nyati pia anapoenda kunywa MAJI , wakati mwingine hujaribu hata kumuwinda tembo Mdogo, lakini anapotokea mama wa tembo zoezi hill huishia hapo.

SIFA ZAKE ZA KIPEKEE

1. Jamaa ni fundi wa kuogelea vibaya mno, ana kasi kubwa sana ndani ya maji.
2. Anaweza kuishi majini na nchi kavu.
3. Mashambulizi yake ni ya kishitukiza.
4. Ana akili na mjanja sana anapomuona mnyama ambaye hana uwezo wa kucheza naye hujifanya amelala usingizi ili uingie katika maji.
5. Ndio mnyama pekee ambaye amewatafuna sana binadamu.
6. Anapoiona hatari hukimbilia katika maji haraka sana, na akifika huko anakukaribisha.
7. Hapatani na simba kabisa kwakuwa ndiye mnyama, ambaye hupenda kumbughuzi awapo mapumzikoni, hivyo wawili hawa wanapokutana ni kama watani.
8. Mamba anajua sana kuzira, hupenda kuachana na vitu vinavyomuumiza kichwa.
9. Wakati mwingine huigiza amekufa ili kuwakamata samaki wakubwa kwa urahisi, akiwa majini utaona anazunguka tuu kama anapelekwa na maji, samaki wakubwa hubaki kumshangaa.
10. Ngozi yake ni dili sana, ila ukikamatwa nayo popote duniani utashughulikiwa maana anarindwa na Sharia umoja wa mataifa.
11. Aonapo hatari hukimbilia majini na akifika tuu hugeuza kichwa chake alikotoka.
12. Mkia wake pia huutumumia kumsukumia kiumbe anayejaribu kumshangaa nchi kavu, na ukishaingia kwenye naye huja.
13.:huwa na nguvu zaidi akiwa kwenye maji, kuliko nchi kavu.
14. Ni mnyama anayeua haraka sana, tofauti na wanyama wengine walao nyama, hivyo kifo chake sio cha mateso sana kama kwa simba au chui, ila kwa mtizamaji atapata hofu Mara dufu kuliko akiona mauaji ya wanyama wengine.
15. Anaweza kunyata katika maji na kiumbe aliyepo pembeni asishituke kabisa, akiwa mwanadamu ndio kabisa atakosa habari.
16. Mamba jike hapendi mambo ya mahaba, Mara nyingi hutumia muda mwingi kulikimbia dume.
17. Madume kwa sababu ya ukubwa wao na uzito, wakati mwingine hutumia ubabe kulipanda jike lake.
18. Dume LA mamba lina msaada mdogo sana kwa jike, msaada huo hutoa pindi linapokuwa na muda wa ziada.
19. Kutafuta chakula huweza kushirikiana.
20. Ni mnyama pekee anayekula nyama na anaishi umri mrefu, tofauti na wanyama wengine ambao hula nyama umri wao wa kuishi ni mfupi, hii ni kwasababu moja tuu mfumo wake wa mmeng'enyo wa chakula upo vizuri anaweza kula hata mifupa pasina kuchagua steki tuu.
21. Wakati mwingine mamba humeza mawe lakini bado sijapata uhakika mawe hayo sababu ya kumeza ni IPI, baadhi ya watu hudai mawe hayo humsaidia katika mfumo wa umeng'enyaji wa chakula na wengine hudai humsaidia katika kuogelea.

UKIKUTANA NAYE UFANYE NINI

Ushauri wa pekee ni kukimbia tuu, kwani hakuna namna yoyote inayoweza kukufanya utoke salama, mnyama huyu ana nguvu kubwa ya mwili na ni kiumbe ambaye huwezi pambana naye hata ukiwa na silaha kwa sababu ya ngozi yake ngumu.
Epuka kukaa sehemu ambazo kuna uwezekano wa uwepo wa kiumbe huyu ni hatari sana, sehemu hizo ni kama mito iliyopo vijijini au mbugani, kaa mbali kabisa na fukwe za mito hiyo, wala usidiriki kunawa au kutaka kunywa maji yake bila ruhusa ya anayewaongoza.
images(5).jpg

1597214013843.png

1597214153437.png
 
“Mayai yake yanapokuwa tayari kutoa watoto, mamba husikia sauti na akiyatoa mayai hayo katika kiota watoto hujitoa wenyewe”.

Hiyo sauti husikika kutoka ndani ya mayai yaliyofukiwa ardhini...?
Ndio mkuu, ni uwezo aliojaliwa
 
Na mimi niliwahi kusikia kuhusu kumgusa macho yake kama amekukamata anakuachia je ni kweli kama mdau mmoja alivyouliza hapo juu?

Kuhusu nchi kavu naomba ufafanuzi kidogo maana nimewahi kusikia mamba hata awe mkubwa kiasi gani akiwa nchi kavu unaweza kumkimbizwa kama panya wala hana ujanja kabisa ila akishaingia mtoni tu rudi mbio ulikotoka. Je hii nayo ni kweli au ni chai?
 
Kuna stori za kusadikika, kuwa mamba akinasa mawindo yake (hasa binadamu) huzama naye lakini kabla ya kutokomea humwinua juu ‘mateka’ huyo eti ili kuaga (heshima ya mwisho).... hili likoje mwalimu Kashasha..?
Ninachojua huzama naye moja kwa moja mkuu. Ila binadamu ni adui mkubwa sana wa Mamba so inawezekana hilo pia maana amemkamata adui yake mkubwa
 
Na mimi niliwahi kusikia kuhusu kumgusa macho yake kama amekukamata anakuachia je ni kweli kama mdau mmoja alivyouliza hapo juu?

Kuhusu nchi kavu naomba ufafanuzi kidogo maana nimewahi kusikia mamba hata awe mkubwa kiasi gani akiwa nchi kavu unaweza kumkimbizwa kama panya wala hana ujanja kabisa ila akishaingia mtoni tu rudi mbio ulikotoka. Je hii nayo ni kweli au ni chai?
Kwenye macho ndio sehemu laini mno katika mwili wake na tumboni

Ni kweli nchi kavu sio mbabe sana ila ni mviziaji sana anapoona windo lake na akishalikamata hurudi majini haraka kwa kuwa ufalme wake mkubwa upo majini
 
30 Reactions
Reply
Back
Top Bottom