Sielewi mpango w serikali katika kuchochea maendeleo ya sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
996
1,511
Nimesoma, na nimeisikiliza kwa umakini hotuba ya Wizara ya Elimu,Sayansi na teknolojia,sijasikia wala sijaona kipengele kilichozungumzia kinagaubaga maaendeleo ya sayansi na teknolojia nchini,na katika kudadavua mchanganuo wa bajeti waziri ameorodhesha mgawanyo wa bajeti hiyo lakini sijaona fungu lililoelekezwa katika maendeleo ya sayansi na teknolojia,hata wakiniambia kwamba fungu hilo limejumuishwa katika fungu laUNESCO nakataa kwa maana fungu lile nikwa ajili ya matumizi ya kawaida na mishahara ya watendaji.

Kurasa zote waziri anazungumzia maendeleo ya elimu,hajazungumzia maendeleo ya sayansi na teknolojia,kwamba imesha jizungumzia humo ndani? Ama sielewi?,kuna ulazima gani wa kuita WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA kama hiyo Sayansi na teknolojia haijadiliwi na haipewi nafasi ya kujadiliwa na kupewa fungu?mnafeli wapi?

Kwamba hamjui umuhimu wa maendeleo ya teknolojia na sayansi katika dunia ya leo?,kwamba hamjui uchumi wa leo unategemea ukuaji wa teknolojia? Kwamba hamjui biashara za leo zinahitaji fikra shindani za kiteknolojia ili kushindana katika soko? Nani katuroga? Hebu niambie unatakaje kuukuza uchumi wan chi wakati unataka kuendele kuwa tegemezi katika teknolojia za mataifa mengine?

Ukienda pale muhimbili mshine zote za maabara,ICU,Theatre zote made in China,German,USA nk,mashine nyingine zikiharibika nchi inalazimika kumgharamia engineer wa kampuni zalishi kuja kuitengeneza ata sisi hatuna wajuzi,na ni kweli maana wenzetu wanalinda teknolojia zao kwa nguvu.

Tunashindwa hata kutengeneza bomba la sindano tiba kweli,?hii yote ni kwa sababu serikali haijaipa kipaumbele maendeleo ya sayansi na teknolojia labda nadhani kwa sababu tuna viongozi wavivu wa kufikiri ambao wanaendeshwa na taaluma zao na sio elimu zao.

Serikali iache masihara,itazame kwa umakini nchi zinazoendelea zimewekeza kiasi gani katika maendeleo ya sayansi na teknolojia,na faid aliyoipata kupitia uwekezaji huo,hata ukisoma kwa kina katika DIRA YA MAENDELEO YA SERIKALI KUFIKIA MWAKA 2025,wamepuyanga tu hawapo clear,wanazungumzia uvunaji wa gasambao ulipaswa uwe umekamilika mpaka mwaka 2022,lakoni upoupo tu hatuoni outcomes zake

Ukimsikiliza kwa umakini Mark Beare,Principal Consultant, Oxiford Policy Management,kupitia msdahalo ulioandaliwa na UONGOZI INSTITUTE, uliopewa jina “EXTRACTIVES OF HUMAN DEVELOPMENT,yenye subtitle “MAXIMIZING DOMESTICPARTICIPATION ALONG THE VALUE CHAIN” uliofanyika 27-28October 2016 Zanzibar kipindi ambacho mchakato wa mradi wa gas kule Mtwara umepamba moto, katika presentation yake alisema kwamba ili Tanzania iweze kufikia uchumi wa kati nakuwa nchi ya uchumi wa kati (MIC)basi inatakiwa kuwekeza kwa nguvu suala la uzalishaji wa gas asilia, lakini ili iweze kufanikisha hili italazimika kuwa na maendeleo bora ya TEKNOLOJIA NA MABORSHO, kushindwa kufanya hivyo kutakufanya kusuasua,na yametimia,angalia suala la gas lipolipo tu.

Ni nani katuroga?hawa maprofesa wa aina gani?,huwezi kukwepana na maendeleo ya sayansi na teknolojia katik dunia ya leo labda ukubari kuwa mpumbavu,sasa bajeti ya wizara yenye mamlaka yakuzungumzi maendleo ya elimu inasomwa,lakini hakuna sehemu wamezungumzia mikakati katika kuhakikisha Sayansi na Teknolojis inapaa.

Ndio maana COSTECH haieleweki kabisa

USHAURI WANGU NA RAHI YANGU.

Serikali Ivunje WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA ,iunde wizara 2 ambazo ni WIZARA YA ELIMU pamoja na WIZARA YA MAENDELEO YA SAYANSI,TEKNOLOJIA NA UVUMBUZI,ili kupatikane kipaumbele.
 
Hata COSTECH haijulikani wanawajibika wapi.
Hii inchi bila ya kuwa serious na Sayansi na Teknolojia,hatutafika popote.

Nakumbuka Prof. Mwamila alianzisha project yake ya kuibua na kuatamia wanasayansi vijana wa vyuo, sina hakika kama serikali walitia mkono wake pale.

Hiyo ilikuwa ni moja ya project kubwa sana ya kuiinua Tanzania kisayansi na kiteknolojia.
 
Back
Top Bottom