Boss la DP World
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 1,997
- 7,552
Vitendo vya unyanyasaji wa kingono vimeendelea kushamiri katika nchi yetu na tunategemea jamii iwe na ushirikiano katika kupinga na kutokomeza uovu huu ili kuokoa jamii yetu.
Katika hali ya kushangaza, mwanafunzi mmoja (jina linahifadhiwa) (KE) wa shule ya msingi Kilakala katika manispaa ya Morogoro amebainika kufanyiwa vitendo hivyo na ndugu zake 2 ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakimwingilia mwanafunzi huyo kinyume na maumbile.
Baada ya walimu kubaini hilo, walimshauri mzazi kuchukua hatua stahiki ambapo mtoto alipelekwa hospitali kwa uchunguzi na madaktari walibaini kuwa ni kweli mtoto amekuwa akiingiliwa hivyo alipatiwa matibabu ya awali.
Mara baada ya hatua hiyo, mzazi alikwenda kuripoti polisi na polisi walihitaji akaripoti kwanza kwenye serikali ya mtaa, kiongozi wa serikali ya mtaa akamwelekeza mzazi kuanzia kwa mwalimu mkuu.
Jambo la ajabu ni kuwa mwalimu mkuu ambaye ni mwanamama amemshauri mzazi kuwa kwakuwa mtoto amepata matibabu basi hakuna haja ya kulipeleka kwenye vyombo vya sheria hivyo kumsihi mzazi asiendelee kufuatilia.
Pia amewatisha walimu wasitoe ushirikiano kwa mtu yeyote kuhusiana na jambo hili.
Binafsi nilitegemea kuwa mwalimu mkuu ambaye ni mama angeshirikiana na mama wa mtoto kuhakikisha mtoto anapata haki yake badala yake, yeye ndiye anamshawishi kuachana na jambo hilo.
Pili nilitegemea polisi kufanyia kazi jambo hili hata kama mlolongo wa utoaji taarifa haukuwa sahihi.
Tatu nilitegemea ofisi ya serikali ya mtaa ingetoa ushirikiano kumsaidia mwananchi wake.
Nadhani mambo yamekwenda hivyo kwakuwa aliye lawitiwa si mtoto wao kwahiyo haiwahusu.