Siasa za utakatifu!

Siasa za utakatifu!

Kwahiyo unasema kwamba hata wewe huna uhakika na dhana hiyo ya kupotezwa kwa wanaopaza sauti ?

Basi tuseme wenye uhakika ni vyombo vya ulinzi lakini mbona hawatoi majibu ya kueleweka
Majibu yao sasa yalipaswa kua kwa vitendo wanaoteka watu wangefunguliwa mashtaka na
Kuwajibishwa ila hii tuhuma itoke juu utawala si ndio?
Ndugu mdau,
hiyo ni dhana tu na itabaki hivyo kwasababu hayupo wa kuithibitisha pasina shaka, na kwahivyo hakuna haja ya kupoteza wakati sana kwenye dhana, unless una mawaidha maalumu ya namna ya kuthibitisha dhana hiyo ili umma uweze kujua ni ya kweli ama vinginevyo.

changamoto kubwa kwenye mambo haya ya siasa za utakatifu ni pamoja na hata wanaoripoti changamoto kama hizo, kutoonyesha ushirikiano kwa vyombo husiaka , na matokeo yake kunakosekana na hitimisho lenye uhakika wa jambo lenyewe.

na hao wanasiasa wa kutafuta utakatifu wa kisiasa,
hawapendelei mambo haya kuhitimishwa kwasababu ndio hua mataji wao wa kisiasa. Na saa zingine huona hata ufahari endapo maafa ya kutatanisha humpata mwanachama wao. :NoGodNo:
 
Ahaaa sawa
Asante kwa maoni karibu tena
 
Kama Title inavyosema

Wengi tuna amini kuwa utakatifu ni hali ya usafi maadili mema na kutokuwa na dosari

Lakini je, nini hutokea pale ambapo dhana ya utakatifu inapohusishwa na siasa

Mimi naamini hasara zake zinaweza kuwa kwa kiwango kikubwa sana

Pale ambapo mtu au kundi la watu linaonekana kuwa watakatifu, kiasi kwamba jamii inaanza kuamini hawawezi kukosea, kukosolewa au hata kuhojiwa, matokeo yake huwa mabaya

Kwa upande mwingine, je, tatizo ni utakatifu wenyewe, au ni namna ambavyo binadamu anaweza kutumia dhana hiyo kwa maslahi yake binafsi, akijiona kuwa bora kuliko wengine?

Kwa sababu historia imeonyesha kuwa pale ambapo mtu anaaminiwa kupita kiasi na kupewa nafasi ya kuonekana hakosei, wakati mwingine inakuwa vigumu kwa jamii kuhoji maamuzi yake. Hata pale anapokosea, inaweza kuwa ngumu kuwajibishwa kwa sababu tayari kuna kundi kubwa la watu linalomwamini na kumwekea kinga

Swali la mjadala👇

Je, dhana ya utakatifu kwa binadamu ni mbaya yenyewe?

Au tatizo hujitokeza pale ambapo utakatifu unapogeuzwa kuwa kinga ya kukwepa uwajibikaji na kuzima sauti za wanaohoji?

Mnalionaje suala la siasa za utakatifu?

Unadhani linaweza kuwa chachu ya kujenga jamii yenye maadili au linaweza kuwa chanzo cha changamoto pale linapotumiwa vibaya?

Mwisho wa yote tujiulize

Je, utakatifu unapokuwa sehemu ya siasa unabaki kuwa mwongozo wa maadili au unaweza kugeuka kuwa chombo cha nguvu au ngao?

ShesRise_1 ✋️
Very philosophical and good thinking!
 
Back
Top Bottom