Siasa za utakatifu!

Siasa za utakatifu!

Hapa sasa yaweza kua ni propaganda inatengenezwa kweli kuhadaa umma au kweli ni mtoaji

Sasa namna ya kutofautisha kama huyu anafata script
Au anatoa hadharani kama kua motivated kwa wengine inabaki kwa
Anaetazama ndiyo atachagua upande kukingana na uelewa wake
Ni kweli, umewaza mbali Twin, lakini ni rahisi sana kugundua, wewe angalia tu bajeti na mifumo ya nchi, wengi huwa wanapenda sana kuonekana mbele ya camera wakiwa wanatoa hiyo misaada wakati huo huo ukiangalia upande wa taasisi utagundua mapungufu makubwa kama siyo makosa kabisa.

Lakini pia angalia ni jinsi gani huyo kiongozi anavyobeba ukosoaji, hii ndiyo njia nyepesi zaidi kugundua.
 
Ukianzisha Uzi wako unakuwa na marking scheme nini?
Pitia comment za wadau jifunze kama huna cha kuchangia idadi ya views hua kubwa kuliko wachangiaji

Sio kusema et ni propaganda
Propaganda hapo iko wapi
Thibitisha!

Ukielewa mjadala karibu tena mkuu😊
 
Ni kweli, umewaza mbali Twin, lakini ni rahisi sana kugundua, wewe angalia tu bajeti na mifumo ya nchi, wengi huwa wanapenda sana kuonekana mbele ya camera wakiwa wanatoa hiyo misaada wakati huo huo ukiangalia upande wa taasisi utagundua mapungufu makubwa kama siyo makosa kabisa.
Hii ndio tuiite cinema zetu
Mambo ya kujionesha haya
Lakini pia angalia ni jinsi gani huyo kiongozi anavyobeba ukosoaji, hii ndiyo njia nyepesi zaidi kugundua.
Hapa viongozi wengi wanaingia mkenge sana
 
Utakatifu ni illusion.

Hakuna mtakatifu chini ya ardhi na hata mbinguni
 
Hakikisha ukija kwenye uzi wangu unakuja na fact tupu

Sipendezwi sana na mtu anaechukulia mambo jumla jumla

Sasa soma tena na ukaribie kwenye mjadala😊😊
Hao nyumbu wa cdm watakuvurugia uzi.
Ngoja nitoke bank, nije ku comment vizuri.
 
Siasa chafu ina uongo, uzushi, unafiki na propaganda nyingi. Kujivika utakatifu unakozungumzia uko zaidi upande wa watawala na mnaofaidika nao. Kama hoja ni kutaka kuthibitisha tuhuma za ubadhilifu wa makamu mwenyekiti muongozo umeshatolewa.
 
Nukuu :Kujivika utakatifu unakozungumzia uko zaidi upande wa wa watawala na mnaofaidika nao!mwisho wa kunukuu.

Kuhusu mada haihusiani na upande wa mwenyekiti kabisa labda kama umeona kuna namna inaweza kufanania
 
Kama Title inavyosema

Wengi tuna amini kuwa utakatifu ni hali ya usafi maadili mema na kutokuwa na dosari

Lakini je, nini hutokea pale ambapo dhana ya utakatifu inapohusishwa na siasa

Mimi naamini hasara zake zinaweza kuwa kwa kiwango kikubwa sana

Pale ambapo mtu au kundi la watu linaonekana kuwa watakatifu, kiasi kwamba jamii inaanza kuamini hawawezi kukosea, kukosolewa au hata kuhojiwa, matokeo yake huwa mabaya

Kwa upande mwingine, je, tatizo ni utakatifu wenyewe, au ni namna ambavyo binadamu anaweza kutumia dhana hiyo kwa maslahi yake binafsi, akijiona kuwa bora kuliko wengine?

Kwa sababu historia imeonyesha kuwa pale ambapo mtu anaaminiwa kupita kiasi na kupewa nafasi ya kuonekana hakosei, wakati mwingine inakuwa vigumu kwa jamii kuhoji maamuzi yake. Hata pale anapokosea, inaweza kuwa ngumu kuwajibishwa kwa sababu tayari kuna kundi kubwa la watu linalomwamini na kumwekea kinga

Swali la mjadala👇

Je, dhana ya utakatifu kwa binadamu ni mbaya yenyewe?

Au tatizo hujitokeza pale ambapo utakatifu unapogeuzwa kuwa kinga ya kukwepa uwajibikaji na kuzima sauti za wanaohoji?

Mnalionaje suala la siasa za utakatifu?

Unadhani linaweza kuwa chachu ya kujenga jamii yenye maadili au linaweza kuwa chanzo cha changamoto pale linapotumiwa vibaya?

Mwisho wa yote tujiulize

Je, utakatifu unapokuwa sehemu ya siasa unabaki kuwa mwongozo wa maadili au unaweza kugeuka kuwa chombo cha nguvu au ngao?

ShesRise_1 ✋️
Katika jamii ya kidemokrasia kama ya kwetu hapa Tanganyika na hata kule mkoa wa kimkakati wa Zanzibari, heshima na uwajibikaji vinaweza kwenda pamoja. Tunaweza kuheshimu viongozi na taasisi zao wanazoziongoza aidha iwe kiroho, kisiasa au kijamii, huku tukidumisha haki ya kuuliza maswali hata yale wasiyoyapenda, kutoa maoni bila kuvunja sheria na kwa njia zisizo tweza utu na kuwawajibisha wanaobainika kukosea pale inapobidi kwa misingi ya sheria tulizojiweke.

Hivyo kila mchangiaji wa huu uzi,anatakiwa kuweka akilini mwake kwamba utakatifu unapokuwa chanzo cha maadili ni baraka kwa jamii na taasisi husika, lakini utakatifu unapogeuzwa kuwa ngao dhidi ya uwajibikaji na uzembe unaweza kudhoofisha haki, uwazi na imani ya wananchi. muelewa kuwa demokrasia yenye afya huhitaji maadili, lakini pia huhitaji uwazi na nafasi ya hoja tofauti zenye mashiko kusikilizwa kwa heshima.
 
Unahisi watawala au viongozi wengine wa siasa wameacha mlango wazi kukoselewa ikiwa wanaenda kinyume na maadili na sheria ?
Au wamevaa vazi la utakatifu ?
Au wakosoaji wanaonekana kuvuka mipaka ?
Hivyo kila mchangiaji wa huu uzi,anatakiwa kuweka akilini mwake kwamba utakatifu unapokuwa chanzo cha maadili ni baraka kwa jamii na taasisi husika, lakini utakatifu unapogeuzwa kuwa ngao dhidi ya uwajibikaji na uzembe unaweza kudhoofisha haki, uwazi na imani ya wananchi. muelewa kuwa demokrasia yenye afya huhitaji maadili, lakini pia huhitaji uwazi na nafasi ya hoja tofauti zenye mashiko kusikilizwa kwa heshima.
Naunga mkono 🤝
 
Kama Title inavyosema

Wengi tuna amini kuwa utakatifu ni hali ya usafi maadili mema na kutokuwa na dosari

Lakini je, nini hutokea pale ambapo dhana ya utakatifu inapohusishwa na siasa

Mimi naamini hasara zake zinaweza kuwa kwa kiwango kikubwa sana

Pale ambapo mtu au kundi la watu linaonekana kuwa watakatifu, kiasi kwamba jamii inaanza kuamini hawawezi kukosea, kukosolewa au hata kuhojiwa, matokeo yake huwa mabaya

Kwa upande mwingine, je, tatizo ni utakatifu wenyewe, au ni namna ambavyo binadamu anaweza kutumia dhana hiyo kwa maslahi yake binafsi, akijiona kuwa bora kuliko wengine?

Kwa sababu historia imeonyesha kuwa pale ambapo mtu anaaminiwa kupita kiasi na kupewa nafasi ya kuonekana hakosei, wakati mwingine inakuwa vigumu kwa jamii kuhoji maamuzi yake. Hata pale anapokosea, inaweza kuwa ngumu kuwajibishwa kwa sababu tayari kuna kundi kubwa la watu linalomwamini na kumwekea kinga

Swali la mjadala👇

Je, dhana ya utakatifu kwa binadamu ni mbaya yenyewe?

Au tatizo hujitokeza pale ambapo utakatifu unapogeuzwa kuwa kinga ya kukwepa uwajibikaji na kuzima sauti za wanaohoji?

Mnalionaje suala la siasa za utakatifu?

Unadhani linaweza kuwa chachu ya kujenga jamii yenye maadili au linaweza kuwa chanzo cha changamoto pale linapotumiwa vibaya?

Mwisho wa yote tujiulize

Je, utakatifu unapokuwa sehemu ya siasa unabaki kuwa mwongozo wa maadili au unaweza kugeuka kuwa chombo cha nguvu au ngao?

ShesRise_1 ✋️
Daud kwenye bible ndo msingi wa siasa na utakatifu, kuna jamaa alimletea taarifa eti nimemuua Sauli, Daud akasema damu yake iwe juu yako nawe utauawa. Jamaa alidhani hizo taarifa zingelimfurahisha daudi ikawa kinyume chake. Siasa na utakatifu inawezekana ukiondoa wapambe nuksi. 2 Samweli 2
 
Daud kwenye bible ndo msingi wa siasa na utakatifu, kuna jamaa alimletea taarifa eti nimemuua Sauli, Daud akasema damu yake iwe juu yako nawe utauawa.
Baada ya hapo huyo mleta taarifa aliuwawa ?
Siasa na utakatifu inawezekana ukiondoa wapambe nuksi. 2 Samweli 2
Nitanenda kusoma hiyo 2 Samweli 2
Nitakuletea mrejesho nimeona nini

Asante kwa kifungu hicho
 
Back
Top Bottom