Siasa za utakatifu!

Siasa za utakatifu!

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
16,869
Reaction score
39,941
Kama Title inavyosema

Wengi tuna amini kuwa utakatifu ni hali ya usafi maadili mema na kutokuwa na dosari

Lakini je, nini hutokea pale ambapo dhana ya utakatifu inapohusishwa na siasa

Mimi naamini hasara zake zinaweza kuwa kwa kiwango kikubwa sana

Pale ambapo mtu au kundi la watu linaonekana kuwa watakatifu, kiasi kwamba jamii inaanza kuamini hawawezi kukosea, kukosolewa au hata kuhojiwa, matokeo yake huwa mabaya

Kwa upande mwingine, je, tatizo ni utakatifu wenyewe, au ni namna ambavyo binadamu anaweza kutumia dhana hiyo kwa maslahi yake binafsi, akijiona kuwa bora kuliko wengine?

Kwa sababu historia imeonyesha kuwa pale ambapo mtu anaaminiwa kupita kiasi na kupewa nafasi ya kuonekana hakosei, wakati mwingine inakuwa vigumu kwa jamii kuhoji maamuzi yake. Hata pale anapokosea, inaweza kuwa ngumu kuwajibishwa kwa sababu tayari kuna kundi kubwa la watu linalomwamini na kumwekea kinga

Swali la mjadala👇

Je, dhana ya utakatifu kwa binadamu ni mbaya yenyewe?

Au tatizo hujitokeza pale ambapo utakatifu unapogeuzwa kuwa kinga ya kukwepa uwajibikaji na kuzima sauti za wanaohoji?

Mnalionaje suala la siasa za utakatifu?

Unadhani linaweza kuwa chachu ya kujenga jamii yenye maadili au linaweza kuwa chanzo cha changamoto pale linapotumiwa vibaya?

Mwisho wa yote tujiulize

Je, utakatifu unapokuwa sehemu ya siasa unabaki kuwa mwongozo wa maadili au unaweza kugeuka kuwa chombo cha nguvu au ngao?

ShesRise_1 ✋️
 
Utapel umejaa kila sehemu ukikutana na nature ya mtu ambaye amejijengea heshima kupitia matendo yake huwa ni rahisi kumuamini
 
Siasa za Utakatifu zinalenga katiba na sheria za haki zitakazowachochea watu kuwa Watakatifu wanapokuwa kwenye vyombo vya maamuzi, na hata wananchi wa kawaida.

Na ikitokea mtu kakosea, katiba na sheria itaweka mfumo wa hukumu ambazo ni takatifu yaani za haki.
Na hapo ndipo Uwajibikaji ndani ya siasa unapojitokeza.

Hivyo watu wanataka utakatifu hata kama wao sio watakatifu. Ili hata wahalifu na waovu wapate matunda ya utakatifu kwa kuhukumiwa kitakatifu/kihaki.

Hiyo ndio maana siasa za utakatifu.

Kukataa kukosolewa sio sehemu ya utakatifu. Hizo ni siasa za kihalifu na kishetani.

Ukosoaji ni sehemu ya utakatifu. Ili kuleta ubunifu wenye tija na mabadiliko chanya
 
Kaka hapa nadhani umeongelea faida tu na unaweza kua sahihi

Vipi kuhusu hasara ?
Mwanasiasa
Au vikundi vya siasa kujivika utakatifu
Unaopelekea kukataa maoni au kuhojiwa hiii ndio maana yangu !

Huoni kama kuna madhara hapa?

Je mwanasiasa au vikundi vya siasa vikijivika vazi la utakatifu ni kinga wanajiwekea au wanalenga hizo faida ulizotaja hapo?
 
Kimsingi, binadamu yeyote aliye hai huwa ana mapungufu na ana uwezo wa kukosea. Ndiyo maana dhana yenyewe ya binadamu kuwa mtakatifu au mkamilifu ni illusion.

Mwanasiasa anapojivika vazi la utakatifu, lengo lake huwa ni kutafuta ngao ya yeye kufanya madudu bila kuhojiwa.

Ukiangalia siasa za aina hii upande wa propaganda na vyombo vya habari utagundua ni jinsi gani huwa vinaratibiwa ili kusafisha taswira. Kila siku utaona habari zinazomwonyesha kiongozi kama mtu anayetoa sadaka, anayelia kwa ajili ya maskini, au anayeshinda na kukesha akifikiria maendeleo, hizi propaganda huwa zinatengenezwa kitaalamu ili ziwaguse wananchi emotionally, lengo likiwa ni kuwafanya hao wanachi wasipime utendaji wa kiongozi wao kwa kutumia akili bali wamtetee kwa kutumia hisia. Mtu yeyote anayepingana na hizo scripts za kusifu na kuabudu huwa anapewa jina la adui wa maendeleo.

Angalia nchi kama Zimbabwe ya Robert Mugabe. Mwanzoni alionekana kama Mkombozi Mtakatifu aliyepigania nchi yake. Watu walimwamini kiasi kwamba ikaonekana kuwa ni dhambi kubwa sana ukijaribu kumkosoa. Matokeo yake yalikuwa nini? Uchumi wa nchi uliporomoka, mfumuko wa bei ukawa wa kihistoria, nchi ikapukutika huku wananchi wakiwa bado wanamshangilia mtakatifu wao. Kila aliyetaka kuhoji alionekana msaliti wa ukombozi.

Hata hapa Tanzania, tumepitia nyakati ambazo ukosoaji ulionekana kama uhaini kwa sababu tu viongozi fulani walionekana watakatifu na wana uchungu sana na nchi. lifikia hatua ukichambua mkataba mbovu au ukikosoa matumizi mabaya ya fedha za umma, badala ya kujibiwa kwa hoja za hesabu, unaambiwa unapinga maendeleo au umetumwa na mabeberu! Jamii ikajazwa chawa wa kutosha wanaotetea makosa makubwa kwa sababu kwa mtazamo wao wanaona kiongozi hawezi kukosea.

Kifupi siasa za aina hii zinatumika tu kama ngao, wanajua wakishajenga hiyo imani, hata wakifanya ufisadi wananchi wenyewe ndio watakaopigana kuwatetea! Ni utapeli unaoua demokrasia na kuwaacha wananchi wakiwa masikini.
 
Kaka hapa nadhani umeongelea faida tu na unaweza kua sahihi

Vipi kuhusu hasara ?
Mwanasiasa
Au vikundi vya siasa kujivika utakatifu
Unaopelekea kukataa maoni au kuhojiwa hiii ndio maana yangu !

Huoni kama kuna madhara hapa?

Je mwanasiasa au vikundi vya siasa vikijivika vazi la utakatifu ni kinga wanajiwekea au wanalenga hizo faida ulizotaja hapo?
Acha kuzunguka, propaganda zimegonga mwamba.
 
Kaka hapa nadhani umeongelea faida tu na unaweza kua sahihi

Vipi kuhusu hasara ?
Mwanasiasa
Au vikundi vya siasa kujivika utakatifu
Unaopelekea kukataa maoni au kuhojiwa hiii ndio maana yangu !

Huoni kama kuna madhara hapa?

Je mwanasiasa au vikundi vya siasa vikijivika vazi la utakatifu ni kinga wanajiwekea au wanalenga hizo faida ulizotaja hapo?

Hasara ya utakatifu ipo zaidi katika mtazamo, tafsiri potofu kuhusu utakatifu iliyomo vichwani mwa baadhi ya vikundi vya watu hasahasa wenye mamlaka. Kama vile Wazazi, viongozi wa Dini/kimila na serikali.

Utakatifu kama utakatifu hauna tatizo. Ishu ipo nani anatafsiri huo utakatifu na mtazamo wa watu kuhusu utakatifu.

Kama watawala ikiwemo wazazi na viongozi wa serikali wakiwa na mtazamo na tafsiri potofu kuhusu utakatifu hapo kizaazaa lazima kizuke.

Mfano wa dhana potofu utakaoleta tafsiri potofu:
1. Mkubwa Hakosei.
Kuna ile dhana potofu kwamba Mkubwa hakosei, tumeiona mpaka kwa Miungu, kwamba Kazi yake Mola haina Makosa, au Mungu hakosei. Jambo ambalo sio sahihi katika dhana ya utakatifu.

Utakatifu haimaanishi kutokukosea kama wengi wanavyofikiri.

Dhana ya kutokosea kama sehemu ya utakatifu ndio inaleta matatizo mengi uliyoyataja. Mtu kama anaamini au imewekwa dhana ya kundi fulani halikosei. Automatically uonevu, ukandamizaji. Unyanyasaji lazima viwepo. Kundi fulani likijiona special kuliko kundi jingine.
 
Kimsingi, binadamu yeyote aliye hai huwa ana mapungufu na ana uwezo wa kukosea. Ndiyo maana dhana yenyewe ya binadamu kuwa mtakatifu au mkamilifu ni illusion.
Naunga mkono hapa
Mwanasiasa anapojivika vazi la utakatifu, lengo lake huwa ni kutafuta ngao ya yeye kufanya madudu bila kuhojiwa.
Exactly 💯
Ukiangalia siasa za aina hii upande wa propaganda na vyombo vya habari utagundua ni jinsi gani huwa vinaratibiwa ili kusafisha taswira. Kila siku utaona habari zinazomwonyesha kiongozi kama mtu anayetoa sadaka, anayelia kwa ajili ya maskini, au anayeshinda na kukesha akifikiria maendeleo, hizi propaganda huwa zinatengenezwa kitaalamu ili ziwaguse wananchi emotionally, lengo likiwa ni kuwafanya hao wanachi wasipime utendaji wa kiongozi wao kwa kutumia akili bali wamtetee kwa kutumia hisia. Mtu yeyote anayepingana na hizo scripts za kusifu na kuabudu huwa anapewa jina la adui wa maendeleo.
Hapa sasa yaweza kua ni propaganda inatengenezwa kweli kuhadaa umma au kweli ni mtoaji

Sasa namna ya kutofautisha kama huyu anafata script
Au anatoa hadharani kama kua motivated kwa wengine inabaki kwa
Anaetazama ndiyo atachagua upande kukingana na uelewa wake
Angalia nchi kama Zimbabwe ya Robert Mugabe. Mwanzoni alionekana kama Mkombozi Mtakatifu aliyepigania nchi yake. Watu walimwamini kiasi kwamba ikaonekana kuwa ni dhambi kubwa sana ukijaribu kumkosoa. Matokeo yake yalikuwa nini? Uchumi wa nchi uliporomoka, mfumuko wa bei ukawa wa kihistoria, nchi ikapukutika huku wananchi wakiwa bado wanamshangilia mtakatifu wao. Kila aliyetaka kuhoji alionekana msaliti wa ukombozi.
huu ni mfano unaoishi wenye kuonesha madhara makubwa na mabaya ya mwanasiasa kujivika vazi la utakatifu na kufunga mlango wa kukosolewa au kupokea ushauri
Hata hapa Tanzania, tumepitia nyakati ambazo ukosoaji ulionekana kama uhaini kwa sababu tu viongozi fulani walionekana watakatifu na wana uchungu sana na nchi. lifikia hatua ukichambua mkataba mbovu au ukikosoa matumizi mabaya ya fedha za umma, badala ya kujibiwa kwa hoja za hesabu, unaambiwa unapinga maendeleo au umetumwa na mabeberu! Jamii ikajazwa chawa wa kutosha wanaotetea makosa makubwa kwa sababu kwa mtazamo wao wanaona kiongozi hawezi kukosea.
Kwa hapa Tanzania hili swala nadhani limekua kama ugonjwa unaoambukiza
Binafsi naona karibia kila pande hazitaki kupokea au kusikia maoni kinzani

Hakuna tena fact ni vitisho na matusi
mpka siasa inakosa Ladha
Kifupi siasa za aina hii zinatumika tu kama ngao, wanajua wakishajenga hiyo imani, hata wakifanya ufisadi wananchi wenyewe ndio watakaopigana kuwatetea! Ni utapeli unaoua demokrasia na kuacha wananchi wakiwa masikini.
Naunga mkono hoja
 
Hasara ya utakatifu ipo zaidi katika mtazamo, tafsiri potofu kuhusu utakatifu iliyomo vichwani mwa baadhi ya vikundi vya watu hasahasa wenye mamlaka. Kama vile Wazazi, viongozi wa Dini/kimila na serikali.

Utakatifu kama utakatifu hauna tatizo. Ishu ipo nani anatafsiri huo utakatifu na mtazamo wa watu kuhusu utakatifu.

Kama watawala ikiwemo wazazi na viongozi wa serikali wakiwa na mtazamo na tafsiri potofu kuhusu utakatifu hapo kizaazaa lazima kizuke.
Upo sahihi bro
Mfano wa dhana potofu utakaoleta tafsiri potofu:
1. Mkubwa Hakosei.
Kuna ile dhana potofu kwamba Mkubwa hakosei, tumeiona mpaka kwa Miungu, kwamba Kazi yake Mola haina Makosa, au Mungu hakosei. Jambo ambalo sio sahihi katika dhana ya utakatifu.
Na hii ni dhana mbaya sana huu msemo ni wa kujivika utakatifu ambao kimsingi haupo et mkubwa hakosei🤔
Hii ni ngao ya kukwepa kuwajibika au kukosolewa
Utakatifu haimaanishi kutokukosea kama wengi wanavyofikiri.

Dhana ya kutokosea kama sehemu ya utakatifu ndio inaleta matatizo mengi uliyoyataja. Mtu kama anaamini au imewekwa dhana ya kundi fulani halikosei. Automatically uonevu, ukandamizaji. Unyanyasaji lazima viwepo. Kundi fulani likijiona special kuliko kundi jingine.
Hakika hakika
Asante kwa maoni karibu tena kaka!
 
Back
Top Bottom